Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Mkoa wa Bukoba uko nchi gani vile? Sikonge umeniangusha kwe..... kweli! kumbe kweli we mtu wa Tabora aiseeeeeUkweli ni kuwa haya makabila yanabebana sana sana.
Hapa Sikonge, alikuwepo Abeid Katikaza kama MD wa NBC kama sikosei. Hakufanya lolote la maana huku Sikonge na kwa Wanyamwezi kwa ujumla. Baada ya yeye kuuguwa na kuachishwa kazi, ndipo akaingia Nsekela.
Amon Nsekela, aliwabeba Wanyakyusa si kawaida. Kazi zote za ujenzi akawa anapewa baba yake Dr. Mponjoli. NBC ikawa ikihema Kinyakyusa na Kinyakyusa ikawa kama lugha ya Taifa ndani ya NBC. Yule Boss wa Kipare pale Muhimbili na yeye alijaza Wapare kibao pale na siku aliondoka, Wapare walianza kunyanyaswa sana pale. Wachaga nafikiri tatizo lao si kubebana sana kama Wahaya ila wao wakifika sehemu, wanakomba pesa kama hawana akili nzuri. Ona Mramba na watu kama yeye.
Wahaya wengi story ni kama hizo hapo juu. Wakishajazana ofinisi, ndipo zinapoanza "usinigambire Shut up kuru-public lwa watu" yaani hapo itabidi tu ujifunze Kihaya ili uweze kufanya nao kazi.
Wanyamwezi/Wasukuma ni kabila ambalo lilikuwa limelala ila wako wengi sana. Mnyamwezi akishika kazi sehemu, basi Wanyamwezi wengine anawapishia mbali. Anaona hadi kinyaa kukaa nao kuongelea mambo ya kwao au kilugha. Atashirikiana na makabila mengine huku akiwakimbia wa kwake kama ukoma. Muone mtu kama Chenge na usomi wake. Jamaa alikuwa kwenye position ya kuwa hata Rais wa Tanzania ila ndiyo hivyo tena, akaanza KUFISADI na akina Lowassa na ndiyo mwisho wake.
Hili kabila Nyerere alilitakia kila la kheri katika usingizi wake. Usingizi wa hili kabila imekuwa heri ya CCM kwa miaka mingi sana. Tangu waanze kuamka, mabadiliko mengi sana Tanzania yanaanza kuonekana. Kwa sasa ni Mwanza imeamka ikifuatiwa na Shinyanga na nina imani siku Tabora nayo ikiamka, basi patakuwa hapatoshi.
Haya Makabila mengine kama Wachaga na Wanyakyusa, idadi yao si kubwa na hivyo hata kama wamesoma (zamani) kwa sasa hiyo haionekani sana. Sanasana wako mbele kipesa. Wengi wao sasa hivi wanajenga pwani au mbali na mikoa yao. Wanyamwezi/Wasukuma ndiyo kwanza wanaanza kurudi nyumbani maana sasa hivi wamechoka kuishi mbali na kwao wakishazeeka. Mtu kama Jaji Mfwalila ni mmoja ya mifano kuwa alipozeeka, karudi hapa Sikonge.
Kuamka kwa Kabila hili, inaweza kuwa ni habari njema na habari nzuri. Kutokana na ukubwa wake kihistoria, utakuta kuwa siku zote mikoa kama Mara na Bukoba huwa inaingia kwenye kundi hili na pia mkoa wa Rukwa huwa unaingia Tabora na hapo kulifanya hili kundi kuwa kubwa zaidi. Mji wa Mwanza ni kama vile umejengwa na makabila ya hiyo mikoa ya Mara, Mwanza na Bukoba na hii imejenga ushirikiano na ujirani mwema wa makabila ya hao watu.
Wingi wa watu wa mikoa hii Mitano, siku wakiungana, nina wasiwasi itatokea kama inavyotokea nchi kama Senegal ambako kuna kundi moja kubwa sana (Mouride brotherhood -Senegal's richest and most powerful Islamic brotherhood ) ambalo liko well organised na ndiyo wamempeleka jamaa yao hadi akawa Rais.
Kwa mawazo yangu mie, kuna haja ya kuwa na kitu kiitwacho MADARAKA MIKOANI. Hii itafanya hii mikoa iwe ikishindana kwa maendeleo na siyo kama sasa hivi kuwa na Central Government. Kwa hali ilivyo sasa, ni rahisi sana siku moja akaja Mnyamwezi/Msukuma mwenye uwezo wa kuwaunganisha kama Mirambo, na akajenga kundi moja kubwa na lenye nguvu sana Tanzania na hapo kuanza kukandamiza makabila mengine ambayo kwa uchache wake, hawatakuwa na nguvu sana. Hii mikoa kwa kutumia madini yake, inaweza kuwa tajiri na kuanza kutawala wengine kwa nguvu hadi ikapelekea makabila mengine kutaka kujitenga na mwisho vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Ni jambo zuri kuliongelea na kuanza kutafuta solution mapema. Wachina wanasema "jasho jingi wakati wa amani, damu kidogo wakati wa vita". Tusiwe waoga kujadili tipic ngumu maana hali ikibadilika, tunakuwa tumejiandaa na tusiwe kama Mbuni kwa kuficha kichwa kwenye mchanga.
Please: Usiniite mie Mkabila. Maishani nimesaidiwa na watu wa makabila mengi sana na namba moja Wahaya.