Wanyama 130 wakiwemo twiga watoroshwa KIA kwenda Qatar

tusilaumu wizara... yalianza tangu mwinyi tumegawa kipande cha nchi kwa mwarabu..... what do you expect?
 
NOVEMBA 26, 2010, saa saba usiku, wakati idadi kubwa ya Watanzania wakiwa usingizini, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kulikuwa na pilikapilika kubwa ya kupakia mizigo kwenye ndege ya jeshi la anga la Qatar (Qatar Emir Air Force).

Mizigo iliyokuwa inapakiwa usiku huo mkubwa katika ndege hiyo haikuwa ya kawaida. Wahudumu walikuwa wanapakia wanyamapori hai 130 wa aina 14 tofauti na shehena kubwa ya nyamapori iliyokaushwa, mizigo hiyo yote ni inayotambuliwa kuwa kati ya rasilimali muhimu za Taifa.

Kwa mujibu wa wafanyakazi wa uwanja huo na raia wema kadhaa, wanyama hao hai 130 pamoja na shehena ya nyama zilizokaushwa vilikuwa vinatoroshwa kwenda Doha, Qatar.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, mizigo hiyo ilikuwa inaondoka nchini kinyume cha sheria kwa kuwa haikuwa na kibali wala nyaraka sahihi za kiserikali na walioshiriki katika kuratibu na hatimaye kusafirisha mizigo hiyo nao walifanya makosa ya kuhujumu Taifa.

Kati ya wanyamapori hai 130 wakiwa wa aina 14 tofauti, walikuwamo twiga wanne. Twiga hutambuliwa kama alama ya Taifa, sheria za Tanzania zinaharamisha mnyama huyo mpole kuuawa au kusafirishwa kibiashara nje ya nchi.

Shehena ya viroba vya nyamapori zilizokaushwa inaelezwa kuwa ni ya wanyama wengi waliouawa “kijangili” na mtandao wa watu wanaoendesha biashara haramu ya nyamapori.

Ndege hiyo ya Jeshi la Qatar iliwasili KIA Novemba 24, mwanzo ikionekana kama ndege iliyokuwa katika safari za kawaida hadi Novemba 26 usiku wafanyakazi uwanjani hapo waliposhuhudia ikipakia mizigo wakiwamo wanyama hai.

soma zaidi hapa.. Ufisadi Maliasili
 
Maskini Tanzania.
Tunaitaka wizara ya mambo ya ndani kuchunguza uhalifu huu. Wahusika washughulikiwe kisheria. Huyo Mhindi mshenzi kama walivo wahindi wengi sheria zichukue mkondo ikiwa ni pamoja na kufukuzwa na kutokanyaga tena Tanzania kama atapatikana na hatia baada ya kifungo chake.
Ziwekwe sheria kwa wahalifu wabaya kama hawa kunyongwa au kufungwa maisha.
Waziri aliyekuwepo kipindi hicho kama bado yuko serkalini; waziri wa utalii au wanyama pori na waziri wa mambo ya ndani wanastahili kujiuzulu haraka.
 
si tumewauzia waarabu mbuga? ndio maana uk hawataki kutupa pesa wanajua kuwa watanzania ni wajinga na wapumbavu
 
NAPE NNAUYE atalifuatilia hili na atahakikisha kila mtu aliyehusika anawajibishwa. Huyu kijana sio mchezo kwenye ufisadi. Hataki kabisa kuusikia
 
Kulikuwa na taarifa mwezi wa tatu iliyoandikwa kwamba asilimia 30 ya TWIGA wanatoroshwa kila mwezi unategemea nini tungojee semina elekezi ili kuzuia ujangili wa wanyama wetu
 
Tanzania nchi yangu mbona unapunyuliwa hivyo nawe upo kimya!! Ni lini utaamka na kushinda nguvu ya mafisadi?
 
Tume za nchi hii nyingi zimeundwa na hakuna hatua zinazochukuliwa kwani ni "Funika kombe mwanaharamu apite."

Ndugu!
Hivi Tangu uhuru hujatambua tu kazi ya Tume. kazi yao ni moja tu:-
Kufanya kazi ya kufunika ukweli!!
 
