WANAWAKE roho mbaya namna hii mnaitoa wapi mnapokua MAMA WA KAMBO?

Ni kweli NN, ukaribu wa baba kwa mtoto ndio kinga pekee inayoweza kumwepusha mtoto na manyanyaso/vipigo kutoka kwa mama wa kambo...

Taire! Taire!

Ila cha kushangaza kuna wanaume wajinga sana, eti libaba linahama upande wa mwanae na kuwa upande wa mkewe, kila anachoambiwa na mtoto ni uongo na kila anachoambiwa na mkewe ni ukweli, mtoto anabaki peke yake, hana wa kumsapoti wala kumweleza shida zake...hapa atanyanyasika mpaka apate akili ya kiutu uzima aweze kujiokoa peke yake.

Mijanaume kama hiyo inahitaji kwenda kusafishwa nyota.

Mama wa kambo huwa wanapima upepo wa baba akikuta libaba lege lege basi huyo mtoto cha moto atakiona, ila kama baba anamsimamo na yuko upande wa mtoto kamwe hatathubutu kumnyanyasa... Mtoto anajenga kujiamini na ataishi kwa amani...

Ni kweli kabisa. Wakishakusoma tu na kuona huna msimamo wala kanuni mtoto anaweza kupata shida sana. Ila wakijua kuwa una msimamo thabiti watajiuliza mara mbilimbili kuleta sokomoko kwa sababu wanajua lazima patachimbika bila jembe wala shoka.
 
inasikikitisha kuwa ulichokisema ni kweli kwa asilimia nyingi..........................!
ila wapo mama wa kambo wazuri sana tu...................hata hivyo huwa najiuliza.............mtoto ni mtoto lakini kinachomshinda mama kumpenda mtoto ambaye hajamzaa ni kitu gani.............!......ingekua vizuri kama tungepata wamama wakambo tukawasikia maelezo yao...................labda tungeelewa kiini cha roho zao mbaya...................!
Ni kweli father wapo wamama wazuri sana kiasi ambacho usiyemjua huezi kugundua kama sio mama mzazi wa mtoto...

Afu hakuna kitu kinaniuma kama mmama kumnyanyasa mtoto ambae mamake ametangulia mbele ya haki, huwa naumia sana, daah sijui bana hizo roho mbaya zao huwa zinaletwa na kitu gani. Labda kweli waje hapa waseme chanzo ni nini haswa!
 
@ NN siku zote nikiona/ kusikia mtoto ananyanyaswa na mama wa kambo huwa napeleka lawama zangu moja kwa moja kwa baba manake ameachaje mama akapata hiyo nafasi?..

Ni kupagawa na mapenzi mpaka anaacha kumthamini mwanae au?

nimecheka sana hapo pa kwenda kusafisha nyota lol... Ni kweli manake wanakuwaga na akili sio za kawaida...
 
Baba wa mtoto akiwa karibu na mtoto wake na kumpenda kwa dhati atahakikisha huyo mama wa kambo hamnyanyasi mwanae.

Kwangu mtoto anatangulia kabla hata ya maslahi yangu. Asilani siwezi kuruhusu mtoto wangu kukosa furaha na amani kisa mama yake wa kambo.

Ndiyo maana ni vyema wazazi wakawafundisha watoto wao kutokukubali kunyanyaswa na yeyote yule. Mimi sioni ubaya wowote ule kumfundisha mtoto wako kuwa hakuna mwenye haki ya kumpiga, kwa mfano.

Na ikitokea kapigwa basi naye apigane. Heshima wakati mwingine ni lazima mtu uitafute la sivyo utafanywa mkeka.

Nimekupata vizuri sana,hii itasaidia kwa watoto wakubwa. Mm naomba msaada wakujua mtoto wa miaka 4 atajisadiaje kwenye hili tatizo na kama baba mtu akirudi anaanza kuelezewa na hawara yake kuwa mtoto hasikii maneno kibao! Halafu baba huyo bila haya anaanza kumpiga huyo malaika. Unaweza kuielewa kweli hii NN?
 
