Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia, ni kuwa Mungu alichukua ubavu wa mwanaume aitwae Adam na kumtengeneza mwanamke aitwae Eva. Hiyo ni dhana tosha kwa mtu wa kawaida kuamini kuwa mwanamke aliumbwa akiwa kipande kidogo kilichotoka kwenye umbo kamilifu la mwanaume. Hiyo ni sababu ya kinasaba kuwa; mwanamke humpenda mwanaume katika ukamili wake kwanza na kumtii halafu ndipo anaweza kudai vitu vingine vya nje ya maumbile ya mwanaume. Kwa sababu mwanaume anajua kuwa mwanamke ni kipande tu au sehemu ndogo kutoka sehemu kubwa ya mwanaume hivyo humpenda vipande vipande na kumhurumia.
Na hivyo ndivyo mwanamke anavyojifahamu na kujitambua. Na mwanamke yeyote ambaye hajipendi vipande vipande hata wanawake wenzie lazima wamseme, wamponde na kumsimanga. Ushahidi uliopo, unaonesha kwamba mwanamke yuko tayari kupoteza pesa nyingi sana muda na rasilimali nyinginezo katika harakati za kuboresha au kukarabati sehemu au vipande vya mwili wake. Inaweza ikawa ni uso, nywele, kucha, nguo za kuonesha kitovu, matiti, kiuno nakadhalika…… Linapokuja suala la kutengeneza vipande huwa hawajali madhara au matokeo ya baadae ya kile wanachokifanya. Kwa mtazamo wa haraka haraka inaweza kudhaniwa kuwa wanatangaza bidhaa zao. La hasha. Ukweli ni kwamba kwa asili wao ni kipande tu cha ukamilifu wa utu, linapokuja suala la mwili, sio akili na hisia.
Katika uhusiano na jamii kwa ujumla mwanmke hupenda kusifiwa vipande vipande. Kwa mfano ukimwambia mwanamke kwa ujumla wake kuwa yeye ni mzuri na amependeza; haoneshi kufurahi, bali ataishia tu kusema ‘ahsante.' Lakini ukimwambia kuwa sehemu au kipande fulani cha mwili wake ni kizuri, mfano macho, nywele, kiuno, nk. Hapo atafurahi sana na kutoa kicheko cha aina fulani kuashiria kuwa sasa karidhika, hatimaye jamii imemtambua kuwa yeye ni mwenye kitu fulani bora kuliko wanawake wenzake.