Wanawake wenye uwezo kimaisha muoe,musingoje kuolewa.

Watunduru

Senior Member
Dec 29, 2011
170
39
nina rafiki yangu wa kawaida tu si kimapenzi, mwanadada mjasiriamali mama wa watoto wawili na kwa sasa ni mbunge pia,ktk bunge letu tukufu.ki maumbile si haba kwani ktk kundi la warembo nae yumo.miezi miwili iliyopita alinieleza jambo ambalo kwake alidai linamkosesha raha ktk maisha na jambo lenyewe ni kukimbiwa na kila mwanaume anaempata.alidai kuna wakati huamka usiku na kulia machozi juu ya hali hiyo kwa kujihisi mwenye balaa,na kwamba ameshazunguka kwa waganga wasio na idadi bila mafanikio.nilipojaribu kumtia moyo ikawa kama nimejipalia mkaa kwani aliongeza ukaribu na mimi mara dufu na kuanza kunichukulia kama mr wake.japo sikuwahi kukutana nae kimwili niliweza kubaini mapungufu yake ktk muda huo nikajiweka pembeni mapema kabla sijamgusa mheshimiwa.kasoro moja kubwa aliyonayo ni kumfanya mwanaume kama house boy wake,yeye ni mtu wa kutoa maagizo,maelekezo na amri hali ambayo mwanaume yoyote anaejitambua hawezi kuvumilia.nimebaini kumbe hayuko peke yake,kuna wimbi kubwa la wanawake wasomi wanaomudu maisha vizuri kutokana na ajira au biashara lakini upande wa ndoa mambo si mazuri,na walio na ndoa utagundua waume zao ni wale wanaume suruali,nikakumbuka au ndio sababu hata bosi wa mjengoni nasikia hana ndoa!?kumbe huko kote mbali,hapa jf tunao kina dada wanajitokeza kutaka waume lakini ukipitia maelezo yao utagundua ndo walewale kutokana na masharti wanayoweka.hebu tujiulize inawezekanaje mwanamke ana zaidi ya miaka 30 hajaolewa na asiwe na kasoro au hila yoyote?mimi nawapa ushauri wa bure dada zangu hawa kwamba njia pekee ya kuondokana na upweke unaowakabili ni wao ndio waoe wasingoje kuolewa.wako wanaume tegezi kwa wanawake bila kujali kama wananyanyasika au la,hawa ndio suluhisho la kudumu.ni mtazamo tu,
Karibuni kuchangia
 
Dah wapo vijana kibao wanatafuta watu kama hao lakini bahati hawana so wamsikia na ujumb wako wameupata.
wataufanyia kazi.
 
mwambie aje hapa jamiiforums,love conect kuna watu wanatafuta masugar mumy daily lol:baby:
 
  • Thanks
Reactions: KUN
Maskini mbunge! Nahisi ni mh..................................
Ila umetoa ushauri mzuri kwa kina dada lakini umesahau kuolewa ni majaliwa ya allah.

Wengine hushindwa kuolewa kwaajili ya tabia zao.
 
The world is unfair sometimes, hupati yote. Hata hivyo akiamua kuoa kweli hapo hakuna mume wa maana, naona kama mtu anazidi kujipotosha.
 
kumbe waweza kuwa na mapesa na bado ukakosa usingizi?? nilidhani ni cc masikini tu ndio hatupati usingizi, kha pole yake! ila huwa wana maringo fulani na majivuno juu, nadhani hiyo pia huchangia!
 
Ni vizuri zaidi ukawashauri wafuate misingi ya dini, kwani dini zote zinaeleza mwanaume ni nani na mwanamke amfanyie nini mwanaume katika mahusiano. Wanawake hao wenye uwezo wakielewa hilo tu mahusiano yao watayafurahia.
 
