Wanawake wanataka wenye...

Basi angalau aonekane ni hard worker hapo mbeleni future itakubali tu kwa ushirikiano wa watu wawili Eiyer mie napita tu hapa Ingawa si wote wako kama unavyodhani....:A S-rose:

Mbona mimi nina machungu sana ya kazi na wananikataa?Ni kweli sio wote wapo kama nikivyosema ila wengi wapo hivyo . . . .
 
Kumbe wewe darasa la saba hee!!lakini unaweza ukampata mtu mwenye upendo wa dhati na asiangalie elimu.Sisi enzi zetu ilikuwa haijalishi kwa sababu darasa la saba ilikuwa poa tu unamkontrol unavyotaka na pia unajaribu kumwendeleza .Mbona elimu ni ela yako tu.Pia wasichana wajue umaskini si kilema ni hali tu na unaweza kumwondoka mtu kama kuna juhudi kwani tumeshuhudia matajiri wengi tu hawakusoma ni determination tu na juhudi ya kazi huku ukidhamini unachokifanya

Wewe ulidhani mi nimesoma mpaka wapi vile?
 
ngoja nimwite Erickb52 ( MoD wetu wa ukweli) aje akulambe ban kwa kuongea mitusi,kha!
Bishanga mitusi unalala nayo nyumbani kwako hapa naaongea kiswahili fasaha kabisa. ama kwa kiingereza niseme sexual intercourse, love making, dating, they all mean penetration of man's penis into a vagina.
 
Last edited by a moderator:
mimi nasema kwa upande wangu,mambo ya hela siyafagilii.mbona uwezo wa kuzitafuta mwenyewe ninao,ni ku work hard tu.kipato ninachokipata nashukuru mungu,kwani maisha niliyokulia ilikuwa dhiki tupu,kula ndani ilikuwa ikitupiga chenga.namshukuru mama,kwa kila kitu.kuhusu suala la mapenzi,sijali mvuto naangalia tabia,uaminifu na uwe unajali,majisifu na dharau ya kumuona asiekuwa nacho kuwa sio mtu huwa sipendi. na moyo kama umependa.maybe chaguo langu ni uwe mrefu basi,maana na mimi twiga anasingiziwa

Hawa viumbe wa aina hii hawapo siku hizi!Unatudanganya tu nyie ndo hamfai kabisa!
 
gfsonwin mkianzia wote chini, hiyo ni tofauti; tena mara nyingi mkija kufanikiwa wengi wa wanaume husahau mlipotoka na kutafuta vimodel kwamba ndio hadhi yao at that moment.

Lkn mwanamke akiwa juu, chances kubwa sana ya ndoa kuwa na matatizo. Too bad kila mtu anahitaji mapenzi lkn isingekuwa hivyo, kuliko kugamble looking for an 1 understanding man among 10, bora kuwa mwenyewe!
Kaunga, mimi sikubaliani na wewe kwanba ni "heri uwe peke yako". Je, wewe waweza kuishi peke yako?
 
Last edited by a moderator:
Najua mtanibishia sana,lakini ukweli wa kile ninachokishuhudia na kinachotokea kinawatia hatiani. . . . .

Niliwahi kuwa na uhusiano wakati fulani na Luteni wa JW,lakini kabla uhusiano wangu ule na yule dada haujashika kasi niliamua kumwambia ukweli yule dada kunihusu,bahati nzuri sikua na elimu aliyokua akihitaji yule dada,na pia kingine ambacho sikua nacho ambacho alihitaji niwe nacho ni pesa,uhusiano wetu ulikufa siku ileile,usishangae nilivyosema bahati nzuri,we hujui kujua mtu ni wa hovyo mapema ni bahati,alinieleza wazi hawezi kuwa na mtu mwenye elimu kama yangu halafu asiekua na hela,nilicheka sana,wadada wa aina hii nimekutana nao wengi,wengine hawasemi lakini unajua tu . . . . . . Tangu mwaka uanze mpaka leo nimeshuhudia mahusiano kumi tofauti yakifa yangali machanga,na yamekufa baada ya wadada kugundua wanaume walionao,hawana hela wala elimu kubwa.

Lakini pia najua mahusiano zaidi ya matano ambayo yanaendelea lakini wanaume wale wamewadanganya wanawake kuhusu kipato na elimu.Je wanawake mnapenda uongo? . . . . . Ukweli ulio wazi ni kuwa,wanawake hawawataki wanaume kama mimi wasio na elimu wala pesa.Najua mtakuja na ubishi wenu hapa na maisha yenu ya mdomoni msiyoyaishi ya kudai eti mnataka mwanaume mwenye upendo wa dhati wakati mnajua ni uongo.

Mwanamke anataka mwanaume mwenye hela, elimu kubwa na sura kama ya mdoli.

Hayo ya upendo na kumjua Mungu ni uongo. Hebu nenda Love Connect (hua naiona kama chit-chat) uone kama sisi wa darasa la saba na tunaishi kwa vibarua kama tuna nafasi. Tukiacha mizaha ya love connect, Ukweli ndo huo, hayo ndo yanayotokea mitaani, ukija huku wanajidai nataka mwanaume mwenye upendo mengine mungu atatupa,ukikutana nae mtaani anakuangalia juu chini kisha anakuhoji elimu na kazi unayofanya,mkiachana unaona simu hapigi tena wakati kabla hajajua kuhusu hayo ya kazi na elimu,sms na simu mpaka zilikua kero(nina watu wa3 yamewatokea).

Mimi kwa mfano,sijazoea kudanganya,waliopata kukutana nami wanajua,ninakuambia ukweli,mimi ni darasa la saba,kama unasepa usepe,sina sababu ya kudanganya,mara niazime gari sijui nguo!

Nakuambia wazi nakaa uswazi,nyumba haina bafu,ukitaka kuoga unasubiri usiku,choo pasport size,huwezi tembea,niache atakaeona upendo ndo mpango mzima atakua nami.

Kama hujiamini utaishi maisha fake sana. . . . . . . . All an all wanawake 98% wanataka wanaume wenye hela na elimu kubwa,ila watu hawa wamegeuka kilio kwa akina dada baada ya hao jamaa kutokua waaminifu.

Huo ndio UKWELI hata mkibisha!Action speaks than words!!!!

Kwa jinsi ulivyolalamika hapa kwanini usiende kusoma, na kutafuta hizo pesa mkuu.....:A S confused:
 
Angalia ulichosema halafu uone kama sijaelewa!

basi sentensi yangu kumbe ni tungo tata nisamehe. Nilimaanisha nikukaribishe ili uone jinsi ambavyo shemejio anafaidi maupendo na siyo kwa rum kama ambavyo it can mean on the other hand. kwa kiswahili cha kitaa yaani uje ufaidi kwa macho tu
 
Ukweli ni kwamba, wanawake wengi mimi included tunataka mwanaume ambaye anakupenda na he can take care of you, financially na kimawazo na kimtazamo; hivyo basi tungeprefer au tunadream kuwa awe na uwezo kukuzidi (kama wewe unao any), elimu/uelewa wa mambo kukuzidi n preferable hata akuzidi walau miaka 2.

Ukipata unaye mzidi hivyo vyote juu, hata kama unanpenda kiasi gani, kama uelewa wake mdogo ndoa huwa na shida sana. Nami nimeshashuhudia my friends ambao ndoa zimevunjika coz mwanaume hajiamini na kuamua kuwa physical just to prove yeye ndie man of the house.

I was in a sort of the same relationship, sikumzidi pesa, but elimu na mafanikio; siwezi rudia bora niwe peke yangu aisee!

Sikatai, kuna baadhi yetu tunakuwa na nyodo lkn ni wachache sana kuliko wanaume mnavyopenda kujiaminisha ktk story zenu kiasi kwamba mnaanza kujihami kwa ubabe usio na kichwa wala miguu.

Kuhitimisha nasema, wanawake hatupendi kudanganywa but tunahitaji mwanaume tunayeweza mtegemea!

Hapa kwenye uelewa mdogo nadhani ni tatizo kubwa.Wanaume wengi uki-compare na wanawake wana uelewa mdogo sana tena hawajiamini....
 
Kaunga, mimi sikubaliani na wewe kwanba ni "heri uwe peke yako". Je, wewe waweza kuishi peke yako?

Si kuna madildo jamani. Tena siku hizi hadi life size silicon robot unapata, ngoja nitakuwekea kwenye jukwaa la wakubwa!
 
Last edited by a moderator:
mwanaume unaemzidi kwa kila kitu hafai, huta kaa uenjoy raha ya mapenzi, wanajistukia kwa kila kitu ni balaa tupu

sasa uwe na kazi inayokulazimu usafiri safiri mmh utajuta, bora wa kukuzidi elimu ukamzidi pesa kidogo mnaweza elewana
 
Eiyer mdogo wangu wa moyoni pole sana kwa yaliyokukuta.Nianze kwa kucomment kwenye uandishi ungeiwekea paragraph ingekaa vizuri kweli na kusoeka kwa raha zaid.

back to the point duniani kotwe miye huwaga naasema kuna mapenzi ya aina 2 tu katka mahusiano ama yawe mapenzi ya kweli ama yawe mapenzi feki. matamanioa siyaguzi kabisa wala siyapi nafasi amanke yaweza sababisha either of the two.