Huu ni upumbavu kabisa, hatua za haraka hazina budi kuchukuliwa kwa wote haina haja ya tume, bali washtakiwe mara moja, kama ni kutoka watatokea mahakamani. Nashindwa niseme nini kwa hasira nilizo nazo kuhusu suala hili, kwa sababu sio bure inaonekana wizi huu umeanzia mbali sana kwa karibu wizara ya utalii, tanapa, polisi, uhamiaji nk. Kama wananchi wa kawaida wakipotelea tu hifadhi wanauwawa, inakuwaje twiga asionekane? tunataka kuona mwisho wake.
 
Kuna siku member wa jf nao tutapakizwa kwenye ndege kama hizo, halafu inakwenda kubamizwa kwenye ubalozi wa yuesi ei!
 
Guardian leo wameiandika story hii pia:

Wildlife theft scam unfolds

May 29, 2011

Were it a replay of the most blood-chilling scenes in a big-time crime movie, it wouldn’t matter, because that passes for entertainment.

But when a huge plane lands on Tanzania’s second biggest airport, 140 live animals are loaded onto the mechanical bird that subsequently flies off under the glare of local operatives tasked to detect and block anomalies, mouths are left agape and eyebrows are raised.

That’s what is now happening, in the wake of the discovery that, nearly six months ago, an illegal wildlife trade syndicate smuggled the precious animals aboard a Qatar Emiri Air Force plane from Kilimanjaro International Airport (KIA).

An emerging picture shows that the aircraft had been cleared to land there, and then, in the wee hours of November 26, 2010, it took off for Doha, bearing a wildlife cargo comprising 14 species, totally valued at $113,715 (Sh170 million).

The Kilimanjaro Regional Police Commander, Lucas Ngh’omboko, says the scandal is being investigated, specifying that the Police Headquarters in Dar es Salaam is handling the assignment.

According to a preliminary police report, the deal involved six masterminds, comprising unscrupulous government officials, international traders, airport security personnel and airport ground handlers.

Smuggled trophies

The Guardian on Sunday chanced to see a Certificate of Valuation of the smuggled trophies issued by game officer Oscar Julius Lipili, which indicates that they included four giraffes, part of a species cherished, in the collective context, as the country’s national symbol.

Others were six oryx, 68 Thomson’s gazelle, two impalas, and 10 dik dik, three elands, 20 Grant’s gazelle, seven kori bustard, four ground hornbill, and two each, of Lapet faced vultures and sual cats.

In the list too were one secretary bird, five spring hares and two black verreoux eagles, according to the certificate dated 11th March, 2011, in reference to criminal case No. KIA/IR/31/2011. Police say a subsidiary smuggled cargo were several sacks of dry wild meat.

Gateway

The Kilimanjaro International Airport (KIA) is at the centre of this latest and probably the highest profile scandal of live wildlife smuggling to ever rock Tanzania in recent memory.

As a consequence, KIA is currently the focus of scrutiny by security organs, for being used as a gateway for smuggling Tanzanian trophies and other natural resources, at the expense of the nation.

The Managing Director of the Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO), a firm contracted to run KIA, Marco Van de Kreeke, confirmed to The Guardian on Sunday that indeed police investigations at KIA were underway, but exonerated KADCO of blame.

He remarked: “KADCO has nothing to do with the allegations because our key responsibility is to ensure the airport security. Cargo and passengers are normally handled by airport ground handling firms and airline operators.”

Besides security agencies, KIA, like other airports – and this is a universal phenomenon – hosts other outfits tasked with specific roles, such as the Tanzania Revenue Authority, customs department, livestock and wildlife offices.

At the very minimum, they are supposed to coalesce into a network that ensures that any property, resource or cargo that passes through the airport is backed by proper documents like permits, licences and tax compliance receipts.

The Kilimanjaro Region TRA manager, Ms Patience Minga, told The Guardian on Sunday that at the time when the purported animals were spirited out of the country, the customs office at KIA was closed.

Some offices, including that of the revenue authority, don’t operate round-the-clock. However, a former TRA officer (name withheld) who retired on June 30, 2010, is alleged to have been one of the masterminds of the scandal. Ms Minga expressed shock over that aspect.

The Managing Director for airport ground handling company, Swissport Tanzania Limited, Gaudence Temu, distanced his firm from the scam.

Speaking over the phone, he said they had explained to the police that Swissport had lent carriage tools to a firm called Equity Aviation Services, for $3000.

