Wanawake mna tatizo gani?

Kwanini wanawake walio wengi (sio wote) wanakubali kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume walio na huruka ya kulala na wanawake walio tofautitofauti (play-boys) ingawa wanawake hao wakifahamu fika juu ya tabia za play-boys hao? Nataka kujua kitu gani kinawasukuma kufanya hivyo? Nasema haya baada ya tafiti nilizozifanya za kimazingira si za kisayansi katika maeneo mbalimbali ambyo nimeishi ni si Tanzania bali ni nchi tofauti katika mabara tofauti.

Huenda wengine wakasema tatizo ni pesa la! si kweli huenda kwa baadhi, nasema hivyo kwa sababu mimi naishi kwenye mazingira ambayo watu wote wote wanaoishi hapa wanaume/wanawake wote wanapesa za kutosha kabisa lakini tabia ipo.

Kwakuongeza kuna dada mmoja mgeni alifika hapa na tukawa tunaongea kirefu kuhusu bwana mmoja mwenye tabia hiyo, na huyu dada anaonekana yupo decent, ana elimu ya juu sana na senio staff, chakushangaza wakati narudi toka likizo nikakuta yeye ana mahsiano ya mapenzi na huyo jamaa aliyekuwa akimkandia siku moja. Si yeye tu bali ni wengi, wsomi na wanapesa, why? Kama wasingekuwa wanakubali huyu jamaa asingepewa jina la play-boy, ni kwa sababu tu anawapanga na anaendelea kufana hivyo kwa kila anayekuja. Huyu jamaa, nimetolea mfano tu si kwamba yeye tu ali wengi waliokama eye ni rahisi kukubalwa na wanawake.

Wana jf ebu nielezeni, ni kwanini hii inatokea sana?
ndugu yangu kuna njemba zina ngekewa ya kupendwa na wanawake we acha tu utadhani imechanjia.
 
Back
Top Bottom