Wanawake na Uongozi: Je ni sababu ya Ngono?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,407
54,886
Naomba tuweke heshima ya forum hii mbele. dada zangu naomba mnisamehe, nawaheshimu.

Jamani hapa jamboforums kumezuka tabia ambayo inataka kuota mizizi. Tabia hiyo ni ya kushutumu wanawake waliofanikiwa kielimu, kiuongozi na kisiasa, kwamba wamepata mafanikio hayo kwa kutumia miili yao.

kuna mambo ya ajabu hapa yametokea hapa jambo forums. Kwa mfano, wanachama tofauti hapa wamedai kiongozi mmoja kutembea na ndugu wa familia moja.

Yaani hata wale ambao wanaonekana wana qualifications bado wanashutumiwa kwa kugawa ngono hata udini, ukabila, kujuana, havipewi nafasi.

jamani naomba busara zetu sote wanajambo forums katika kulitafakari suala hili.

NB:
..Augustino Mosha na Dr.Kichuguu nawaomba mchango wenu.
..Mwanakijiji,KadaMpinzani tuleteeni mtizamo wenu kupitia vyama vya siasa.
..Field Marshal ES, Mzee Mkandara, wazee wa meli, watoto wa mjini. Kuna mengi mnayajua nyinyi.

Mwafrika wa Kike tupe mchango wako.
 
naomba tuweke heshima ya forum hii mbele. dada zangu naomba mnisamehe, nawaheshimu.

jamani hapa jamboforums kumezuka tabia ambayo inataka kuota mizizi. tabia hiyo ni ya kushutumu wanawake waliofanikiwa kielimu,kiuongozi,na kisiasa, kwamba wamepata mafanikio hayo kwa kutumia miili yao.

kuna mambo ya ajabu hapa yametokea hapa jambo forums. kwa mfano: wanachama tofauti hapa wamedai kiongozi mmoja kutembea na ndugu wa familia moja.

yaani hata wale ambao wanaonekana wana qualifications bado wanashutumiwa kwa kugawa ngono. hata udini,ukabila,kujuana, havipewi nafasi.

jamani naomba busara zetu sote wanajambo forums katika kulitafakari suala hili.

NB:
..Augustino Mosha na Dr.Kichuguu nawaomba mchango wenu.
..Mwanakijiji,KadaMpinzani tuleteeni mtizamo wenu kupitia vyama vya siasa.
..Field Marshal ES, Mzee Mkandara, wazee wa meli, watoto wa mjini. kuna mengi mnayajua nyinyi.

..Mwafrika wa Kike tupe mchango wako.
mimi sioni unachoongea humu na ningependekeza uongozi wa jf uangalie uwezo wako wa kiakili na ikibidi ubakizwe msomaji, kwani unapoteza muda wetu....sisi tupo hapa kujadili mambo ya nchi yetu na watu wetu na sio kupoteza muda na nishati kwa hoja zisizokua nakichwa wala miguu.....
 
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, si akina mama wote walio na madaraka wamepata hayo madaraka kwa kupita ngonolaizesheni. Pili, pengine niseme kwa upande mwingine kuwa swala la akina mama kupanda vyeo kupitia mgongo wa ngono sio geni. Hili linaweza kutoweka endapo tamaa za ngono walizonazo wanaume zitatoweka. Kwa ujumla, ngono ni aina ya ufisadi mwingine ambao akina mama wengi kwa kushirikiana na wanaume wenye mapepo ya ngono wametumia kupeana kazi, tenda serikalini, kupanda vyeo, likizo, uhamisho,skolaships, etc. Si vyema kuanza kuwataja majina yao hapa hadharani. Ushahidi upo, hasa kwa viongozi walio katika kada ya makatibu wakuu wa wizara, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, etc. Aidha, naomba nirudie kuweka wazi. Sio akina mama wote, ni baadhi yao tu.
 
mwanamalundi,
nashukuru kwa mchango wako. lakini hivi huoni kwamba kuanzia waziri,mkuu wa mkoa,katibu mkuu,kamishna, hapo mteuzi ni mmoja. sasa atatafuna wangapi? vilevile does he have too? hata kama ana "mapepo," mbona nyama nzuri, tena laini ziko nyingi tu?

yaani hata kupata likizo wanawake inabidi watoe ngono? sasa mwanaume yeye anatoa nini? au ni kwamba wanawake wanahiyo extra advantage?
 
lakini hivi huoni kwamba kuanzia waziri,mkuu wa mkoa,katibu mkuu,kamishna, hapo mteuzi ni mmoja. sasa atatafuna wangapi?

