Wanawake huzeeka haraka kabla ya wanaume (maranyingi)

DrRonny

Member
Dec 26, 2011
31
10
Halooo, habari zenu wanajamii wote, wakaka na wadada. Karibuni mchangia maada hii kwa hoja za msingi. Maranyingi katika jamii huwa tunaona kuwa katika ndoa, baada ya kujifungua mtoto au watoto mwanamke huchakaa ghafla na hadi mwanaume anaonekana alioa mwanamke mwenye umri karibu sawa na mama yake.

Hata kama wataishi maisha ya bila kuzaa, hili pia huweza tokea. Na hata kama wakiishi bila mapenzi yaani ngono. Na tukiachilia mbali kuwa kuna watu waliojaliwa kuwa na umri mkubwa ila bado anaonekana ni kijana.

Je, nyinyi mnadhani tatizo lipo wapi?
Je, inahepukika?

Karibuni.
 
Hao walikuwa wanawake wa zamani (tafuta thread ya 'mbu' juu ya ndoa za siku hizi dhidi ya za zamani utaelewa sababu)
Wanawake wa siku hizi hatuzeeki manake hatukubali stress. Ukijaribu kum-stress unaishia wewe kuwa frustrated. Ndo maana unaona siku hizi vilio vya wanaume na wanawake viko sambamba kama sio vya wanaume vimezidi,lol!
 
Tukiangalia kwa upande mwingine wanaume wengi wanawahi kufa na kuacha wake zao, hata ukiangalia waloathirika mwanaume anawahi kufariki nayo inachangia na nini?
 
Swala la kuwahi kuzeeka halina mahusiano na jinsia .Hujaona mwanamke ana wwtoto watatu na bado anafunga belt kiuno chembamba,hilo ni swala la mtu binafsi kujiachia,hata mwanaume asipojitunza atawahi kuzeeka.
 
kuzeeka kwenye ndoa vinaendana na jinsia...wanawake hasa wanaozaa au hata wale wasiozaa lakini wanaofanya sana ngono tena na watu tofautitofauti huzeeka haraka kuliko wanaume walio na umri sawa na wao...hii ni kwasababu, akipata mimba, mwili huwa unaumuka ukija kujirudi basi hata kama atapewa chakula safi bado utakuwa umeshajegejela kidogo..hiyo haipingiki....akizaa kila baada ya miaka miwili mtoto, lazima ananyong'onyea sana.
 
Du mpaka leo watu mnafikira kama hizi basi masister wasinge zeeka.Fanya utafiti kwa wanawake wa sasa kama kuzaa kuna wazeesha.
Zamani hasa vijijini ilikuwa hivyo kwa sababu mwanamke anazaa watoto 9,10 na kuendelea
bado kulima kunamngoja,kutwanga,kwenda kutafuta kuni,matokeo yake miaka 25 anaonekana mzee.
 
wa siku hizi wengi umri wao tofauti na muonekano wao wa miaka 47 kama 35 kweli tena:eyebrows:
 
Wanajiachia sana mwanamke inabidi ajimantain(figure) na asiwe tipwatipwa(sanamu la michelini)
 
Sio kweli!!
Kinachozeesha watu ni kula na matunzo duni bila kusahau stress.
Kuna wanaume ,tena nisema vijana wa chini ya miaka ishirini ila ukiulizwa umri wao unaweza ukajibu 40. Mtu asipokula vizuri kwa mpangilio,akiwa na mawazo/stress kedekede, asipoujali mwili na muonekano wake lazima azeeke kabla ya muda, awe mwanaume au mwanamke.
 
Lazima tuzeeke, kuujaza ulimwengu si kazi ndogo bado kuwa hoteli ya mtu mwingine.

Cheki tu hilo jamaa kwenye avatar yangu linachofanza.
 
Back
Top Bottom