Wanawake muolewe na wanaume wenye nyumba tayari

Umenichekesha sana mdogo wangu Fixed Point??

Kwa nini mnampa Natalia prescription ya ugonjwa usio wake??

Nyie msaidieni katika kile anachokihitaji....Sidhani kama haya mnayoyasema anayataka!

Ndo maana mie nimeamua kumpenda (sema tu maji yalishamwagika)!!

Babu DC!!
najua babu, nimeamua tu kumpasha upande wa pili wa shilingi.
hela, majumba, magari..... siyo kila kitu katika maisha.
babu wewe mpende tu, ila kama unavyosema bibi tayari alishawahi namba
 
Bibi DC anajua majuto haya uliyonayo ya kushindwa kumposa marehemu natalia (naona keshalambwa ban, sijui mzungu kamnunulia chopper?

Wewe King'astisasa unataka kuniletea kasheshe?? Bibi atajuaje wakati mie naugulia kimoyo moyo??

But ni kweli....Natalia ni kind of special girl/woman......Labda mie naona haya kwa sababu ya makengeza yangu!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
najua babu, nimeamua tu kumpasha upande wa pili wa shilingi.
hela, majumba, magari..... siyo kila kitu katika maisha.
babu wewe mpende tu, ila kama unavyosema bibi tayari alishawahi namba

Lakini hayo "the would be" mpenzi wangu Natalia hayataki.......Kwa nini msipe ushauri anaohitaji kuusikia??

Unadhani angekuwa anaandika watu kazi, wewe ungepata ajira kwenye kampuni yake??

Mie naona ningepewa walau kazi ya ulinzi ili nijikumbushe kutupa nchale!!

Babu DC!!
 
Yupo mwanamke mwenzio namfahamu alitaka wenye nyumba na magari km wewe unavyotaka, na kwa kweli alimpata jamaa mwenye majumba na magari, Kilichotokea ni kuwa yule mwanamke hakuwa na raha ya kukaa pale nyumbani kwani muda wote jamaa alikuwa yuko bize na miradi yake na wakati wa kujirusha ukifika anawachukua watoto wake anaenda nao beach mama akitaka kwenda anaambiwa kuwa yeye ni hapo nyumbani eti kwa sababu nyumba ilikuwa ina kila kitu ambacho mwanamke huyo alikihitaji. Cha kushangaza hata gari alikuwa analitumia kwa ruhusa maalum toka kwa mumewe akichukua maamuzi yake mwenyewe ya kutumia gari anaambulia kipigo............... Akijiachia sana sebuleni anaambiwa hana sababu ya kujiachia kiasi hicho kwani hajui gharama ya ujenzi wa nyumba. Wakija ndugu wa mwanamke wanapangishiwa guest house eti hawana hadhi ya kukaa kwenye nyumba hiyo kwa sababu ndugu yao (Mwanamke) hajachangia chochote hivo haruhusiwi kuleta wageni hapo nyumbani
Sasa nikuulize hizo nyumba na magari vinamfaa nini huyu mwenzio mwenye akili tegemezi, maana ni afadhali kuvumilia kelele za mwenye nyumba na purukushani za kugombea daladala kuliko hizi kashfa ila kama unazitaka wewe nenda tu ukakae kutwa nzima na hayo majumba na ushinde na gari halafu uone km hilo gari litapanda kitandani wakati wa menu za usiku wa manane...................
Uamuzi uko kichwani mwako
huyo mume alikuwa na yake, siyo sababu mke hakuchangia kitu
 
Lakini hayo "the would be" mpenzi wangu Natalia hayataki.......Kwa nini msipe ushauri anaohitaji kuusikia??

Unadhani angekuwa anaandika watu kazi, wewe ungepata ajira kwenye kampuni yake??

Mie naona ningepewa walau kazi ya ulinzi ili nijikumbushe kutupa nchale!!

Babu DC!!
lakini babu ukisoma post yake yeye ndo anatushauri kuwa tukitaka kuolewa tutafute "MKAMILIFU", hataki ushauri wa mtu, mimi nilikuwa nampa experience yangu tu ili aone huko kwingine pia kunalipa
 
Inawezekana hukutegemea km mamako anaeza kuwa katibu mkuu, cyo kngne nahc ulimbukeni unakusumbua! Poyeee
 
Yaani mnatoka povu na post za Natalia? Mtajiumiza vichwa bure,huyo mtu si wa kukupopotezeeni muda!Fuatilieni thread zake tu mtakubaliana na mimi.
 
Huyo mwanamume hana tofauti na mtu aliyenunua machine ya kutotoa vifaranga kutoka china.....Kwani wachina watakuwa wanamdai kitu??

Babu DC!!
nashangaa sana.
kama umebahatika kuwa na hivyo vyote kabla hujaoa siyo sababu ya kumnyanyapaa mwenzako. kuna watu wengine wanapenda wajikamilishe kwanza ndo waingie kwenye ndoa ili kuepuka kugawanya ada na hela ya site
 
tunamjua na wala hatutoi povu, haya ni "mazungumzo baada ya habari" tu

Mwanzoni nilihis huenda huyu Natalia katoroka mirembe, kumbe ni mazungumzo baada ya habari tu! Ila ingependeza kama angekuwa na 'mume' wake wwe wanaongea kama Julius Nyaisanga na Yule mtangzaji mwingine, jina nimelisahau, kwenye kibwagizo cha kile kipindi cha BP cha Idhaa ya Biashara...............!
 
Inawezekana yeye yupo serious, ila sisi wachangiaji ndo tupo kwenye mazungumzo baada ya habari aliyotoa
 
Back
Top Bottom