Wanawake wanaweza, wengi tunabisha kishabiki tu………………..

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Mwanamke akipewa nafasi anaweza mengi ambayo mwanaume hayawezi linapokuja suala la mtu kupata kile anachokihitaji maishani wake. Mwanamke ndiye mwenye subira kuliko mwanaume,ndiye msamehevu kuliko mwanaume, ndiye mweka akiba mzuri kuliko mwanaume, ndiye mpangaji mzuri kuliko mwanaume.

Ni mara chache kukutana na mwanamke asiyejua bajeti, hata kama anafanya bajeti kwa ajili ya kununua vipodozi. Hata ukiangalia vijana wawili wanaoanza maisha baada ya masomo. Yule wa kike na wa kiume, ambao wanapata mshahara sawa. Utakuta kwamba yule wa kike atamudu kununua vifaa vya ndani haraka zaidi kuliko mwanaume. Unawezakusema ni kwa sababu anahongwa au kusema ni kwa sababu wanawake wanapenda samani na mapambo.

Lakini tafiti nyingi zimethibittisha kwamba, mwanamke ni mzuri sana katika kuyaelekea malengo yake, anakuwa na subira zaidi wakati wa kuelekea malengo yake na anajua afanye nini ili mambo yaende sawa katika mazingira ambayo mwanaume anababaika, hasa katika uhusiano, na ndio chimbuko la msemo huu wa, ‘nyuma ya kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke.’ Hii ina maana kwamba. Mwanaume, hata angekuwaje , mafanikio yake yangetegemea sana ana mwanamke wa aina gani karibu yake.

Ukiona mwanaume amefanikiwa, ujue wazi kwamba, mwanamke aliye nyuma yake, awe ni mkewe, rafiki au mshauri wake, ndiye chachu ya mafanikio hayo. Kwa wanaume ambao hawawaamini wake zao kiasi cha kutowashirikisha kabisa kwenye mipango ya maendeleo na masuala mengine ya kifamilia, wanatakiwa kuanza kufanya hivyo. Mpe nafasi ashindwe kwanza. Na hata akishindwa, mjaribu tena kwa njia nyingine, labda anaweza kumudu.

Wanaume wanaojibebesha kila jambo, mara nyingi hukwama na kurejea kwa wake zao na kusema, ‘fanya maarifa tuweze kula.’ Wakiwa na njaa, wanagundua kwamba, wanawake ni wazuri sana kwa mikakati wa kuwezesha mambo kunyooka. Wanaume wote walioamua kuwashirikisha wake zao kikamilifu katika masuala yote ya familia, wana ahueni kubwa sana.
 
ila mkuu sio kwamba huwa hata kwenye familia unakuta bajeti ya mtoto wa kike huwa iko juu kuliko wa kiume hiyo sio inawafanya hata mambo mengine wanayamudu..
 
Hakuna ubishi ktk hili na kwa kweli dunia bila wanawake ingekwisha mapema sana, pengine Yesu na mtume SAW wangekuwa wanahubiria miti tu. Lakini pamoja na yote hayo bado vidume huwa hatuthamini sana mchango wao, until the last moment
 
Mwanamke akipewa nafasi anaweza mengi ambayo mwanaume hayawezi linapokuja suala la mtu kupata kile anachokihitaji maishani wake. Mwanamke ndiye mwenye subira kuliko mwanaume,ndiye msamehevu kuliko mwanaume, ndiye mweka akiba mzuri kuliko mwanaume, ndiye mpangaji mzuri kuliko mwanaume.

Ni mara chache kukutana na mwanamke asiyejua bajeti, hata kama anafanya bajeti kwa ajili ya kununua vipodozi. Hata ukiangalia vijana wawili wanaoanza maisha baada ya masomo. Yule wa kike na wa kiume, ambao wanapata mshahara sawa. Utakuta kwamba yule wa kike atamudu kununua vifaa vya ndani haraka zaidi kuliko mwanaume. Unawezakusema ni kwa sababu anahongwa au kusema ni kwa sababu wanawake wanapenda samani na mapambo.

Lakini tafiti nyingi zimethibittisha kwamba, mwanamke ni mzuri sana katika kuyaelekea malengo yake, anakuwa na subira zaidi wakati wa kuelekea malengo yake na anajua afanye nini ili mambo yaende sawa katika mazingira ambayo mwanaume anababaika, hasa katika uhusiano, na ndio chimbuko la msemo huu wa, ‘nyuma ya kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke.' Hii ina maana kwamba. Mwanaume, hata angekuwaje , mafanikio yake yangetegemea sana ana mwanamke wa aina gani karibu yake.

Ukiona mwanaume amefanikiwa, ujue wazi kwamba, mwanamke aliye nyuma yake, awe ni mkewe, rafiki au mshauri wake, ndiye chachu ya mafanikio hayo. Kwa wanaume ambao hawawaamini wake zao kiasi cha kutowashirikisha kabisa kwenye mipango ya maendeleo na masuala mengine ya kifamilia, wanatakiwa kuanza kufanya hivyo. Mpe nafasi ashindwe kwanza. Na hata akishindwa, mjaribu tena kwa njia nyingine, labda anaweza kumudu.

Wanaume wanaojibebesha kila jambo, mara nyingi hukwama na kurejea kwa wake zao na kusema, ‘fanya maarifa tuweze kula.' Wakiwa na njaa, wanagundua kwamba, wanawake ni wazuri sana kwa mikakati wa kuwezesha mambo kunyooka. Wanaume wote walioamua kuwashirikisha wake zao kikamilifu katika masuala yote ya familia, wana ahueni kubwa sana.

...mwanaume ni kichwa, mwanamke ni moyo....!
mwanamke "anaweza" kuishi bila mwanaume...

je? mwanaume anaweza kuishi bila mwanamke?

hapo umesema sawa kabisa. Ni vizuri kuwashirikisha wake zetu katika mambo mbalimbali tufanyayo. Utakuta mtu ni mfanyabiashara mkubwa lakini mkwewe hajiu lolote kuhusiana na biashara ile. Ikitokea mwanaume kafa na biashara nayo inakufa na familia nzima inaanza kuteseka.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom