"Wanawake wa siku hizi wanadeka sana"

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Khabari ya Jumapili kwa mpigo,
Kuna gynecologist mmoja maarufu sana hapa nchini anasema kati ya wanawake 20 wenye umri kati ya miaka 16 – 35 wanaopelekwa kujifungua, 15 hujifungua kwa njia ya caesarean section.


Bingwa huyo amedai kuwa hiyo inatokana na wanawake wengi wa siku hizi kuwa "wanadeka sana" hasa wakiwa wajawazito.

Akiwafananisha na wale waliozalizaliwa hasa nyuma ya miaka ya 70, amesema hawa wa siku hizi ni "wavivu" wanapokuwa wajawazito, hawapendi kujishughulisha.

"Utamkuta mdada mjamzito eti kwa kuwa ana msaidizi/wasaidizi basi nyumbani hashiki kitu, yeye ni kulala tu….wenzao wa zamani walikuwa wanajishughulisha bwana, yaani huwezi kumjua kama mjamzito kwa kazi anazozifanya…mara ataenda shamba, atabeba kuni, akirudi atachota maji, atafua, atapika…ili mradi yupo bize….hata delivery kwao ilikuwa rahisi sana…tena wengi wao waliweza kujifungulia nyumbani, wengine bila hata msaidizi. Hawa wa sasa thubuuutu" alisema bingwa huyo.


Wadau hii ni kweli..?
 
Sasa mnataka watu wasideke kwanini?!Nwy hiyo iko mijini tu...vijijini mwendo bado ni ule ule!!
 
Kama zipi?!

Pia unajua effect zinazotokana na kufanya kazi ngumu wakati wa ujauzito?!

Nipe zote tulinganishe!!!

Si lazima kufanya kazi ngumu Lizzy,
Walau kujishughulisha shughulisha.
Yaani hata kuosha vyombo au kupika pia ufanyiwe...!!!!!? Hapana bwana!
 
Mkuu umeongea wadada wa sikuhizi wamekaa kimapicha zaidi
kwanza hata huyo anaye pata ujauzito ujue bahati mbaya
wako kistarehe mno
 
mbona mie najidekeza nikiwa mjamzito ila kujifungua napush? sema siku hizi matatizo ni mengi watu wanaona wasirisk
 
Si lazima kufanya kazi ngumu Lizzy,
Walau kujishughulisha shughulisha.
Yaani hata kuosha vyombo au kupika pia ufanyiwe...!!!!!? Hapana bwana!

Sasa huo ni uvivu wa asili hauna cha ujauzito wala mwepesi!!Inabidi na nyie muwe mnawasoma wenzi wenu vizuri kabla ya kuwaweka ndani na kuanza kuendesha wadada wa kazi!!!
 
mbona mie najidekeza nikiwa mjamzito ila kujifungua napush? sema siku hizi matatizo ni mengi watu wanaona wasirisk
<br />
<br /
Kujidekeza muhimu mwaya ukijifanya wewe ndio bingwa wa kufanya mikazi unaweza kupata miscarriage. Nimeumwa uchungu wa 1st born nikiwa jikoni napika chapati,2nd born nimeumwa nikiwa najiandaa kwenda kazini lakini bado kudeka kama kawa! Muhimu ni ku do the needful ukiingia leba(ku push).
 
kama unae wa kumdekea sio vibaya kudeka.madeko si ya muda tu,ukishajifungua deko halipo tena.na massage utanifanyia
 
wanadeka mno siku hizi....


kufua mashine
kuosha vyombo mashine
kupika majjiko ya umeme
ma house girl wawili still....
 
Khabari ya Jumapili kwa mpigo,
Kuna gynecologist mmoja maarufu sana hapa nchini anasema kati ya wanawake 20 wenye umri kati ya miaka 16 &#8211; 35 wanaopelekwa kujifungua, 15 hujifungua kwa njia ya caesarean section.


Bingwa huyo amedai kuwa hiyo inatokana na wanawake wengi wa siku hizi kuwa "wanadeka sana" hasa wakiwa wajawazito.

Akiwafananisha na wale waliozalizaliwa hasa nyuma ya miaka ya 70, amesema hawa wa siku hizi ni "wavivu" wanapokuwa wajawazito, hawapendi kujishughulisha.

"Utamkuta mdada mjamzito eti kwa kuwa ana msaidizi/wasaidizi basi nyumbani hashiki kitu, yeye ni kulala tu&#8230;.wenzao wa zamani walikuwa wanajishughulisha bwana, yaani huwezi kumjua kama mjamzito kwa kazi anazozifanya&#8230;mara ataenda shamba, atabeba kuni, akirudi atachota maji, atafua, atapika&#8230;ili mradi yupo bize&#8230;.hata delivery kwao ilikuwa rahisi sana&#8230;tena wengi wao waliweza kujifungulia nyumbani, wengine bila hata msaidizi. Hawa wa sasa thubuuutu" alisema bingwa huyo.


Wadau hii ni kweli..?

Kwanza oa..; mpe mimba mke wako halafu fanya hiyo experiment yako..hasa wakati anajifungua inabidi uwe hospital.uone wakati mkeo anapigana na maisha yake....JF bado ipo..baadaye lete majibu hapa....

Kumbuka maisha ya ndoa ..siyo "Big Brother reality show" na kumbuka kuzaa sio filamu ya kanumba.. ni Real life.. ni kitu cha kufa na kupona..

Jiulize swali hili.. utapenda mke wako ajifungue kwa kawaida?.kama hapana.. utapenda mke wako apate operation? na kama ni Yes...utapenda operation unajua wakati anafanyiwa hiyo operation kuna uwezekano anaweza kuongezwa damu?.. na kutokana na magonjwa ya sasa damu hiyo inaweza kuwa sio salama? Uko tayali kuchukua risk hiyo? au utakubali operation kama tu imeshindikana kawaida na kuokoa maisha ya mama?

Kaa chini na jibu hayo maswali..hapo juu .. basi utapata jibu la swali lako..
 
Back
Top Bottom