Wanawake Togo wasusia ngono kudai Mageuzi

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280

Wanawake nchini Togo, wametakiwa kususia kitendo cha ndoa kuanzia Jumatatu wiki hii kama njia ya kushinikiza serikali kuleta mageuzi.
Kampeini hiyo yenye kauli mbiu ''Juhudi za kuokoa Togo'' imeanzishwa kwa ushirikiano na mashirika tisa ya kijamii pamoja na vyama saba vya upinzani pamoja na vyama vingine vya kijamii.
Kiongozi wa upinzani, Isabelle Ameganvi alisema kuwa kususia ngono huenda ndio itakuwa silaha inayofaa kuweza kuleta mageuzi ya kisiasa.
Muungano wa vyama hivyo pamoja na mashirika yasiyo ya kijamii unataka rais Faure Gnassingbe, ambaye familia yake imeshikilia madaraka kwa miaka mingi waweze kuondoka mamlakani.
"tuna njia nyingi za kuwashinikiza wanaume kuelewa tunachotaka sisi wanawake'' alisema bi Ameganvi, kiongozi wa tawi la wanawake la muungano huo.
Alisema kuwa yeye ameweza kushawishiwa na mgomo sawa na huo nchini Liberia mwaka 2003,ambao walitumia njia ya kususia ngono kushinikiza amani.
"ikiwa wanaume watakataa kusikia kilio chetu, tutalazimika kufanya maandamano ambayo yatakuwa makali zaidi kuliko mbinu hii ya kususia ngono.'' aliongeza bi Ameganvi
Togo imekuwa ikiongozwa na familia moja kwa zaidi ya miaka arobaini.




Je, njia hii huenda ikawa silaha madhubuti kwa hali ya kusuasua kwa utawala hapa Tz? Tafakari....
 
wakisusia kwa hapa TZ zitakuwa habari njema sana kwa machangu na nyumba ndogo!!
 
ingependeza kama ungetoa preamble kidogo! Imekuwakuwaje mpaka wakasusia
 
cropped520_femmeNUE480083_464829743551289_107273574_n.jpg


Togolese women turn their back (sides) on police | The Observers
 
Back
Top Bottom