yanapokuwa ya kweli mtu hataangalia alichonacho mtu hata siku moja tena ukisimuliwa na wengi waliopo kwenye ndoa za muda mrefu they can tell. imagine atu wanaoana na hata nyumba hawana wala chumba they start life maisha ya uswazi kuliko unayoyajua wewe dont dare say and they move on from there.

sasa wewe umetoa mfano wako mye nakupa ya kwangu tena ambayo mimi na wengine wengi tu ninaowajua tumepitia.
Nilianza life kuish nyumba ya udongo maeneo ya survey tena miaka ile ya 2000 hapakuwa vile zilikuwa niza udongo hazina bafu ndani sakafu hakuna dirisha ni dogo kama la choo. choo passpotsize. hapo mtu metoka kufunga ndoa mume ni mwanafunzi wa chuo na mke pia.hela hamna but love tu ndio iliyokuwa ina stand inbtn. maisha hayo unazaa mtoto house maid analala kwa jirani ili wewe na baba muweza kulala na asubui kwakua chumba ni kimoja anawagongea mnafungua anaendeela na kazi zake.Tena usiseme panapo upendo wa kweli hata mtu aseme nini you will not listen wanasema kaolewa na maskini wewe mnakula dagaa mnalala tena daga lenyewe walifwata buguruni manake ndio dagaa la 400 mnakula wk nzima. Acha eiyer lakn watu tulimudu. Fikiria katika hali ngumu kiasi hicho mtu unamtahiri mtoto kwenye kajumba kama hicho na bado Mungu anawalinda.

maisha haya kwangu sasa ni historia na nabaki kuwapa wengine ushuhuda manake hata close friends nilikuwa sitaki waje kwangu it was shameful life but Mungu aliona uaminifu na upendo wetu akatubariki sasa namtukuza sijisifu but naish mazuri sana. wengi huwa wanafkiri nilianzia hapa but ukweli siyo hivyo nilianzia chini kuliko mtu mwingine yyte.Panapo mapenzi ya kweli huwez kuona kama pesa ama elim ni factor but to you life is all what God has gave you.

hao wenye fake love wapo tena wengi tu kwako wanaangalia pesa kiasi ganai mwenzi anazo, ama elimu. nawajua wanaume ambao wameoa wanawake kwasababu mke anakzi nzuri na kipato but yeye hamfeel kivile matokeo mwanamke anahisi anapendwa kumbe jamaa hana mpango zaid ya pesa yake tu . na pia kuna wanawake wa dizain hizo so inategemea umekutana na wa aina gani.
Mdau inaonekana wewe unamjua Mungu aliye kulinda kipindi hicho akakuvusha hali hiyo hadi akakufikisha hapa ulipo sasa, swala hapa ni kumjua Mungu muweza wa yote!!!!Huyo ndugu yetu anahitajika kupata mpenzi yaani mke mzuri toka kwa Bwana Mungu, na mwali vile vile apate mme toka kwa Mungu bila hivyo kudanganyana ni kwingi!!!! Mume mwema na mke mwema utoka kwa Mungu Baba, jamani mbarikiwe wote!!!!
 
Mdau inaonekana wewe unamjua Mungu aliye kulinda kipindi hicho akakuvusha hali hiyo hadi akakufikisha hapa ulipo sasa, swala hapa ni kumjua Mungu muweza wa yote!!!!Huyo ndugu yetu anahitajika kupata mpenzi yaani mke mzuri toka kwa Bwana Mungu, na mwali vile vile apate mme toka kwa Mungu bila hivyo kudanganyana ni kwingi!!!! Mume mwema na mke mwema utoka kwa Mungu Baba, jamani mbarikiwe wote!!!!

to me life is what God has gave. So huku kuhangaika ni kusumbuka tu ila kama kakukusudia utapata tu. Thanks sana mkuu na lihimidiwe jina Mungu aliyejuu asiyeuacha unyayo wetu kusogezwa wala asiyesinzia asitulinde. Barikiwa sana
 
hii story imenikumbusha stori moja nilisimuliwa na baba yangu mkubwa, alipokuwa kijana kuna binti walipendana sana, ikafika kwenda kujitambulisha kwa wazazi ili taratibu za mahari zifanyike, yule bint alikuwa anasomea ualimu enzi hizo, dingi yeye alikuwa anapiga degree yake pale Uclas. Basi kufika pale wazee wa binti faster wakataka kujua kazi ya dingi, dingi aliwapa jibu la kuwakatisha tamaa kwamba yeye ni mtapisha vyoo, aminni usiamini shughuli iliishia hapohapo, hii issue si kwa wanawake tu, hata familia zetu nazo ziko hivyo hivyo, wachungulia mpaka upande wa pili wa shilingi
 
Back
Top Bottom