Joka kuu, moja, sio kweli kuwa mawaziri wote (akina mama)ni lazima watafunwe na mkuu wa kaya. Kwanza wengine hawana hata mvuto. Ndio maana nilisema pale awali kuwa ni baadhi ya akina mama. Sasa unaweza kukuta katika kundi la akina mama mawaziri, mkuu wa kaya katafuna mmoja. Katika wakuu wa mikoa, inawezekana ametafuna mmoja, nk.

Pili, mkuu wa kaya amezungukwa na washauri/maswahiba/mawaziri walio karibu naye, ambao pia nao wangependa kuona watu wao wa karibu wanaingia serikalini. Katika kundi hili, wapo baadhi ya akina mama, wanaopata vyeo kwa kupitia mahusiano ya ngono na hawa washauri/maswahiba/mawaziri walio karibu na mkuu wa kaya.

hata kama ana "mapepo," mbona nyama nzuri, tena laini ziko nyingi tu?

Ni kweli nyama zipo nyingi tu. Lakini kumbuka nyama ya jana bei yake ni nafuu kuliko nyama ya leo. Isitoshe, nyama nyingine zina sumu, hazifai kwa afya ya binadamu.

yaani hata kupata likizo wanawake inabidi watoe ngono?

...Kama watachangia, utasikia yaliyowasibu dada zetu. mengine huwezi kuamini.

sasa mwanaume yeye anatoa nini?

rushwa ya pesa, offer ya pombe bar, kujipendekeza kwa bossi, etc.

kwamba wanawake wanahiyo extra advantage?

Wegine wanasema ngono is the oldest profession
 
ama kweli wanaume hawabadiliki, hakuna kitu ambacho tunaweza kukifanya tukapewa credit kuwe we earned it. Sasa kama kuna mwanamke ambaye hajiamini uwezo wake na anasubiri "atongozwe" ndipo apate nafasi mwanamke huyo ni aibu ya wanawake wote. That said, ninawafahamu wanaume ambao na wenyewe walipanda vyeo kwa sababu "mama" aliwachangamkia.

asante.
 
Bi. Senti 50,

Wanaume wanacheza fouls, wakizidiwa na Mwanamke wanaanza visingizio. Wapeni dada zetu respect, walicho nacho wamekipata
kihalali sawa tu na wanaume. Wale waliopata kwa njia za mkato
wapo pia sawa tu na wanaume ambao ni mafisadi na wanauza mali zetu.

Tuache kutanguliza mambo ya ngono tunavyojadili mafanikio au utendaji wa dada zetu labda kama tuna ushahidi wa kutosha. Haya mambo ya hearsay, naona lengo lake ni kudhalilisha wanawake ili wengine wenye uwezo waogope.
 
Unajua watu wana mawazo ya kizamani sana. Sasa kuna wanawake tena huwezi kuwasogelea iwe ni shule au siasa. Ukikaa naye kwenye ana-argue hakuna mchezo. Of course, tatizo bado lipo kwa baadhi ya kina mama huko home, wapo wengi ambao bado wanataka short cut through their nice attractive thighs hasa kwa wenzetu wa CCM! Lakini hao wanazidi kupungua na kina mama wengi tulio nao kwenye utawala ni wazuri zaidi vichwani mwao kuliko muonekane wa nje. Hiyo ndiyo kusema it is their competence and perhaps their ukada that put them where they are.
 
Tunaishi kwenye mfumo dume?
 
ama kweli wanaume hawabadiliki, hakuna kitu ambacho tunaweza kukifanya tukapewa credit kuwe we earned it. Sasa kama kuna mwanamke ambaye hajiamini uwezo wake na anasubiri "atongozwe" ndipo apate nafasi mwanamke huyo ni aibu ya wanawake wote. That said, ninawafahamu wanaume ambao na wenyewe walipanda vyeo kwa sababu "mama" aliwachangamkia.

asante.

Bi senti 50. Kwanza tumetahadhirisha kwamba SI wanawake wote waliopata madaraka/uongozi wamepitia katika mlango huo. Pili, si wanaume wote ambao wanatawaliwa na hayo mapepo machafu ya ngono. Kubisha hilo ni sawa na kubisha kuwa hakuna wachawi wanaoruka angani usiku simply because hujawahi kuwaona wakifanya hivyo.

Inawezekana hata wachangiaji wengi hapa katika forum wameajiri masekretari katika kampuni zao mara baada ya kufanya ngono na hao waliowaajiri. Kwa hiyo unapobisha hii tabia haipo, unatupatia credits sisi wanaume. Ni hayo tu.
 
Bi. Senti 50,

Wanaume wanacheza fouls, wakizidiwa na Mwanamke wanaanza visingizio. Wapeni dada zetu respect, walicho nacho wamekipata
kihalali sawa tu na wanaume. Wale waliopata kwa njia za mkato
wapo pia sawa tu na wanaume ambao ni mafisadi na wanauza mali zetu.

Tuache kutanguliza mambo ya ngono tunavyojadili mafanikio au utendaji wa dada zetu labda kama tuna ushahidi wa kutosha. Haya mambo ya hearsay, naona lengo lake ni kudhalilisha wanawake ili wengine wenye uwezo waogope.

Mtanzania, hakuna anayependa tabia kama hizi ziwepo katika jamii zetu. Akina dada ni mama zetu, shangazi zetu, etc. Na tusingelipenda kuona baadhi yetu tunatumia madaraka/dhamana tuliyopewa na taifa tunazitumia kwa kukidhi matamanio ya kimwili na kurusha roho zetu.

Mtoa mada, Joka kuu, ameuliza: Wanawake na Uongozi: je ni sababu ya Ngono?? Tulichomjibu mtoa mada ni kuwa, jibu lake ni ndio kwa kiasi fulani, na Hapana kwa kiasi fulani. Na tumetoa sababu na uzoefu tuliokutana nao katika ofisi za serikali.

Sasa, kama wewe ndugu yetu unadhani mambo haya ni kudhalilisha dada zetu nadhani unapotea njia. Ni mambo ambayo yapo katika jamii, na yanapaswa kupigwa vita. Ushahidi upo.

Sasa ukisikia daktari anamtongoza mgonjwa mwanamke?? Mgonjwa!!! Utasemaje hapo??.
 
Hayo masuala ya rushwa za ngono yapo sana tu, hasa yale maeneo ambayo utaratibu mzima wa kuajiri haueleweki, na kumuachia mkuu wa kaya kuajiri mtu kama anavyotaka na hakuna wa kuuliza. Mimi mwenyewe nimeona kwa macho yangu, nilikuwa nafanya kazi Kigoma kwenye mashirika ya wakimbizi, utakuta ajira nyingi sana zinapitia mlango huo wa ngono.Na kama unavyosema, baadhi ya wanawake wanaendekeza lakini ni kweli wenngine wako competent huwezi kuwa-approach kijinga namna hiyo.
 
Hili suala lisiishie kwenye ajira na uongozi tu. Lakini pia shuleni na vyuoni kuna madai ya namna hii, kwamba wanafunzi wa kike wanaofaulu kwa alama za juu kimasomo wanakuwa wamehonga ngono kwa wahadhiri na walimu!.Nakumbuka mwaka 2002 nikiwa nasoma chuo, ulitokea mjadala mkali sana kati ya mhadhiri wa somo la taaluma za maendeleo (Development Studies) na sisi wanafunzi. Profesa huyu mwanaume alikuwa anajaribu kufafanua kuwa, kuna baadhi ya wanafunzi wanadai (wanahisi)kuwa iwapo mwanafunzi wa kike kapata alama za juu kuwashinda wanafunzi wenzake, basi itakuwa alihonga ngono kwa mhadhiri.
Hoja ya profesa ilikuwa kwamba, je mwanafunzi wa kike hastahili kupata alama za juu kimasomo? Je kama mhadhiri ni wa kike na mwanafunzi aliyepata alama za juu ni wa kike, hapa napo mnafafanua vipi? Mjadala ulikuwa mkali sana.
Kwa mtazamo wangu, kuna akina dada wengi sana wakali kimasomo, ki-hoja na kimtazamo kuliko wanaume wengi. Nimekutana nao wengi sana na nawakubali kuwa wako imara. Sitashangaa sana kuwakuta katika sekta nyeti wakifanya kazi, kwa hiyo siwezi kuwahukumu kuwa walihonga ngono ili kuwepo pale walipo. Hata kama wengine sikusoma nao wala sifahamiani nao, siwezi kuwahukumu moja kwa moja kwamba wapo pale walipo kwa ssbabu walihonga pesa ama ngono. Nao wana uwezo wa kujitetea katika mahojiano ya kuomba ajira kama sisi wanaume.
Lakini hoja yangu hii haiondoi uwezekano wa kuwepo rushwa ya ngono katika kupata alama za juu kimasomo, kwani nakumbuka kulikuwa na aina tatu za shahada enzi zetu. Kulikuwa na shahada za pesa, (mwanafunzi anayemhonga mhadhiri ili kupata alama nzuri), kulikuwa na shahada za ngono (kama wengi mlivyochambua hapo juu), na shahada za kihalali (kwa wale ambao hawahusiki na tuhuma za hapo juu).
Ila lazima tuwape akina dada heshima wanazostahili, nao wana uwezo kama sisi.
Nawasilisha!
 
Hili suala lisiishie kwenye ajira na uongozi tu. Lakini pia shuleni na vyuoni kuna madai ya namna hii, kwamba wanafunzi wa kike wanaofaulu kwa alama za juu kimasomo wanakuwa wamehonga ngono kwa wahadhiri na walimu!!

IDIMI,

Sema mkuu, tena hawa jamaa wa vyuo wako wengi hapa, lakini hivi mwanamke anaweza kwenda kum rape mwanaume ili atembee naye? Na mbona vyuoni kuna walimu wanawake pia, je hao wanaofaulu kwa ngono, wanaenda kufanya hivyo hivyo na kwa hao walimu wa kike?

Wanaume ndio waanzilishi wa hayo mambo na matokeo yake wanawalaumu wanawake.

Pia kwenye cases nyingi ni hearsay tu. Hakuna ukweli, ili mradi wamewapakazia wanawake. Ninayajua mambo ya mlimani miaka hiyo yaani ni aibu tupu. Tulikuwa hatuwaheshimu dada zetu kabisa.
 
Tuendelee kuelimishana mkuu, hii minong'ono ndio inayoharibu kila kitu. Tuwe ha ushahidi.
 
IDIMI,Mtanzania,Mwanamalundi,Bi.senti 50,...

wanaofika UDSM ni cream of the cream ya wanafunzi wa Tanzania. mtoto wa kike mpaka ajiunge chuo kikuu lazima atakuwa na uwezo.

mazingira[kazi za nyumbani etc] yao dada zetu inawezekana akawa na uwezo kuliko mvulana. kwanini primari,sekondari, na highschool, hawahongi ngono, lakini wanalazimika chuo kikuu?

vilevile,mwanafunzi wa kike atahonga wanaume wangapi ili afaulu chuo kikuu? mimi naelewa chuo kikuu masomo ni mengi jamani. hivi ngono bila uwezo na juhudi inaweza kukupatia degree?

unaweza kukuta mwanamke ana historia ya kufaulu kuliko mwanaume toka mashuleni hadi chuo kikuu. lakini inapofika ktk siasa na uongozi mwanamke huyo analazimika kutoa hongo kwa yule mwanaume ambaye siku zote alikuwa akimzidi.

mimi nadhani hili tatizo linaanza na dharau kwa kina dada. kuna ile hali ya wanaume kujiona zaidi kwa kila hali kuliko wanawake.
 
IDIMI,Mtanzania,Mwanamalundi,Bi.senti 50,...

wanaofika UDSM ni cream of the cream ya wanafunzi wa Tanzania. mtoto wa kike mpaka ajiunge chuo kikuu lazima atakuwa na uwezo.

mazingira[kazi za nyumbani etc] yao dada zetu inawezekana akawa na uwezo kuliko mvulana. kwanini primari,sekondari, na highschool, hawahongi ngono, lakini wanalazimika chuo kikuu?

vilevile,mwanafunzi wa kike atahonga wanaume wangapi ili afaulu chuo kikuu? mimi naelewa chuo kikuu masomo ni mengi jamani. hivi ngono bila uwezo na juhudi inaweza kukupatia degree?unaweza kukuta mwanamke ana historia ya kufaulu kuliko mwanaume toka mashuleni hadi chuo kikuu. lakini inapofika ktk siasa na uongozi mwanamke huyo analazimika kutoa hongo kwa yule mwanaume ambaye siku zote alikuwa akimzidi.

mimi nadhani hili tatizo linaanza na dharau kwa kina dada. kuna ile hali ya wanaume kujiona zaidi kwa kila hali kuliko wanawake.

Aminia mkuu!
Hiki ndicho hasa tunachojaribu kukiweka sawa hapa barazani, kwamba je huyu mwanadada anayekashfiwa kuwa anahonga ngono ili kufaulu, atawahonga wahadhiri wangapi? Hawa mie naamini ni vichwa haswa, wanastahili kuheshimiwa! Chukulia mfano wa dada wa Kitanzania toka kule Kwetu Bulyanhulu ambaye akirudi kutoka shule anakuta marundo ya nguo za kufua, ana jukumu la kupika kwa ajili ya familia, pengine akatafute malisho ya mifugo yao, awaogeshe wadogo zake, baadaye inabidi ajisomee, bado hapo hapo tunamlaumu kuwa anahonga ngono ili afaulu, hii si haki!
There might be something wrong somewhere!
Mfano mzuri, wakati nahitimu chuo miaka hiyo, aliyeongoza kwa kufaulu kwa GPA ya 4.5, kwa darasa letu alikuwa mwanadada mahiri, nilikuwa naona umahiri wake katika mijadala ya makundi. Sikushangaa kusikia kapewa udhamini wa kusoma pale pale chuoni, najua alistahili. Sasa kwa mtu ambaye hajui historia ya huyu mwanadada na akamtuhumu kwamba alihonga ngono ili kupata udhamini, ayakuwa hajamtendea haki kabisa!
Ndio hiki tunachokipinga hapa!
Kama hujatafiti usiseme!
 
Back
Top Bottom