Wanawake na maswali magumu kwa wapenzi wao…!

Hapo penye red ningefurahi kama angesema alikuwa poa lakini wewe zaidi.lol!

Jibu hilo, kwa mwenye akili atajua ni kilemba cha ukoka.............. wampaka mafuta kwa nyuma ya chupa....LOL
 
Mimi: Honey vipi nimenenepa eeh??
Mpenzi: umeongezeka kidogo sana babes.

Yaani hapo najua kanijibu nimenenepa ila siasa nyingi, huh!!..kweli sometimes tuna maswali magumu yanayohitaji majibu muda huo huo tuulizao.
 
Mtambuzi kuna jambo nimejiuliza sana akilini mwangu toka jana usiku, nilikuwa nausoma uzi wa Kaunga, nikaenda nikapitia nyuzi za@darkcity, AshaDii, boss, Mwanajamii one SnowBall Eiyer na wengine kisha nikaona uzi mwingine wa Superman na nyuzi ambazo wewe umetoa na nyingine kibao tu nikajiuliza hivi kweli haya mafunzo kunawatu wanayapata in reality? je michango ya wenzetu huwa tunaifanyia kazi? je tunatoka hatua moja kwenda nyingine in terms of relationships? je kiukweli humu MMU tupo ili kudumisha mahusiano yetu?

kiukweli kama shule humu MMU IPO tena hii ni zaid ya ile ya chuo ila sasa kazi kwa sisi tunaojifunza.

Nakubaliana na ww dada gfsonwin,binafsi kuna mengi ninayojifunza kupitia thread ya hawa wenzetu hasa Mtambuzi na baadhi huwa nayafanyia kazi ila wengine tunashindwa kucomment na kuchangia kutokana na kukosa muda.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom