mie nilidhani wanaume ndio mnapenda ndio maana wanawake wengi siku hizi nusu uchi. Sio lazima kila fashion inayoingia uige. Hata ya kukudhalilisha pia unaiga? kwani lazima uende na wakati? mwingine miguu kama fimbo, lakini ndani ya kimini na mguuni ana bonge la CL, basi utadhani mbuni katoroka ikulu.
na mwingine unamkuta mapaja meupeeeee peeeeee. mwingine giza tupu. halaf anakuonyesha hadi kichupi kimepanda kwa juu
Hiyo ndio size yake kwake,wewe ni nani wa kumpa maelekezo kwamba size ni ipi?
Mwanamke ni mtu mzima,kwanini udhani kwamba una haki ya kumpangia cha kufanya au kuvaa,jamii ya Kiafrika ina penda sana kucontrol wanawake inaboa kiukweli.
Lakini kama ukahaba si wangu,mtu mwingine inamuhusu nini?
Hayo ni mawazo yenu tu, na kwakuwa wengi wenu huwa mnayapelekea mawazo yenu kwenye ngono, ndo maana mnakuwa offside!! Hivi mnajua style asili ya mwafrika katika kuvaa? Waweza chukua mfano wa filamu za kinigeria zile za kiasili au hata ile ya kina bushmen tu.......upaja nje, kitovu nje tena saa zingine hadi kwa wale mabinti unakuta vititi vipo nje kabisa!! Sasa kwangu mimi ukahaba utoke wapi??
Basi usihangaike kupandisha ama kuficha, tujionee sinema ya x uliyoitengeneza mwenyewe, na hy ndo concern ya mitishamba
sasa anahangaika nini kukivuta chini? au nayo ni style?
think outside the box bana!
Sasa huangaikia nini kama hilo ndio pangilizi lake!
Mwanamke ni mtu mzima,kwanini udhani kwamba una haki ya kumpangia cha kufanya au kuvaa,jamii ya Kiafrika ina penda sana kucontrol wanawake inaboa kiukweli.
Kwa nini wewe ukereke akikivuta ni chake na yeye ni mtu mzima.
Pale unapowashirikisha wenzio na ndio mtowa mada akasema hiyo senema iwachiliwe tu watu wafaidi.
Kuvuta au kutokuvuta it's my bussiness, ni hiari yangu na haimuhusu mtu mwingine,huyo anayekereka hana kazi na muda wake.
Kwanza sio kila mtu anayevaa kimini anahangaika,na hata kama anahangaika bado ni chaguo lake binafsi.
Kufaidi au kutofaidi ni tatizo la huyo mtazamaji binafsi,kwa hiyo yeye ndio atafute ufumbuzi na sio mvaaji.
Nashauri acheni kupigana vita ambayo hamtaiweza, Tanzania ni nchi huru.
Naona kama wewe huzingatii huo uhuru, kwani kuna tatizo sisi kusema maoni yetu? Unafikiri dunia hii kila mtu afanye anavyotaka ...... Wapi kwani upo hapa kwenye forum kwa kazi gani? Nini maana ya kubadilishana mawanzo?
na kwa upungufu huo wa akili...tutawacontrol mpaka mnaingia kaburini...mana hamjiheshimu hata kidogo...