Wanawake: Mkitukubalia kirahisi thamani inashuka…….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Wanauchumi wawili David Anderson na Shigeyuki Hamori wanasema kwamba wale wanawake ambao wanapotongozwa kwa mara ya kwanza huwa wagumu hata kama wanapenda, huwa wanaonekana kuwa na thamani kwa wanaume wanaowafuata ukilinganisha na wale ambao huwa hawana kujivuta –vuta kwa aina fulani. Wanauchumi hawa hata hivyo huenda hawajui kwamba jambo hilo lilikuwa linafanyika kwa miaka mingi huku Afrika. Kwa mila za Kiafrika mwanamke hatakiwi kumkubalia mwanaume kirahisi, hata kama anampenda. Hata katika mafunzo ya unyagoni wasichana huwa wanafundishwa kuwa ‘wagumu' wanapofuatwa na wanaume, bila kujali kama wanapenda au hawapendi. Hali hiyo ndiyo ambayo impelekea wanawake wa Kiafrika kushindwa kuwaambia kwanza wanaume kuwa wanawapenda, badala yake husubiri kwa maumivu hadi pale wanaume wanapowaambia.

Wataalamu hawa wanaunga mkono mila zetu za Kiafrika kwa kusema kwamba, iwe ni Ulaya, Asia au Afrika, mwanamke kukubali haraka ombi la mwanaume huwa kunashusha hadhi ya mwanamke huyo. Wanasema hii ni kwa sababu kwa asili watu huwa wanahisi kwamba, bidhaa ambazo ni adimu au zenye bei kubwa huwa ndizo zenye thamani zaidi. Hisia kama hizi haziishii kwenye bidhaa, bali huenda hata katika uhusiano. Kwa mfano unapokwenda dukani kutaka kununua bidhaa fulani ambayo huijui vizuri, kigezo kitakachokuongoza kwenye kujua ubora wake kinaweza kuwa bei. Ile ambayo itakuwa na bei kubwa, itakushawishi kwamba ndiyo imara zaidi. Kwenye suala la mwanamke kufuatwa na mwanaume, wataalamu hawa wanasema mwanaume huwa anaangalia kitu ambacho naweza kukiita, ‘kiwango cha uwanauke' wakati akimtaka mwanamke kwa mara ya kwanza.

Kama mnunuzi wa bidhaa anavyoongozwa na kiwango cha bei kukadiria ubora wa bidhaa, mwanaume naye huongozwa na ‘ugumu' wa mwanamke kutambua kwamba mwanamke huyo ana thamani au urahisi wake kutambua kama hana thamani. Hata hivyo inatahadharishwa kwamba mwanamke anapokataa kwa sababu tu ya kulinda thamani yake, lakini akiwa anapenda, awe na kiwango. Kukataa kwa namna fulani kunaweza kuwafukuza wanaume kabisa hadi mwanamke kudhani ana nuksi………….
 
mtambuzi hayo mambo ya analogue! cku hizi ni kubonyeza batton na kusonga! waeza zungushwa miaka na ukakuta beseni vilevile au masewage yanayofura! na ukapewa ndani ya wiki lakini kitu kinavuta kama volcano na bado mile gauge inasoma 50! we babu mtambuzi wewe, shaurilo! sijui na mababu wenzako kama wakina DC, asprin nao wako hivi au ni wewe tu! lolest!
 
Mkuu thamani ya mwanamke ipo pale pale haijarishi kakubali mapema au la
 
Tunashukuru sana kwa hii habari
Nina swali na wale wanawake wanaowadondokea wanaume na kutupa ndoana inakuwaje hahaha baada ya kukubaliwa anatakiwa aanze kumzungusha njemba huyo aliyekubali nafasi hiyo?Njemba si anaweza kukata kamba Mzee Mtambuzi inakuwaje ?:confused2:
 
Tunashukuru sana kwa hii habari
Nina swali na wale wanawake wanaowadondokea wanaume na kutupa ndoana inakuwaje hahaha baada ya kukubaliwa anatakiwa aanze kumzungusha njemba huyo aliyekubali nafasi hiyo?Njemba si anaweza kukata kamba Mzee Mtambuzi inakuwaje ?:confused2:
Nimeshasema hata kuzungusha pia kufanywe kiakili, sio kwa kutweza, maana wapo wanaume ambao hawana subira, wakizungushwa mara mbili wanakata kamba.....................
 
Kati ya mabara ambayo nimewahi kufika hapa duniani, nadhani bara la Asia linaongoza kwa wanawake wake kuwa wagumu sijui ndio wanafuata sana mambo ya mila au....
 
mtambuzi hayo mambo ya analogue! cku hizi ni kubonyeza batton na kusonga! waeza zungushwa miaka na ukakuta beseni vilevile au masewage yanayofura! na ukapewa ndani ya wiki lakini kitu kinavuta kama volcano na bado mile gauge inasoma 50! we babu mtambuzi wewe, shaurilo! sijui na mababu wenzako kama wakina DC, asprin nao wako hivi au ni wewe tu! lolest!
Hata kama ni kwa kubonyeza kufanywe kiakili, unadhani ni mwanaume gani atamthamni mwanamke aliyemtongoza siku hiyo hiyo na kumega siku hiyo hiyo........."kahaba....!"
Labda kama unazungumzia ... "one night stand..." lakini kwa mwanaume anayetaka serious relationship, lazima atajiuliza, "kama mimi kanikubalia kirahisi namna hii, je keshawakubalia na kumegwa na wanaume wangapi...?"
 
Jamani kuna wanamme wa kudengulia, na unaweza 'play hard to get"

Kuna wengine, kabla hata hajaongea umeshasema 'Yes'

haya mambo ya kudengua inategemea na aina ya mwanamme pia lol

Yaani unanishauri nimdengulie fulani? Thubutu!
 
Back
Top Bottom