Wanaume wanapowabishieni, msiwashangae

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kwa nini wanaume ni wagumu sana kufanya mambo ambayo wake zao wanawaomba au kuwataka kufanya? Jibu, ni kwa sababu ni wanaume na wameona baba zao wakifanya hivyo na wakaiga. Lakini jibu linaweza kuwa lingine, kutegemea na ufahamu wa mtu na hata mazingira. Lakini ukweli unabaki kwamba wanaume sio wepesi wa kutenda yale ambayo wanatakiwa na wake zao kutenda.

Taarifa za kiutafiti zinaonesha kwamba, mwanaume ni mgumu kufanya anayotakiwa au kuombwa na mkewe kufanya kwa sababu nyuma ya ubongo wake, kuna kizuizi. Inadaiwa kwamba ubongo wa kina wa mwanaume kuna kitu kinachopingana na chochote ambacho mwanamke anamtaka kufanya.

Siyo suala la kurithi, hapana. Ukweli ni kwamba, kutokana na mwanaume kutokuwa tayari kuongozwa au kumsikiliza mwanamke na kumkubalia, hatimaye imejijenga akilini na kuwa kama vile ni suala la maumbile. Ukweli ni kwamba, miaka mingi ya kutoamini kwamba, mwanamke anaweza, imefanya kuwe na kizuizi hicho kwenye akili ya mwanaume.

Utafiti wa hivi karibuni kwa mfano, ambao uliongozwa na Gavan Fitzsimons profesa wa masoko na saikolojia, kwenye chuo kikuu cha Duke, anasema, kinachotokea ni juhudi za mwanaume kutotaka kuingiliwa kwenye mambo yake, bila mwenyewe kujua kwamba, anafanya juhudi hiyo. Jambo hili kisaikolojia linafahamika kama reactance, ambapo mtu hufanya kinyume kabisa na anavyotakiwa kufanya. Ni juhudi za mtu kupinga kupewa amri au kuingiliwa katika uhuru wake.

Wataalamu wanasema kwamba, wanaume hujikuta tu wamepinga jambo la mke bila kujua hata sababu. Ndio maana wanaume wengi huharibikiwa kwa kukataa kufanya yaliyopendekezwa na wake zao na baadae hujiuliza ni kwa nini walikataa.
Kwa hiyo wanaume wanapaswa sasa kujua kwamba, wanapombwa jambo na wake zao au kutakiwa kulifanya, wako kwenye hatari ya kulikataa. Kwa hali hiyo, wanapaswa kuwa waangalifu.
 
kweli kabisa wakati mwingine unakuta anabisha halafu unakaa kwa muda unajitia nimegundua hii kitu inafaa kumbe hana lolote..

kazi njema mtambuzi
 
Ndio maana tukaitwa wanaume, hata hivyo kwa asilimia nyingi wanayosema akina mama ni sahihi.
 
Mungu alimuumba mwanaume kwa sababu maalumu na kumleta mwanamke kumsaidia tu. Kwa kudanganywa kwake na nyoka, ikaleta dhahma duniani, hivyo mwanaume lazima uwe makini na kila unaloambiwa na mwanamke.
 
Hivi Mwl Nyerere (RIP) kwa nini alikemea kitendo cha Rais kushauriwa na mkewe? mnakumbuka hiyo hotuba?
 
mungu alimuumba mwanaume kwa sababu maalumu na kumleta mwanamke kumsaidia tu. Kwa kudanganywa kwake na nyoka, ikaleta dhahma duniani, hivyo mwanaume lazima uwe makini na kila unaloambiwa na mwanamke.
aimen!!!!!!mtumishi
 
Thanks God u have created me Mwanaume, mambo ya kuanza kubshiwabishiwa ningewezana nayo vipi.
 
Nachofahamu sisi kama wanaume huwa ni wagumu kushawishika kirahisi kama walivyo wanawake. Hoja inapokuja, sisi hulazimika kuifikiria kwa kina kabla ya kurush into conclusion kama baadhi ya wadada wanavyofanya. Ni suala la nature. Hata maandiko yanaonyesha kuwa Shetani alimdanganya mwanamke kwanza, kwa mwanaume yamkini ka usbishi kangekuwepo.
Kwa upande wa wanawake nao pia naona kama wana nature ya kufanya maamuzi ya haraka au pengine kudanganyika kirahisi kabisa pengine hata kwa vitu ambavyo ktk hali ya kawaida vinaonekana haviko sawa.

Unaweza kuprove haya zaidi kwenye mahusiano ya kimapenzi. Utakuta dada anapewa mimba na kijana, huyo kijana anakuja nyumbani kwa mwanamke anatukana matusi yote anayoyajuwa na kumkataa huyo mwanamke. Mwanamke anaapa kabisa kutokuwasiliana tena na huyo kaka. Baada ya miaka michache unakuja kusikia kijana huyo huyo kampa mimba nyingine tena dada yule yule! Ni kesi nyingi za namna hii nimewahi kuletewa. Ni mambo ya kushangaza.
 
Hilo ni kweli kabisa. Unaweza kumshauri mtu kitu akakataa, afu kesho yake anakuja na same solution kisa ameambiwa na rafiki yake kuwa ina work. Lol. Mi nshawajua, nawa enjoy tu. aaah. Utanibishia lakini mwisho wa siku utakubali kuwa na mimi kichwa.
 
Tatizo la huu utafiti umeshindwa kuweka wazi kuwa wanaume na wanawake ni viumbe tofauti sana hasa jinsi wanavyofikiri, kufanya maamuzi na kutenda kazi. Hizi tofauti ni muhimu ziwepo ili hawa viumbe waweze kuishi pamoja kama mme na mke. Ukiziondoa hizi tofauti unaishia kuwa na wanaume wanaofikiri kama wanawake mpaka wanaona ni sawa tu kuolewa kama wanavyoolewa wanawake. Wazungu ambao ndio chanzo cha huo utafiti wako ndipo walipofika. Sio ajabu sasa wameweka ushoga kama moja ya masharti ya mikopo yao.
 
Hilo ni kweli kabisa. Unaweza kumshauri mtu kitu akakataa, afu kesho yake anakuja na same solution kisa ameambiwa na rafiki yake kuwa ina work. Lol. Mi nshawajua, nawa enjoy tu. aaah. Utanibishia lakini mwisho wa siku utakubali kuwa na mimi kichwa.

kweli kabisa wako ivo
 
Back
Top Bottom