Ni kweli kabisa. Wakishakusoma tu na kuona huna msimamo wala kanuni mtoto anaweza kupata shida sana. Ila wakijua kuwa una msimamo thabiti watajiuliza mara mbilimbili kuleta sokomoko kwa sababu wanajua lazima patachimbika bila jembe wala shoka.

Hahahahaaaa walau nimecheka daaah,asante.
 
Nimekupata vizuri sana,hii itasaidia kwa watoto wakubwa.

Kwanza kabisa akina Tuli hawajambo? Waambie anko kawamiss mbaya.

Ni kweli kabisa, hiyo iko applicable zaidi kwa watoto wakubwa lakini misingi yake ni vyema ikawekwa wangali wadogo.

Mm naomba msaada wakujua mtoto wa miaka 4 atajisadiaje kwenye hili tatizo na kama baba mtu akirudi anaanza kuelezewa na hawara yake kuwa mtoto hasikii maneno kibao!

Kwa kweli mtoto wa miaka 4 hawezi kujisaidia mwenyewe. Ila kama mama yake mzazi yupo (assuming mama mzazi na baba hawaishi pamoja), basi huyo mama mzazi anapaswa kuhakikisha kuwa mwanae yuko kwenye mazingira mazuri awapo huko kwa baba yake.

Ni vyema kumkagua mwanao, kumuangalia kama ana vi alama vyovyote mwili na kama anavyo unamdadisi kulikoni. Watoto ukiwa nao karibu watakuambia tu ukweli. Pia ni muhimu kuangalia tabia yake kwa ujumla - je ni mwenye furaha? ni muoga? anaogopa kuongea? Na mengine kama hayo.

Ukigundua yote hayo na ugundue kuwa yanaletwa na mama wa kambo, usipoanzisha timbwili nitakuona hufai kuwa mzazi. Mimi lazima ngumi zitalika tu. Mtoto wangu hawezi kunyanyaswa na baba wa kambo halafu nikae kimya.

Halafu baba huyo bila haya anaanza kumpiga huyo malaika. Unaweza kuielewa kweli hii NN?

Hili siwezi kabisa kulielewa. Hakuna kitakachohalalisha kumpiga mtoto mdogo. Hakuna. Mtoto wa miaka 2 au 4 kumpiga kama mtu mzima ni ukatili dhidi ya watoto na unapaswa kukemewa na kulaaniwa kwa nguvu zote.
 
kwakweli msitukumbushe sie tulioteseka jamani,huwa sielewi ni nn hasa inakua ivo mana hatukuwa wakorofi wala nini
ila Mungu hulipa hapahapa duniani,now tuko ngangari kama "skype avosema"

Poleni sanaaa Aza na Skype,Mungu wetu ni mwema sana na huwa hamtupi mja wake ndio maana mmefika hapo mlipo. Kuna post moja nilicomment nikasema naomba kama kuna mama wa kambo wanasoma humu jamaniiiii wabadilikee,sio vizuri kuwanyanyasa hao watoto hawana makosa. Kama vipi ni bora mkatae kuishi nao kabisa tena umjie juu huyo mumeo kuwa toto lako lina tabia mbaya mm siwezi kulilea nimejitahidi nimeshindwa tafadhali lirudishe kwa mama yake yani mtukane matusi yooote ila mwisho wa siku mtoto arudishe kwenye mikono inayostahili kumlea kuliko kuwatesa watoto wa wenzenu. Yaani inaniuma mnooo kusikia hizi habari za hawa watoto wa kambo.
 
Kwanza kabisa akina Tuli hawajambo? Waambie anko kawamiss mbaya.
Hawajambo,wanakutaja kila saa

Ni kweli kabisa, hiyo iko applicable zaidi kwa watoto wakubwa lakini misingi yake ni vyema ikawekwa wangali wadogo.
Mmhh MY SON ALINIAMBIA MAMI HIVI KWNN TUSICHUKUE GUN TUKAMPIGA DADI,NILISHTUKA SANA!Namshukuru Mungu tulikua wenyewe maana duuh balaa! Sasa wakiwa na anko km wewe si ndio watafanya kweli...lol

