Wanawake acheni usister duh kwenye mambo ya msingi

Kichwa Ndio Mtu

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
3,079
1,706
Inawezekana vipi dada mtu mzima usijue ratiba za period yako?

Najua period haina kanuni maalum inaweza kukutokea ghafla lakini kwa dada anaejitambua lazima atachukua tahadhari.

Jana nimejisikisia aibu sana kwenye daladala baada ya dada mmoja kumwaga radhi. Dada ameingia period ghafla kwenye daladala, anajifanya sister du hana hata mkoba awe amabeba zile taulo za usafi, alikua kavaa vile vinguo vinaitwa kondom(skin wao wanaita). Nimejisikia aibu sana jana.

Kwenye daladala bahati nzuri kulikua na mama akampa kitenge ajistili. wadada kuweni makini bhasi msituaibishe.
 
aseee ni aibu kwa kweli period hata iwe vipi lazima utaona dalili tu sipati picha alivungajeee ahah halafu dada unatoka kwenda mbali bila handbag mkononi wengine wanadhani ni fasheni kubeba ila ukweli zinatusaidia kubeba vifaa muhimu kama hivyo hata kanga pia
 
Hyo mdada hata ajielewi.. Yaan anatembea bila hata kimtandio huo sasa sio usista du huo ni umburulaaa
 
ila jamani hicho kitu nani asiyekijua katika maisha ya sasa!!!
mimi sioni aibu imetokea wapi ni sawa na mgonjwa wa kifafa tu muda wowote anaanguka na wote wanajua ni kifafa!!!
hapo kila mtu alijua ni period mbona kawaida tu...
 
Yani kuanzia nilpokua kabinti ile nikitaka kutoka mama ananiuliza kama nimebeba kanga au mtandio....Nilikuwa sijui maana yake, nlikuwa nakasirika ila kumbe ina maana kubwa.
Njiani kuna mengi, achilia mbali kuchinja kuku unaweza kupoteza fahamu ghafla, watu watakustiri na kipedo chako au?
 
Mimi naamini hali hyo inaweza kutokea ghafla na bila dalili yeyote.......kosa lake kutembea bila kitenge au mtandio ili kama chochote kikitokea kitakusaidia kujistiri mpaka pale utakapojistiri vyema.Na sio period tu kuna mengine mengi...nguo imechanika ghafla unajisitiri vp.
 
cha kushauri hapo ni mdada kuwa na utaratibu wa kutembea na either kanga, kitenge kikoi au mtandio kwenye poch full stop ....mana hiyo hainaga formula maalum...na sidhani kama mdada anaeza fanya makusudi akiwa na akil timamu!! Ni kutokujua tu.
.
 
Sidhani.kama kuna haja ya kumlaumu huyo dada....

Shit happens sometimes.....

Na siku ya kutembea uchi ndio ya kukutana na mkweo
 
Huhuhuuuu nimecheka si kama ni mazuri ila nimeona kuwa nami laweza kunikuta vile nimezoea kuzulura na kiwallet pekee. Pyuuuuu!
Pole yake kwa hiyo ajali aliyoipata
 
Inawezekana vipi dada mtu mzima usijue ratiba za period yako?

Najua period haina kanuni maalum inaweza kukutokea ghafla lakini kwa dada anaejitambua lazima atachukua tahadhari.

Jana nimejisikisia aibu sana kwenye daladala baada ya dada mmoja kumwaga radhi. Dada ameingia period ghafla kwenye daladala, anajifanya sister du hana hata mkoba awe amabeba zile taulo za usafi, alikua kavaa vile vinguo vinaitwa kondom(skin wao wanaita). Nimejisikia aibu sana jana.

Kwenye daladala bahati nzuri kulikua na mama akampa kitenge ajistili. wadada kuweni makini bhasi msituaibishe.

Haipendezi kwakweli
 
Hakika tuko tofauti.... yan bidada hajaona hata dalili mweee kuna watu wana raha sana aiseee khaaaa ila alitia aibu mmxiiuuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom