Wanawake wanataka wenye...

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Najua mtanibishia sana,lakini ukweli wa kile ninachokishuhudia na kinachotokea kinawatia hatiani. . . . .

Niliwahi kuwa na uhusiano wakati fulani na Luteni wa JW,lakini kabla uhusiano wangu ule na yule dada haujashika kasi niliamua kumwambia ukweli yule dada kunihusu,bahati nzuri sikua na elimu aliyokua akihitaji yule dada,na pia kingine ambacho sikua nacho ambacho alihitaji niwe nacho ni pesa,uhusiano wetu ulikufa siku ileile,usishangae nilivyosema bahati nzuri,we hujui kujua mtu ni wa hovyo mapema ni bahati,alinieleza wazi hawezi kuwa na mtu mwenye elimu kama yangu halafu asiekua na hela,nilicheka sana,wadada wa aina hii nimekutana nao wengi,wengine hawasemi lakini unajua tu . . . . . . Tangu mwaka uanze mpaka leo nimeshuhudia mahusiano kumi tofauti yakifa yangali machanga,na yamekufa baada ya wadada kugundua wanaume walionao,hawana hela wala elimu kubwa.

Lakini pia najua mahusiano zaidi ya matano ambayo yanaendelea lakini wanaume wale wamewadanganya wanawake kuhusu kipato na elimu.Je wanawake mnapenda uongo? . . . . . Ukweli ulio wazi ni kuwa,wanawake hawawataki wanaume kama mimi wasio na elimu wala pesa.Najua mtakuja na ubishi wenu hapa na maisha yenu ya mdomoni msiyoyaishi ya kudai eti mnataka mwanaume mwenye upendo wa dhati wakati mnajua ni uongo.

Mwanamke anataka mwanaume mwenye hela, elimu kubwa na sura kama ya mdoli.

Hayo ya upendo na kumjua Mungu ni uongo. Hebu nenda Love Connect (hua naiona kama chit-chat) uone kama sisi wa darasa la saba na tunaishi kwa vibarua kama tuna nafasi. Tukiacha mizaha ya love connect, Ukweli ndo huo, hayo ndo yanayotokea mitaani, ukija huku wanajidai nataka mwanaume mwenye upendo mengine mungu atatupa,ukikutana nae mtaani anakuangalia juu chini kisha anakuhoji elimu na kazi unayofanya,mkiachana unaona simu hapigi tena wakati kabla hajajua kuhusu hayo ya kazi na elimu,sms na simu mpaka zilikua kero(nina watu wa3 yamewatokea).

Mimi kwa mfano,sijazoea kudanganya,waliopata kukutana nami wanajua,ninakuambia ukweli,mimi ni darasa la saba,kama unasepa usepe,sina sababu ya kudanganya,mara niazime gari sijui nguo!

Nakuambia wazi nakaa uswazi,nyumba haina bafu,ukitaka kuoga unasubiri usiku,choo pasport size,huwezi tembea,niache atakaeona upendo ndo mpango mzima atakua nami.

Kama hujiamini utaishi maisha fake sana. . . . . . . . All an all wanawake 98% wanataka wanaume wenye hela na elimu kubwa,ila watu hawa wamegeuka kilio kwa akina dada baada ya hao jamaa kutokua waaminifu.

Huo ndio UKWELI hata mkibisha!Action speaks than words!!!!
 
Gazeti lote hilo(Hoja yako) kumbe ungeweza kuiandika ndani ya sentensi moja tu. jifunze kufupisha habari.
 
Eiyer mdogo wangu wa moyoni pole sana kwa yaliyokukuta.Nianze kwa kucomment kwenye uandishi ungeiwekea paragraph ingekaa vizuri kweli na kusoeka kwa raha zaid.

back to the point duniani kotwe miye huwaga naasema kuna mapenzi ya aina 2 tu katka mahusiano ama yawe mapenzi ya kweli ama yawe mapenzi feki. matamanioa siyaguzi kabisa wala siyapi nafasi amanke yaweza sababisha either of the two.

yanapokuwa ya kweli mtu hataangalia alichonacho mtu hata siku moja tena ukisimuliwa na wengi waliopo kwenye ndoa za muda mrefu they can tell. imagine atu wanaoana na hata nyumba hawana wala chumba they start life maisha ya uswazi kuliko unayoyajua wewe dont dare say and they move on from there.

sasa wewe umetoa mfano wako mye nakupa ya kwangu tena ambayo mimi na wengine wengi tu ninaowajua tumepitia.
Nilianza life kuish nyumba ya udongo maeneo ya survey tena miaka ile ya 2000 hapakuwa vile zilikuwa niza udongo hazina bafu ndani sakafu hakuna dirisha ni dogo kama la choo. choo passpotsize. hapo mtu metoka kufunga ndoa mume ni mwanafunzi wa chuo na mke pia.hela hamna but love tu ndio iliyokuwa ina stand inbtn. maisha hayo unazaa mtoto house maid analala kwa jirani ili wewe na baba muweza kulala na asubui kwakua chumba ni kimoja anawagongea mnafungua anaendeela na kazi zake.Tena usiseme panapo upendo wa kweli hata mtu aseme nini you will not listen wanasema kaolewa na maskini wewe mnakula dagaa mnalala tena daga lenyewe walifwata buguruni manake ndio dagaa la 400 mnakula wk nzima. Acha eiyer lakn watu tulimudu. Fikiria katika hali ngumu kiasi hicho mtu unamtahiri mtoto kwenye kajumba kama hicho na bado Mungu anawalinda.

maisha haya kwangu sasa ni historia na nabaki kuwapa wengine ushuhuda manake hata close friends nilikuwa sitaki waje kwangu it was shameful life but Mungu aliona uaminifu na upendo wetu akatubariki sasa namtukuza sijisifu but naish mazuri sana. wengi huwa wanafkiri nilianzia hapa but ukweli siyo hivyo nilianzia chini kuliko mtu mwingine yyte.Panapo mapenzi ya kweli huwez kuona kama pesa ama elim ni factor but to you life is all what God has gave you.

hao wenye fake love wapo tena wengi tu kwako wanaangalia pesa kiasi ganai mwenzi anazo, ama elimu. nawajua wanaume ambao wameoa wanawake kwasababu mke anakzi nzuri na kipato but yeye hamfeel kivile matokeo mwanamke anahisi anapendwa kumbe jamaa hana mpango zaid ya pesa yake tu . na pia kuna wanawake wa dizain hizo so inategemea umekutana na wa aina gani.
 
Last edited by a moderator:
Ukweli ni kwamba, wanawake wengi mimi included tunataka mwanaume ambaye anakupenda na he can take care of you, financially na kimawazo na kimtazamo; hivyo basi tungeprefer au tunadream kuwa awe na uwezo kukuzidi (kama wewe unao any), elimu/uelewa wa mambo kukuzidi n preferable hata akuzidi walau miaka 2.

Ukipata unaye mzidi hivyo vyote juu, hata kama unanpenda kiasi gani, kama uelewa wake mdogo ndoa huwa na shida sana. Nami nimeshashuhudia my friends ambao ndoa zimevunjika coz mwanaume hajiamini na kuamua kuwa physical just to prove yeye ndie man of the house.

I was in a sort of the same relationship, sikumzidi pesa, but elimu na mafanikio; siwezi rudia bora niwe peke yangu aisee!

Sikatai, kuna baadhi yetu tunakuwa na nyodo lkn ni wachache sana kuliko wanaume mnavyopenda kujiaminisha ktk story zenu kiasi kwamba mnaanza kujihami kwa ubabe usio na kichwa wala miguu.

Kuhitimisha nasema, wanawake hatupendi kudanganywa but tunahitaji mwanaume tunayeweza mtegemea!
 
gfsonwin mkianzia wote chini, hiyo ni tofauti; tena mara nyingi mkija kufanikiwa wengi wa wanaume husahau mlipotoka na kutafuta vimodel kwamba ndio hadhi yao at that moment.

Lkn mwanamke akiwa juu, chances kubwa sana ya ndoa kuwa na matatizo. Too bad kila mtu anahitaji mapenzi lkn isingekuwa hivyo, kuliko kugamble looking for 1 understanding man among 10, bora kuwa mwenyewe!
 
Eiyer mdogo wangu, wakati ule maisha hayajani-infletikia nilikubembeleza uende shule ukagoma.

Kiukweli mie siwezi kutoka na mtu wa std 7, hata kama ana hela kama kichaa kwa sababu najua atajisikia inferior kila wakati. Na siwezi kutoka na mtu mwenye hela nyingi sana kwa sababu nitakuwa sensitive akichelewa miadi tu nitaona ananidharau. Staki kusikia 'baby, naomba tusitoke/nisije kukuona, kuna business deal imejitokeza....', nita-fume japo ingekuwa ni dili la mzigo wa vitunguu ningekuwa fresh.

Ila kaka, kwani hata wewe si una vigezo vyako kabla ya kumtokea binti? Waache na wao waweke vigezo. Mi naulizaga cv na bank statement za miezi 3 upfront kabla hata ya utani wa kimapenzi,lol
 
gfsonwin, nakubaliana na Kaunga. Walioanzia chini pia wakipata hawakawii kuanza dharau! Niliwahi kumkumbusha ndugu yangu mmoja, mkeo akianza kukupenda ulikuwa unavaa shati unafua usiku na kulianika kwenye feni. hizi bmw na v8 ni majaaliwa tu, na zinapitaga!

Japokuwa kwa mwanamke na hata mwanaume ukishakuwa na mahela mengi, upendo wa kweli ni adimu haswaa
 
Last edited by a moderator:
@gfsowin mkianzia wote chini, hiyo ni tofauti; tena mara nyingi mkija kufanikiwa wengi wa wanaume husahau mlipotoka na kutafuta vimodel kwamba ndio hadhi yao at that moment.

Lkn mwanamke akiwa juu, chances kubwa sana ya ndoa kuwa na matatizo. Too bad kila mtu anahitaji mapenzi lkn isingekuwa hivyo, kuliko kugamble looking for an 1 understanding man among 10, bora kuwa mwenyewe!
Kaunga umesema kweli kabisa to me huwa nasemaga hivi maisha ni vile yanavyokujia na pia ni bahati tu. nimeona baadhi ya wtu they start from ground pamoja but wakishaanza kupata vijisent na maisha yakawanyookea mume huwa anasahau kila kitu.

utakuta mwanaume anaanza kutafuta kimodo ambaye sasa ngozi ni soft hajachoka kwa kutafuta kama wee basi tabu tupu. Mimi kitu ambacho nasimamia kama msimamo wangu ndani ya ndoa ni let him do wereva he thinks its good for him i will stand firm in ma house. and i dont want to be bothered ana tambea na mwanamke gani na wa sura gani neva. sihitaji kujua na nashukuru hanionyesh so wedha he does or not sijui.

mimi humu ndani nyumba safi, menu fresh, najiweka usipime, saloon everyweek, job naenda navaa napendeza pia salam za kuomba hela kila saa hizo sina i look for my own money to make me good.

Nina msemo huwaga nautumia sana pesa yako ukinipa nitapokea but sikuombi hata siku moja unipe. sasa ndio ajiulize huyu huwa anapata wapi hela kila siku? akiwaza napewa sawatu. na siku nikichungulia wallet hana kitu kumdondoshea kilo moja ama mbili siyo tabu.

hawa wanaume ukijifanya uko inferior wanakutesa sana na ndio maana wanawake wengi wenye elim hawapend mtu asiyekuwa na elimu manake atamtesa tu kila saa jitu litahsi kunyanyasika as a defence unalijali unakuta llinalala baa na makahaba. Pumbaf kabisa tena huwa ni mtu wa kujipa raha sana outing kama akitaka twende akiona vipi abaki mm naenda na nilaazima every weekend nitoke na kids na sik moja moja nimpigie tukae japo one for the road.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin, nakubaliana na Kaunga. Walioanzia chini pia wakipata hawakawii kuanza dharau! Niliwahi kumkumbusha ndugu yangu mmoja, mkeo akianza kukupenda ulikuwa unavaa shati unafua usiku na kulianika kwenye feni. hizi bmw na v8 ni majaaliwa tu, na zinapitaga!

Japokuwa kwa mwanamke na hata mwanaume ukishakuwa na mahela mengi, upendo wa kweli ni adimu haswaa


shositito King'asti pana kitu kimoja ambacho huwa tunakisahau. achilia mbali mlitoka wapi na mko wapi sasa, la msingi ni tutaendeleza upendo na mapenzi yetu vipi? hilo ndo la msingi. na hapo ndipo penye mtihani haswa

mimi principle yangu nampa uhuru atakavyo na mimi nipewe uhuru nitakavyo let my conscious choose for me what to o and what not to do. ukianza kumchunga sana mwanaume hasa wakati mnapokuwa na neema ya maisha jua sasa ndio unampoteza.

wanaume walio wengi wanapenda wadharauliwe in terms of yaani wereva they do do not draw your attention to it. Dharau kisha ishi maisha yako safi, pendeza sana mno yaani hapa uwe nyoko kweli kweli. halafu timiza wajbu wako ndani nakwambia atachachawa lkn atarudi tu tena na mapenzi motomoto but ukiwa ni mtu wa kulia from morning to evening uso unanyorodoka hakika maisha ya ndoa yatakuwa msalaba ma dia. ngoja nikuandikie pm just a story of ma life you will understand what i mean
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin,kuhus paragraph haka ka kompyuta nilikokua nakatumia tabu tupu nikaamua niiweke kwa mtindo huo hivyohivyo.Uliyosema ni kweli kwa mlioanzia chini pamoja,halafu ni afadhali mliokuwa mnaolewa/oa miaka ya nyuma,ila kwa sasa ni matatibwa sana.Wanawake wanaojali upendo there not exist now days,trust me!
 
Mkuu Ukitaka kuelewa haya maswala inabidi urudi sana nyuma kihistoria kaka mkubwa!
Kwa sababu hii ni side effect ya ule mfumo wetu asisi (Its 'mfumo dume on backfire').
Mfumo Dume kama unavyoujua unahitaji wanawake wawe ma majukumu fulani ambayo unayajua...sasa Kuwa na uwezo kifedha, kiupeo, kiuongozi na kijamii kumzidi mwanamke ni sifa ya mume. Kwenye hii system lazima mwanamke ataridhia maombi ya aliyemzidi vitu vyote hivyo! Ndo maana haikushangazi ndoa nyingi wanawake ni wadogo kiumri kwa ulinganisho na waume zao (Hii ni kuwapa muda wanaume waweze kutangulia)...
Halafu mkuu kwani unashindwa kujiendeleza kielimu...Trust me ukiangalia vizuri walioishia darasa la saba wamependa
(Utasema wazazi hawakuwa na uwezo, kwani si umekua na kufanya kibarua? mitihani ya qt bei rahisi sana tu).
Now, kama umependa kuishia darasa la saba, kuna dhambi gani mwanamke akataka aliyeishia sekondari?
 
gfsonwin,kuhus paragraph haka ka kompyuta nilikokua nakatumia tabu tupu nikaamua niiweke kwa mtindo huo hivyohivyo.Uliyosema ni kweli kwa mlioanzia chini pamoja,halafu ni afadhali mliokuwa mnaolewa/oa miaka ya nyuma,ila kwa sasa ni matatibwa sana.Wanawake wanaojali upendo there not exist now days,trust me!
 
gfsonwin,kuhus paragraph haka ka kompyuta nilikokua nakatumia tabu tupu nikaamua niiweke kwa mtindo huo hivyohivyo.Uliyosema ni kweli kwa mlioanzia chini pamoja,halafu ni afadhali mliokuwa mnaolewa/oa miaka ya nyuma,ila kwa sasa ni matatibwa sana.Wanawake wanaojali upendo there not exist now days,trust me!

nimekupa like si kwamba umepatia bali kwa kunikosha roho tu. Eiyer piga ua siyo wanawake wote siku hizi ni wabaya interms of hawapend kwa dhati. Wapo ila yakupasa umchague kwa makini na kwaku maanisha. tatizo lenu vijana wa leo mnabweteshwa na nani anajua kufanya matusi vizuri na huyu mkimpata mnaona mengine yatajisolve kumbe ni bora asiyejua utamfunza lakin awe na nidham nzuri na ueleewa wa maisha na hili limekuwa ni tatizo kwa vijana wote wa kike na wa kiume.

labda nikuulize Eiyer kuna umuhimu gani kuoa mtu anayejua kufanya matusi halafu hana nidhamu wala upendo wa kweli? si kweli kwamba matus peke yake ndiyo yanayojenga nyumba ni zaid ya hapo n yote waweza yatengeneza bali tabia ya mtu ni ngumu sana.
 
Last edited by a moderator:
Kaunga my love,listen,during back days there was not such thing,taking care financially but taking care,full stop.Haya mambo mengine yanaletwa na usasa na hayana maana.Najua wapo wanaume wajinga wasiojiamini,pia inawezekana wapo wanawake waliokutana nao,sasa unamhukumuje mtu kwa kosa alilofanya mwingine? . . .Mfano mimi najua wapo wanawake ambao hawajali lolote isipokua upendo na mapenzi,siwezi kuhukumu wote japokua wengi sana.Kujiamini kwa mwanaume ni jambo la muhimu sana na mwanamke anaweza kuchangia jambo hilo kama ana akilg. . . . . . . . . . . Kwenye kudanganywa mwanamke mwenyewe ndo anatengeneza mazingira ya kudanganywa!
 
Dada yangu King'ast,sasa wewe baridi ya Makambako halafu unaambiwa uamke uende shule unadhani vizuri. . . . . . . . . . . . . . . . Hebu rudi hapa uniambie elimu inamfanyaje mtu ajitambue,aujue upendo,kujiamini,kujua majukumu yake n.k kabla hujajua kuwa elimu mtu anaweza kuiongeza wakati wowote ule!
 
Back
Top Bottom