The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,071
Tatizo kubwa linalotukabili wanaume wengi ni kumtambua mwanamke anayekupenda kwa dhati ya moyo wake.
Kuna wanawake wamefuzu chuo cha sanaa, yaani wanajua kujivika ngozi za kondoo huwezi amini, anakuwa mpoleee lakini akitaka kuvuna anajua tu atakukamatia wapi. wanawake wako tayari kuficha tabia zao halisi hata kwa miaka kadhaa ilimuradi watimize malengo. mwingine atakupeleka mpaka utamuoa akijua kwamba kwakuwa umemuoa basi utakuwa umeridhika kwamba anakupenda. Akishatimiza malengo yake hapo sasa anaanza kuchomoa makucha yake.
Kuna jamaa yangu alipatwa na huo mkasa kaoa mwanamke baadae mwanamke kaanza kuzimikia masharobaro wa mjini wanaopata hela kwa msimu na magari ya kuazima akaacha ndoa yake baada ya masharobaro kumtumia vya kutosha wakaachana nae na huku aliishaachana na mumewe kisa hana hela na wala hajamnunulia gari bahati nzuri jamaa akapata kazi nzuri na akawa anawasaidia ndugu wa mwanamke bila kinyongo na bila mwanamke kujua.
Ndugu wa huyo mwanamke wakawa wanamlaumu kweli huyo mwanamke siku ya siku mwanamke anaenda kuomba kazi hiyo sehemu anakuta mtu ambaye anapswa kumfanyia interview ni the same X-Husband alipata mshtuko sana kiasi kwamba alishindwa kuamini nafikiri interview yenyewe hakufanya kutokana na aibu