Kwa kweli mtoto wa miaka 4 hawezi kujisaidia mwenyewe. Ila kama mama yake mzazi yupo (assuming mama mzazi na baba hawaishi pamoja), basi huyo mama mzazi anapaswa kuhakikisha kuwa mwanae yuko kwenye mazingira mazuri awapo huko kwa baba yake.
Ni vyema kumkagua mwanao, kumuangalia kama ana vi alama vyovyote mwili na kama anavyo unamdadisi kulikoni. Watoto ukiwa nao karibu watakuambia tu ukweli. Pia ni muhimu kuangalia tabia yake kwa ujumla - je ni mwenye furaha? ni muoga? anaogopa kuongea? Na mengine kama hayo.
Ukigundua yote hayo na ugundue kuwa yanaletwa na mama wa kambo, usipoanzisha timbwili nitakuona hufai kuwa mzazi. Mimi lazima ngumi zitalika tu. Mtoto wangu hawezi kunyanyaswa na baba wa kambo halafu nikae kimya.
Hili siwezi kabisa kulielewa. Hakuna kitakachohalalisha kumpiga mtoto mdogo. Hakuna. Mtoto wa miaka 2 au 4 kumpiga kama mtu ni ukatili dhidi ya watoto na unapaswa kukemewa na kulaaniwa kwa nguvu zote.

Umenitoa machozi tuuuu.....siwezi hata kuendelea kuandika kitu cha maana hapa. Inshort hayo yote uliyoandika yametokea na kwa mtoto wa umri huo wa miaka 4 na matokeo yake mama alipokuja juu nusu afe kwa kipigo cha ex-husband madai kuwa anaingilia mahusiano yake kwa kisingizio kuwa mtoto ananyanyswa. NN tuyaache tu haya mambo. Ila Tz yetu hiiii sijui kama inaelewa maana ya haki.
Sheria zipo lakini hazifatwiiii.....in the first place 4yrs child hatakiwi kukakaa na baba labda huyo mama yake awe na utindio wa ubongo.
 
@ NN siku zote nikiona/ kusikia mtoto ananyanyaswa na mama wa kambo huwa napeleka lawama zangu moja kwa moja kwa baba manake ameachaje mama akapata hiyo nafasi?..

Ni kupagawa na mapenzi mpaka anaacha kumthamini mwanae au?

nimecheka sana hapo pa kwenda kusafisha nyota lol... Ni kweli manake wanakuwaga na akili sio za kawaida...

SL mpenzi wala sidhani kama ni swala la kupagawa na mapenzi....mm naona ni kutokua na mapenzi na mtoto,ila machoni mwa wetu anataka kujifanya yeye ndio baba tena boraaa na misifa kibao!nyama kabisa.
Mm niliona rafiki zangu walivyokua wakinyanyasika na mama wa kambo jamani mtu unaliaaaa,tena wao angalau walikua wakubwa kidogo. Nisipoangalia nitaandika kitabu bure. Ngoja nihame huu uzi kabla sijafa na pressure.
 
mimi nimelelewa na mama wa kambo karibia maisha yangu yote maana mama yangu alifariki tangu nikiwa darasa la kwanza lakini sijawahi kunyayasika kwa njia yoyote ile huyu mama amekuwa mtu mwenye upendo sana na nimejifunza mengi kutoka kwake na nitaendelea kumshukuru sana maisha yangu yote.

SIO MAMA WA KAMBO WOTE WANA ROHO MBAYA .

Isije ikawa ni mama yako mkubwa au mdogo...

Anamaanisha MKE MPYA wa baba yako baada ya kuachwa,au kufariki mama yako mzazi!
 
Ndio maana mpaka leo Mtoto wangu namlea mwenyewe bila Mama,
Wanawake wengi siwaamini kabisa!!!!
 
@ NN siku zote nikiona/ kusikia mtoto ananyanyaswa na mama wa kambo huwa napeleka lawama zangu moja kwa moja kwa baba manake ameachaje mama akapata hiyo nafasi?..

Ni kupagawa na mapenzi mpaka anaacha kumthamini mwanae au?

nimecheka sana hapo pa kwenda kusafisha nyota lol... Ni kweli manake wanakuwaga na akili sio za kawaida...

shem umetema madini leo...ni nomaa!..asante leo tangu nimeondoka umenilindia uzi wangu dhidi ya wale wachakachuzi....

hapo pakusafishwa nyota mm sijaelewa...so sijacheka bado!
 
Kina baba wana mchango mkubwa katika hili! Mara nyingi kama mama anaumizwa sana na baba (bothy emotionaly na phisically) mara nyingi na mama naye hutafuta mnyonge wake (ambaye hawezi kuwa mtoto wa kumzaa mwenyewe). Sasa ongeza na baba kutokuwa karibu na mtoto, yeye ni kirauli na yeye na small house kwa sana; yaani ni shida tupu!

Of course ni pamoja na sababu zilizotajwa hapo juu (utovu wa nidhamu wa baadhi ya watoto na roho mbaya ya baadhi ya kina mama); lakini pia mashangazi kwa maana ya mawifi wa Mke wanaweza changia au mfanya mtoto asimuheshimu mama yake wa kufikia!
 
Mmh! Sio wote bana, mbona mi nalea watoto wa kaka yako vizuri na tunapendana sana.
 
SL mpenzi wala sidhani kama ni swala la kupagawa na mapenzi....mm naona ni kutokua na mapenzi na mtoto,ila machoni mwa wetu anataka kujifanya yeye ndio baba tena boraaa na misifa kibao!nyama kabisa.
Mm niliona rafiki zangu walivyokua wakinyanyasika na mama wa kambo jamani mtu unaliaaaa,tena wao angalau walikua wakubwa kidogo. Nisipoangalia nitaandika kitabu bure. Ngoja nihame huu uzi kabla sijafa na pressure.
Asante Mama Tuli kwa ufafanuzi!... Cha kushangaza ni kwamba baba huyo huyo alikuwa anampenda mwanae kabla ya kuoa huyo mama mwingine, chukulia mf.. mtoto kafiwa na mamake akiwa bado mdogo, baba kaamua kuoa mwanamke mwingine, eti ghafla mapenzi kwa mtoto yanahama, chochote atakachosema mama anasikilizwa, baba hana tena muda na mwanae sio kupagawa huko ni nini mama tuli?... Jiulize mapenzi kwa mtoto yanaenda wapi?...
 
shem umetema madini leo...ni nomaa!..asante leo tangu nimeondoka umenilindia uzi wangu dhidi ya wale wachakachuzi....

hapo pakusafishwa nyota mm sijaelewa...so sijacheka bado!
Shemu wacha niteme manake ni vitu vya kweli bana, vipo kwenye jamii tunayoishi, tunashuhudia watoto wakiteswa na kunyanyaswa na mama zao wa kambo... Mie huwa nashangaa mama yupo hai afu anakubali mwanae alelewe na mwanamke mwenzie,.. Shemu kuna wanawake wana roho mbaya kuliko maelezo!...

Yaani mie hata ikitokea nakorofishana na kakako kiasi cha kila mtu kuchukua time yake ukae ukijua kabisa kuwa mwanangu ntabeba, simwachi ng'ooo!
 
Ndio maana mpaka leo Mtoto wangu namlea mwenyewe bila Mama,
Wanawake wengi siwaamini kabisa!!!!
Lea baba, tena atakua vizuri sana kuliko angelelewa na mama wa kambo.... Napenda sana nikiona mwanaume mwenye msimamo na mwanae,...

All the best Shark......
 
huwa sielewi mwanamke anapopewa jukumu la kulea mtoto ambaye si wake (namaanisha mama wa kambo) anakua na roho ya tofauti (mbaya)....
ni mara chache unasikia mtoto anaelelewa na mama wa kambo akawa na raha katika maisha!...

huwa ni fujo mvutano mafarakano kusingiziana,ili mtadi tu kupanda na kushuka kwa majambo!...
je haiwezekani mtoto na mama wa kambo kuishi pasi majungu na mivutano???

je baba wa mtoto nae ana nafasi gani katika hili sekeseke?

GTs your highness!.

Sie mababa wa kambo wala hatuna roho mbaya, unalea vizuri mtoto wa mme mwenzio tena kwa upendo wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom