Wanawake wengi wanapenda kuolewa, wanaume wengi wanaogopa kuoa.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,762
155,465
Huku Uswahilini kwetu wanawake wengi wanatamani sana kuolewa, lakini cha kusikitisha vijana wengi wa kiume wanaogopa kuoa. Hivi nini huenda ikawa inasababisha hali hii?
 
Hii ndio inafanya watu waamini wanawake ni wengi kuliko wanaume kumbe sio ila wanaume waoaji ndio wachache na wanawake wanaotaka kuolewa ni wengi mno.
 
Halafu hii tabia ya wanawake kuwazoea waume zao mapema inawakatisha tamaa. Unachumbia mtoto akiwa na heshima pengine anakupa shikamoo. Owa tu baada ya mwezi mmoja anakuwa yeye ndie mwenye sauti na hapo tena ndio kafunguliwa kila kitu.
 
Huku Uswahilini kwetu wanawake wengi wanatamani sana kuolewa, lakini cha kusikitisha vijana wengi wa kiume wanaogopa kuoa. Hivi nini huenda ikawa inasababisha hali hii?
Kwa tamaduni za kibantu imekuwa kawaida mwanamke kuwa tegemezi katika hawa wanandoa wawili, kwahiyo mabinti wengi wanataka kuingia katika ndoa ili wapate unafuu wa maisha. Kwani wanajua kama mwanaume anaamua kuoa basi huenda atakuwa amejiweka sawa au ana shughuli ya kumwingizia kipato. Sasa basi kwa upande wa wanaume wao inapofikia suala la kuoa inakuwa ngumu kwani anajua familia itaongezeka akijua hali ngumu ya maisha.
 
Kwa tamaduni za kibantu imekuwa kawaida mwanamke kuwa tegemezi katika hawa wanandoa wawili, kwahiyo mabinti wengi wanataka kuingia katika ndoa ili wapate unafuu wa maisha. Kwani wanajua kama mwanaume anaamua kuoa basi huenda atakuwa amejiweka sawa au ana shughuli ya kumwingizia kipato. Sasa basi kwa upande wa wanaume wao inapofikia suala la kuoa inakuwa ngumu kwani anajua familia itaongezeka akijua hali ngumu ya maisha. Kwahiyo mambo yako hivyo. Vijana wengi kwa sasa wanaogopa kuingia katika ndoa, wengine wanaamua kuingia katika ndoa kwa kushinikizwa na wazazi wao.
 
usanii umezidi...dada zetu fresh wakati bado hamja oana...akishaingia ndani basi nyodo. alafu wengine nao wanataka kuolewa ili watoe mkosi tuu na sio ili kweli wawe wake.
 
Hii ndio inafanya watu waamini wanawake ni wengi kuliko wanaume kumbe sio ila wanaume waoaji ndio wachache na wanawake wanaotaka kuolewa ni wengi mno.

We mbona umjichanganya mwenyewe sasa! Yaani ni kama umetoa hela kutoka kwa pochi, umeiweka kifuani kwenye sidiria halafu unaitafuta eti imeenda wapi hela yako!
 
Wanawake wanaolewa kwa kuiga flani kaolewa na wao wanataka tofauti kwa wanaume.
 
Hyo ilikuwa zamani siku hizi wanawake wengi hawapendi kuolewa coz hawataki kubanwa banwa.
 
Halafu hii tabia ya wanawake kuwazoea waume zao mapema inawakatisha tamaa. Unachumbia mtoto akiwa na heshima pengine anakupa shikamoo. Owa tu baada ya mwezi mmoja anakuwa yeye ndie mwenye sauti na hapo tena ndio kafunguliwa kila kitu.

Duh! Hiyo ya kumuamkia mume shikamoo kama unamuamkia baba ngumu, lol! Eti shikamoo ...
 
hii ndiyo sababu
 
Attachments

  • 558715_3649058777525_2133693664_n.jpg
    558715_3649058777525_2133693664_n.jpg
    22.2 KB · Views: 137
Back
Top Bottom