Equity Aviation officer in charge at KIA (name withheld) declined to comment on the matter, saying the question should be directed to her director, whose name she declined to disclose.

A one-time airport ground handling staff told The Guardian on Sunday in confidence that illegal smuggling of live wildlife to the Middle East through KIA had been conducted for a couple of years.

It is estimated that the illegal trade of wildlife is worth between $10 billion and $20 billion a year, making it the second-largest illicit market globally after drugs.

The combination of high profits and the low risk of being caught make it highly attractive to organised crimes.


SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY
 
Hii nchi ni kama gari bovu lilokosa dereva halafu linashuka mteremkoni au dereva ni kipofu.Kinacho ongozwa ni polisi kuua na kuwapiga wananchi wanapokuwa wanadai haki zao.
 
Kungekuwa na utashi wa kweli kuhusu nyara za taifa, ingewekwa sheria kwamba hakuna kushughulikia masuala ya wanyama pori, nyara zote za serikali pamoja na madini nyakati za usiku ili kudhibiti hali hii. Lakini kwa kuwa wanaofaidika na ujinga huu ni sehemu ya watanzania wenzetu waliokata tamaa kutokana na ufisadi uliojaa serikalini tutabaki na labda mpaka mwisho.

Kwani imehalalishwa kimya kimya kwamba kila mbuzi atakula kwa mzingo wa kamba yake! Ni aibu lakini haina dawa kwa sasa kutokana na serikali nzima kuoza!
 
Hi wadau

Nawaomba wabunge wote wenye nia njema na nchi yetu wafikirie pendekeo hili

Ni kuishauri wizara ya maliasili na utalii kupiga marufuku kuuza wanyama pori hai nje ya nchi. hatua hii inatakiwa ipelekwa hata k atika ngazi ya bunge la afrika mashariki na ikiwezekana hata bunge la africa.

Kwa nini ?

  • Kuuza wanayama hai wanopelekwa kwenye zoo nje ya nji ni sawa sawa na usaliti uchumi na utalii wa nchi zetu.
  • Kuuza wanyama hai wanaopelekwa nje ya nchi ni kupunguza idadi ya watalii nchini mwetu ?
  • Kama wanataka kuwekeza waje kuwekeza zoo huku.

Nini Kifanyike?

Kama Qatar au UK wanataka kuchkuwa wanyama wetu au kama ulazima wa kuwapeleka huko nchi nyingine basi tuwakodishe sio kuwauza. Tuakodishe wa gharama ambayo kila siku mnyama atakapokuwa kwenye nchi fulani serikali itaingiza pesa. haki miliki za mnyama zinabaki nchi zetu hata akizaaa.

eg kama kunalazima japo sioni basi kwa kwa kila twiga tunaweza kujachi $ 70 kwa siku kwa simba $ 100 kwa , etc . China wana wanayama wao Panda wamewakodisha wamerkani waningiza pesa kila mwaka sio mambo ya kuuza moja kwa moja..........

Kwangu hii ndo aina mikataba endelevu nayamanufaa kwa nchi zetu. Hivi hakuna aliyewai kufikiria hili. Je hakuna aliyewai kujiliza kwa nini zoo za twiga na tembo Uk iwe na mapata makubwa kuliko serengeti.


Kama wanataka kufungua zoo waje wafungue hio zoo huku kwetu. Hii mambo ya kupeleka wanyama nje ni kama Slave trade ya wanyama . teh teh teh . Sijui wenzangu mnaonaje

Wito

kama Wizara ya maliasili ina think ahead wanaweza wakaja na pendekezo hili kabla hawakoromewa na wabunge. but siashangai kuna mawazoamzuri mengi humu yanasomwa na wahusika iwe ni wabunge au serikali lakini hayawafanyiwi kazi. may be mpaka Hilary clinton ndo aje na pendekezo kama hili.

Sasa inashangaza hata wanapoamua kuwauza jumla jumla sijui kama hizoo bei wanzotumia kuuza zinazingatia kuwa kila mnyana anayeuza nje ni kupunguza mapato ya utalii ndani. Maana wangezingatia hili na hakika hawa wanyama bei zao zingekuwa ni kuuubwa mno. but kwa bei niliyoona wale twiga walipelekwa qatar inagwa sina uzoefu na mambo ya wildflife lakini ......................

Nawasilisha kwa mjadala
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom