Wanawake wachangamkie Ubunge mwaka huu-Mama Salma Kikwete

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
mama%20salma.jpg

Mama Salma Kikwete, akiwapungia mkono wanawake waliohudhuria sherehe za Uzinduzi wa Umoja wa Wanawake kutoka vyama vya siasa vyenye wabunge ujulikanao kama Ulingo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa umoja huo Anna Abdallah.(Picha na Selemani Mpochi)



[FONT=ArialMT, sans-serif]Wanawake nchini wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kugombea ubunge wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, ili kufikia lengo la asilimia 50 ya wabunge, badala ya kutegemea viti maalum.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Rai hiyo ilitolewa jana na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, wakati akizindua Umoja wa Jumuia za Wanawake wa Vyama vya Siasa nchin i(TWCP- ULINGO), jijini Dar es Salaam jana.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kwamba wanawake hawana budi kuungana na kupigania haki yao kwa kufuata sheria na katiba za umoja huo na kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, ili kuongeza idadi ya wabunge wanawake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Mimi naungana na ninyi, tushike uzi huo huo, tutasaidiana katika kufanikisha kauli mbiu yetu kwamba wanawake tunaweza, tujitokeze kwa wingi kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu" alisisitiza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alieleza kuwa lengo kubwa la umoja huo ni kuhakikisha kunakuwa na upendo na mshikamano bila kujali tofauti za kisiasa miongoni mwa wanawake wote nchini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Huu ni mwaka wa uchaguzi tukishirikiana hakuna anayeweza kutushinda, mshikamano na umoja wetu pamoja na uongozi thabiti katika jumuia hii ndiyo mafanikio yetu, naamini mshikamano wetu utatuwezesha kufikia asilimia 50 ya wabunge wa kuchaguliwa wanawake na sio kutegemea viti maalum" aliongeza kusema Mama Salma.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mke huyo wa Rais Jakaya Kikwete, alisema kuwa mafanikio makubwa katika jamii yanafanywa na wanawake, lakini akasikitika kuwa wapo baadhi yao wananyanyasika na kukosa haki zao za msingi, ikiwemo kunyimwa kurithi mali walizoachiwa na waume zao ambao wamefariki.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema ni jukumu la umoja huo, kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika masuala ya siasa na elimu ili kujikomboa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Naye Mwenyekiti wa TWCP, Anna Abdallah, alisema baada ya kutafakari kwa muda mrefu waliona kwa sasa kuna umuhimu wa kuanzisha jumuia hiyo kutokana na matatizo ya wanawake wa Tanzania yanafanana na hayabagui itikadi ya kisiasa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema umoja huo unahimiza ushiriki wa wanawake kwenye medani za siasa pamoja na kutokomeza mfumo dume unaoathiri wanawake wa hapa nchini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Umoja huu utasaidia kuongeza nafasi za wabunge wanawake na kutatua matatizo ya wanawake kisiasa, mwaka huu tunapigania kuongeza nafasi bungeni badala ya kutegemea viti maalum" alisema Abdallah.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwashukuru wafadhili mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa uzinduzi huo, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji, Ole Naiko na Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Shyrose Banji, kwa michango mbalimbali waliyotoa kwa jumuia hiyo.[/FONT]



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Nawatakia wanawake wote kila la heri,wafikie malengo yao ya kufikisha 50/50 representation
 
Back
Top Bottom