nina rafiki yangu wa kawaida tu si kimapenzi, mwanadada mjasiriamali mama wa watoto wawili na kwa sasa ni mbunge pia,ktk bunge letu tukufu.ki maumbile si haba kwani ktk kundi la warembo nae yumo.miezi miwili iliyopita alinieleza jambo ambalo kwake alidai linamkosesha raha ktk maisha na jambo lenyewe ni kukimbiwa na kila mwanaume anaempata.alidai kuna wakati huamka usiku na kulia machozi juu ya hali hiyo kwa kujihisi mwenye balaa,na kwamba ameshazunguka kwa waganga wasio na idadi bila mafanikio.nilipojaribu kumtia moyo ikawa kama nimejipalia mkaa kwani aliongeza ukaribu na mimi mara dufu na kuanza kunichukulia kama mr wake.japo sikuwahi kukutana nae kimwili niliweza kubaini mapungufu yake ktk muda huo nikajiweka pembeni mapema kabla sijamgusa mheshimiwa.kasoro moja kubwa aliyonayo ni kumfanya mwanaume kama house boy wake,yeye ni mtu wa kutoa maagizo,maelekezo na amri hali ambayo mwanaume yoyote anaejitambua hawezi kuvumilia.nimebaini kumbe hayuko peke yake,kuna wimbi kubwa la wanawake wasomi wanaomudu maisha vizuri kutokana na ajira au biashara lakini upande wa ndoa mambo si mazuri,na walio na ndoa utagundua waume zao ni wale wanaume suruali,nikakumbuka au ndio sababu hata bosi wa mjengoni nasikia hana ndoa!?kumbe huko kote mbali,hapa jf tunao kina dada wanajitokeza kutaka waume lakini ukipitia maelezo yao utagundua ndo walewale kutokana na masharti wanayoweka.hebu tujiulize inawezekanaje mwanamke ana zaidi ya miaka 30 hajaolewa na asiwe na kasoro au hila yoyote?mimi nawapa ushauri wa bure dada zangu hawa kwamba njia pekee ya kuondokana na upweke unaowakabili ni wao ndio waoe wasingoje kuolewa.wako wanaume tegezi kwa wanawake bila kujali kama wananyanyasika au la,hawa ndio suluhisho la kudumu.ni mtazamo tu,
Karibuni kuchangia

Ndoa ilitakiwa iwe ni sehemu ya furaha na sio karaha. Na ndoa huwa hailazimishwi huwa inakuja yenyewe.Kama kweli mnapendana basi mtadumu kwenye ndoa haijalishi kitu gani....Tatizo letu siku hizi tunapenda sana kumsaidia Mungu...
 
Hayo ni moja ya matatizo ya elimu na malezi!Mtu unatarajia shule ikupe ufaham matokeo yake inakuharibu.Huyo ni wakati wake wa kukaa chini na kupata ushauri ili abadilike!
 
Maskini mbunge! Nahisi ni mh..................................
Ila umetoa ushauri mzuri kwa kina dada lakini umesahau kuolewa ni majaliwa ya allah.

Wengine hushindwa kuolewa kwaajili ya tabia zao.

Mkuu hapo kwa red siyo kweli. Hapo kwa bold umenena!
 
Watunduru nimependa uzi wako maana umeongea ukweli mtupu. Hata mimi nathubutu kusema wanawake wengi wasomi na wenye kipato (ninaowafahamu) wako hivyo. Binafsi huwa najaribu kuongea nao, lakini shida yao kubwa niliyogundua ni kwamba wengi wao hawajielewi kama wako hivyo, halafu pia wanakopi mambo ya western women na kuyaleta Africa bila ya ku-edit.
 
Hizo ni tabia zao, tu hata iwe vipi ni aina ya kiburi cha mafanikio, kwani wapo wenye uwezo wao lakini wanaheshimiana na waume zao. wakumbuke kuwa utu ni bora kuliko mali wakizingatia hilo, basi watafanikiwa. Na ndio maana wengi wanao olewa ni wale wenye maisha ya kati au kawaida. kwasababu ni hulka ya wanawake wengi wenye uwezo kuwa na kiburi na kusahau kuwa mahusiono mazuri yanasehemu kubwa katika maisha ya mwanadamu hapa dunia yaani kupendwa na kupenda. ukikosa haya huna raha yoyote hata ukiwa tajiri kiasi gani na si kwa wanawake tu bali ni kwa wote.
 
Back
Top Bottom