wanaume wenzangu someni mbadilike!

makaburini

Member
Dec 14, 2011
19
22
una mke na watoto pia una kazi nzuri kwa nini hutaki kuwatunza???? samaki samaki kila siku lazima upitie kula bata pale mkeo akiomba hela ya matumizi unagoma akili matope!wanaume kwa sasa tunaelekea pabaya!kuna uzi niliwahi kuuandika unaomuhusu member wa ofisi yetu aliyempa maneno ya kuudhi mkewe alipomuomba msaada kipindi cha shida ya mafuta mkasema sana kuwa huyo dada kwa nini anunue gari ashindwe kununua mafuta nikashangaa sana yaani mke wangu anajitunza mwenyewe na mimi nipo.... halafu bado nahesabika kama mume,hapana labda nivalishwe dera mimi!mke gari ajinunulie na mafuta ajiwekee sasa mimi kazi yangu ni usiku tu au??wanaume badilikeni acheni hizo tunzeni wake zenu au vipi the boss gonga like basi....mtambuzi....wapi chelenje umeadimika sana au uko na ile ID nyingine?
 
Siku hizi maisha tunasaidiana. Mwanamke akijigharamia na kujitunza sio mbaya.
 
chezea samaki samaki na denti za chuo wewe..

kiaina ni ukweli tu take care ila na wao mashosti wapunguze mitego maana ni soo daaaa....
 
.... halafu bado nahesabika kama mume,hapana labda nivalishwe dera mimi!mke gari ajinunulie na mafuta ajiwekee sasa mimi kazi yangu ni usiku tu au??wanaume badilikeni acheni hizo tunzeni wake zenu au vipi the boss gonga like basi....mtambuzi....wapi chelenje umeadimika sana au uko na ile ID nyingine?

Kwa wale wababa wenye uwezo wa kutunza familia zao wakati wake zao hawana uwezo huo, si jambo jema kutozitunza familia zao.
Ila kwa wale wenye familia ambapo baba na mama wana uwezo, na kwa ule mfumo wa haki sawa wa kuleeee beijing, mwanamke kujinunulia gari analolitumia mwenyewe kuna tatizo gani? Huu si ndiyo mfumo wa haki sawa? ni vibaya kusaidiana katika maisha?
 
kweli kabisa mkuu!wanaume akili zetu mbovu kabisa!hata kwenye mambo madogo madogo akili zetu ni madudu tuu!fikiria eti mwanaume anajiita MAKABURINI?sisi wanaume hovyo kabisa
 
aya basi wanawake wanaweza wakiwezeshwa HIVI NYIE WANAUME NA HAWA WATOTO WENU MNATAKA KUSAIDIWA KUWATUNZA NA MASHUGAMAMY NA MASHUGADAD AU? KILIO CHANGU NI KWA WALEE WASIOTUNZA WATOTO WAO MLIWALETA DUNIANI WA NINI KAMA SIO DHAMBI TU MNAJICHUMIA. UTAKUTA MTU MWANAE ANAUMWA HAJALI HATA KAKAMATIKA KWA KIMADA AMBAYE HATA KIZAZI LABDA HANAAAA
BADILIKENII
 
Wewe endelea kutunza familia yako na achana na UMBEYA na KUFUATILIA maisha ya Wanaume wenzio...!
 
mc tilly mimi ntamnunulia vitz mkeo sawa ehhhh halafu na wewe utapanda kaka usihofu.:high5:
 
wanaume wengi hatujui majukumu yetu ,wewe timiza ya kwako kama mkeo ataamua kukusaidia its ok lakini sio unakana majukumu yako mwanaume gani basi vaa gauni tu! hata biblia inatuambi hilo tusikatae
 
mc tilly mimi ntamnunulia vitz mkeo sawa ehhhh halafu na wewe utapanda kaka usihofu.:high5:

MAKABURINI!mbona umepanic mkuu?ok!lengo langu ilikuwa ni kukuonyesha wanaume TUNA mambo mengi ya ajabu!

umetoka povu mzee mpaka ukaanza kuzungumza mambo bahati mbaya sio tu hayahusiani hapa lakini usiyoyajua hata chembe!wanaoijua familia yangu they respect us!na kwa taarifa yako natumia real name!

pamoja na yote,unapotaka kumnunulia mke wa mtu gari huoni unaenda kinyume na post yako?
 
Kuna wanaume wabishi halafu wabahili. Hao hawabadilishiki hata waombewe.
 
makaburini umepotelea wapi tena!jibu swali nililokuuliza hapo juu!baadhi ya watu wanajifanya wapo clean sana huku wakijificha ktk fake id names!utawajua uhalisi wao ukiwabana kidogo tu wanaongea mambo kinyume na walivyotamka!umewakomalia wenzako kwenda samakisamaki halafu hapo hapo unataka umpeleke baba enock!we vipi wewe?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom