Wanawake acheni kujibadilisha maumbile

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Asha Bani

HIVI karibuni vyombo vya habari viliripoti taarifa za kuwapo kwa mashine ya kunyanyua matiti ili yaweze kusimama kwa yale yaliyoanguka.
Licha ya vyombo vya habari kuandika suala hilo, pia kumekuwa na tabia au desturi iliyojengeka kwa wanawake wengi kujibadilisha maumbile yao ikiwa ni pamoja na rangi na makalio kwa kutumia dawa mbalimbali.

Lakini kubwa lililonisukuma kuandika uchambuzi huu ni kutaka kuwatahadharisha wanawake kuacha tabia ya kujibadilisha maumbile na hata muonekano wao halisi, kwani hii inaonesha ni jinsi gani wanashindwa kumkubali muumba na kupingana naye kwa kutumia kemikali, jambo ambalo ni hatari.

Hata hivyo Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) inafanya jitihada kubwa za kupambana na bidhaa bandia ili kuwalinda wananchi wake wasijiingize katika vishawishi vya kujiharibu.

TFDA imekuwa katika mstari wa mbele kupambana na vipodozi vyenye kemikali mwilini ambavyo vingi vina sumu inayojulikana kwa lugha ya kitaalamu ‘Lanolin’, ambayo ni hatari kwa kuwa inachubua ngozi na kusababisha saratani ya ngozi.

Vile vile hivi karibuni kulikuwa na taarifa za wanawake ambao wanatumia dawa za kuongeza makalio ili yaweze kuwa makubwa, jambo ambalo ni hatari. Na kwa wale wenye mawazo ya kufanya jambo hilo wasithubutu.

Katika hili, kwa wale wanaopenda kufuatilia taarifa mbalimbali za habari wanaweza pia kuwa na kumbukumbu ya hapa nchini, ukiondoa ile ya mke wa kigogo mmoja aliyenusurika kifo baada ya kuharibika umbile lake la awali kwa kukuza kalio moja na jingine likabaki kuwa dogo, jambo

ambalo ni hatari na pia alijitia aibu hata kwa taifa na familia yake pia.
Nimeeleza haya ili kama kuna mtu anafikiria kufanya jambo kama hilo asifanye tena, kwa kuwa lina madhara ya kuharibika kwa ngozi na hata kuharibu umbile lake la awali na wakati mwingine kupoteza hata maisha.

Lakini kubwa zaidi la kuzungumzia leo ni hiki kitu kipya kilichoingia, yaani mashine ya kunyanyua matiti, hili ni suala jipya na la hatari kwani hata Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, amelitolea ufafanuzi suala hilo kwa kusema lina madhara endapo utatumia mashine hiyo inayojulikana kwa jina la ‘Beauty Machine.’

Wataalamu wengi wametoa tahadhari kuwa ni hatari, lakini kwa wanawake kuna jambo la kujiuliza; hivi ni lazima kila bidhaa zitokazo China tuzikubali na kuzitumia hata kama zina madhara kama hayo?

Wachina hawa wametuletea bidhaa nyingi bandia, nyingine zina faida na nyingine zina hasara. Sielewi ni kwanini wamekuwa wakifumbiwa macho, labda kwa kuwa bidhaa zao zimepata watumiaji wengi.

Kwa mtazamo wangu, licha ya serikali kuwazuia wanachi, pia kuna haja ya sisi wenyewe kuhakikisha tunazikataa bidhaa zao, kwa kuwa wateja wakipungua hata wao watashindwa kuingiza bidhaa hizo.

Lakini hata TFDA haisaidii kuelezea madhara yake tu na kuingia madukani kuteketeza bidhaa hizo bandia, bali wanatakiwa pia kushirikiana zaidi na serikali na wizara husika ili kuangalia zinaingia kwa njia gani ili kuwepo na udhibiti mkubwa wa kuhakikisha haziingii nchini.

Ni jambo la busara kwa wizara husika kuhakikisha hawa Wachina hawaingizi dawa bandia hata mashine zao zinazoweza kuhatarisha maisha ya watu.

Lakini pia wasichana kwa wanawake wanatakiwa kujiuliza: “Wachina wao hawapendi makalio makubwa?” Ni kwa nini wasingetumia dawa hizo kwanza ndipo walete kwa Watanzania?

Ni kwa nini Watanzania wageuzwe wajinga kwa kutumia kila bidhaa itengenezwayo na Wachina hata kama ina matokeo mabaya kiafya?
Tuachane na tabia hiyo, Mungu ametuumba na ndivyo tunatakiwa kumkubali na kumshukuru pia kwa kila afanyalo.
Wanawake acheni kujibadilisha maumbile


 
Wanawake miili yao ndio mtaji,so wanajitahidi kuhiangaikia figa zao hili waendelee kula vichwa!
 
ushauri mzuri... lakini na wanaume wanaopenda kuongeza ukubwa wa nyeti zao ni vizuri nao waache...
 
Mimi napenda kuwaona wanawake wako fit, wana rekebisha fig zao:violin:
 
wanaume mkianza kuthamini natural appearences huenda ikasaidia
 
kila kitu kina soko lake, wanaopenda nachoro wapo, na wanaopenda feki wapo.

Dunia ya leo ni kuchanganya zako tu.
 
Back
Top Bottom