Wanawake na hofu ya kusaidiwa na nyumba ndogo

pauline

JF-Expert Member
Dec 26, 2010
650
140
nimegundua hili ni tatizo la wanawake wengi,wanakuwa kwenye mahusiano kimachale machale saa yoyote mumewe anaweza kuwa na nyumba ndogo.....hofu hii imepelekea kuwafanya kuwa watumwa wa ndoa zao,atajitahidi amtreat mumewe kama mfalme/bossi lol,atamfulia,atamnyooshea nguo,atajitahidi awe anaamka mapema amtengenezee chai.........akihofia asipofanya haya mumewe ataenda nyumba ndogo.............................wakina kaka kuweni rensponsible kidogo...chochote unachoona kiko kny uwezo wako kifanye!!!.........................usitafute kisingizio cha kuwa lazy ili uvunje nyumba yako.............ukimwi unaua,sijui niko too westernized ila bado sijamfulia na kunyooshea mtu mzima nguo:smash::smash::smash: hata kupika nitajitahidi kumshirikisha na yeye alternative days...lol
 
Pauline hujapata bado mtu unayempenda kwa dhati acha kufua,kupika na kumpigia pasi utafanya vitu hata hujawaza maishani lol! Mimi kuna msichana alinipenda alikuwa anakuja kwangu na kufanya vyote hivyo na kuninunulia nguo,viatu perfumes hadi chupi hahaha!
 
ukiingia jf kila siku unaweza usioe au kuolewa

ndoa humu zoinaonekana nguuumu mno

Kweli kbc mkuu..unaanza kupata hints kwanza b4 you move in...inakuwa ya kufikirika vle..ukiingia napo unakaa kimachalemachale.
 
Kama ni kweli na una mahusiano imara, hongera sana! Wanaume wengi wanasaidiana shughuli mbalimbali na wake/wapenzi wao lakini sidhani kama kuna idadi kubwa kati yao wanaofurahia kauli kama zako kutoka kwa wake au wapenzi wao.

nimegundua hili ni.............ukimwi unaua,sijui niko too westernized ila bado sijamfulia na kunyooshea mtu mzima nguo:smash::smash::smash: hata kupika nitajitahidi kumshirikisha na yeye alternative days...lol

Kutokumfulia jamaa ni jambo la kawaida na inawezekana likaja kwa njia ambayo bado ni romantic lakini eneo lenye red linaashiria huwathamini watu unaokuwa nao katika intimacy. Mwanamke anayependa na kupendwa ni vigumu kukuta anamzungumzia mtu ambaye wako in love kwa kutumia phrase "mtu mzima" tena ktk sentensi sawa na uliyotumia. Ninaowajua wengi wameishia kuwa so bitter kwa kutopata mapenzi wanayotamani pasipokujua tatizo ni kauli zao.

Tafakari kauli zifuatazo ujue ninakusudia kukujuza nini:
Mpenzi X: Honey, kufua kunanipa tabu sana. Can we please do it together?......mmh..?.......Please...!
Mpenzi Y: Fua nguo zako mwenyewe my dear, mi siwezi kumfulia mtu mzima na sijawahi kumfulia katika maisha yangu.
Majibu wanayotarajia kupata hata kama hayata tamkwa kwa sauti ni haya hapa.
Kwa Mpenzi X: Usijali mpenzi nitafua mwenyewe. Just sit there and watch.
Kwa Mpenzi Y: Bitch! (rohoni) Unaumwa nini? (akilini). Unasemaje..?
 
Dada sijajua imani yako,lakini nina wasiwasi na ufaham wako kuhusu kujitambua wewe ni nani!
 
Nakubaliana nawe. Pengine watu wa aina ya huyu mdada ndiyo wanafanya ndoa kuonekana ngumu kama alivyosuggest The BOSS utu uzima na mapenzi wapi na wapi. Kwenye mapenzi ndiko watu hugeuka watoto halafu Pauline anaitoa kwa kiburi utadhani kaachika jana bana.

Dada sijajua imani yako,lakini nina wasiwasi na ufaham wako kuhusu kujitambua wewe ni nani!
 
Mume wangu ni smart sana, kwa hiyo sijawahi kumyooshea nguo kwani anaona yeye hiyo kazi anaiweza zaidi. Lakini kufua nafua. Tuna washing machine nguo zinafuliwa na machine. boxers zake nafua kwa mikono yangu na wala sioni kama ni kuonewa kwa kuwa NAMPENDA kupita maelezo!

Inategemea uko kwenye stage gani ya ndoa. Kwani nakumbuka nilipoolewa nilienda kwa wakwe zangu. Wakati nimekaa nje nafua mume wangu akaja kunisaidia imagine mbele ya mama na bibi yake! Bibi akasema unabahati umepata mume anayekujali.

But with time aliacha kufua na mimi mwenyewe nguo zangu na zake nafua kwa nadra sana kwani tuna H/girl na machine. Ila chupi namfulia na nitaendelea kufanya hivyo.

Hivi kwa Tz kuna kazi gani mpaka mtu utake mume nae akusaidie. Kwa sababu unaweza kuwa na mahouse girl hata wawili sasa sioni kwa nini umpigishe deki mtoto wa mwenzio.

Hao wanaokaa ulaya waache wasaidiane kwani najua mziki wa kuishi nje hamna cha housegirl kwa hiyo msaada ni muhimu.
timiza wajibu wako, kila kitu kitakuwa saaf.
 
Pauline hujapata bado mtu unayempenda kwa dhati acha kufua,kupika na kumpigia pasi utafanya vitu hata hujawaza maishani lol! Mimi kuna msichana alinipenda alikuwa anakuja kwangu na kufanya vyote hivyo na kuninunulia nguo,viatu perfumes hadi chupi hahaha!

hahaha lol bado anafanya hivyo au uliachana naye??na wakina kaka wakipenda huwa wanafanya nini?au mapenzi yako one sided ni wakaka tu ndio wanaopaswa kufuliwa nguo,kunyooshewa out of love?:dance:
 
Mume wangu ni smart sana, kwa hiyo sijawahi kumyooshea nguo kwani anaona yeye hiyo kazi anaiweza zaidi. Lakini kufua nafua. Tuna washing machine nguo zinafuliwa na machine. boxers zake nafua kwa mikono yangu na wala sioni kama ni kuonewa kwa kuwa NAMPENDA kupita maelezo!

Inategemea uko kwenye stage gani ya ndoa. Kwani nakumbuka nilipoolewa nilienda kwa wakwe zangu. Wakati nimekaa nje nafua mume wangu akaja kunisaidia imagine mbele ya mama na bibi yake! Bibi akasema unabahati umepata mume anayekujali.

But with time aliacha kufua na mimi mwenyewe nguo zangu na zake nafua kwa nadra sana kwani tuna H/girl na machine. Ila chupi namfulia na nitaendelea kufanya hivyo.

Hivi kwa Tz kuna kazi gani mpaka mtu utake mume nae akusaidie. Kwa sababu unaweza kuwa na mahouse girl hata wawili sasa sioni kwa nini umpigishe deki mtoto wa mwenzio.

Hao wanaokaa ulaya waache wasaidiane kwani najua mziki wa kuishi nje hamna cha housegirl kwa hiyo msaada ni muhimu.

na yeye huwa anakufulia au yeye hakupendi kuliko maelezo??:smow:
 
hahaha lol bado anafanya hivyo au uliachana naye??na wakina kaka wakipenda huwa wanafanya nini?au mapenzi yako one sided ni wakaka tu ndio wanaopaswa kufuliwa nguo,kunyooshewa out of love?:dance:
Tuliachana,mimi nilikuwa namfulia chupi na sidiria na pia kuzinunua lol!
 
na yeye huwa anakufulia au yeye hakupendi kuliko maelezo??:smow:

Mapenzi sio mashindano.Kama upo kwenye mahusiano/ndoa tu bila mapenzi(kwa faida binafsi) ndo utaanza ‘mbona we hufanyi hivi na vile‘.Hayo ni maisha ya kukomoana!
Kila mmoja anafanya size yake...wapo wanaofua...wapo wanaosaidia hata jikoni...wapo wasioisha kutoa zawadi kama alama ya shukrani n.k
Sidhani kama kuna mwanaume anayekulazimisha umfanyie yote hayo...ila kama ni mpenzi wako na unapenda apendeze utapenda kumfanyia wewe ili kuhakikisha anakua smart at all times.

Kwa mara nyingine MAPENZI SIO MASHINDANO....fanya unachoweza na uachane na mbona wewe mbona wewe!!
 
Mapenzi sio mashindano.Kama upo kwenye mahusiano/ndoa tu bila mashindano ndo utaanza ‘mbona we hufanyi hivi na vile‘.
Kila mmoja anafanya size yake...wapo wanaofua...wapo wanaosaidia hata jikoni...wapo wasioisha kutoa zawadi kama alama ya shukrani n.k
Sidhani kama kuna mwanaume anayekulazimisha umfanyie yote hayo...ila kama ni mpenzi wako na unapenda apendeze utapenda kumfanyia wewe ili kuhakikisha anakua smart at all times.

Kwa mara nyingine MAPENZI SIO MASHINDANO....fanya unachoweza na uachane na mbona wewe mbona wewe!!

mapenzi sio mashindano...ila mapenzi pia si utumwa kama wote mko in love then mtakuwa rensponsible kwa mambo yenu huyu akishika hiki,mwingine atashika kile ili siku ziende......
sidhani kama ni wajibu wa mke kuhakikisha mumewe anakuwa smart all the times,ni wajibu wa mume kufanya hivyo....na mke pia yuko rensponsible kwa usmartness wake sio wajibu wa mume...tusibebeshane mizigo!
 
mimi naamini kila ndoa ina formula zake.na inategemea jinsi wenyewe mlivyozoeshana.mimi kwa upande wangu,simfulii chupi m.me,na anaemfulia simuoni wa ajabu,kwani huyo m.me nae anaweza akawa anamfanyia m.ke mengine mazuri tu.ila kufanya kila kitu kwa kuogopa mume kuwa na nyumba ndogo.m.me hata umfanyie nini akiamua kuitafuta nyumba ndogo,ataitafuta tu.
 
Ni kweli kuwa hofu na wasi wasi vipo sana na vina play part kubwa kwenye mahusiano na ndoa lakini pia mapenzi hayana formula, ni vile mtu anavyojisikia kumfanyia mwenzio na mara nyingi its uncontrolable, so kumfulia, kumpikia... mtu anafurahia kuvifanya na ni kitu kizuri kwa mtazamo wangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom