Wanaume wanaonyemelea wanafunzi wamchukiza Waziri

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Wanaume wanaonyemelea wanafunzi wamchukiza WaziriNa Stella Mwaikusa

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza amesema anachukizwa na baadhi ya wanaume wanaowarubuni wanafunzi wa kike kufanya mapenzi na hatimaye kusababisha mimba na akasema kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Mahiza alisema wanaume wanaofanya vitendo hivyo wanakwamisha maendeleo ya mtoto wa kike.

"Hivi kweli wanaume watu wazima hawana namna nyingine ya kwenda kujikimu shida zao mpaka wakajikimu kwa wanafunzi?" aliuliza na kuongeza:

"Hivi hawa watoto wa kike wakiendelea kutoka kwa maelfu katika shule , tuna matarajio gani, tunataka kujenga Taifa gani na huu ni uonevu wa aina gani, naomba suala hili lisichukuliwe kimasihara," alisisitiza.

Alisema kitendo cha watoto wa kike kupata mimba ni hatari kwao kwani hapo si kwamba atakuwa ameshindwa kufikia malengo yake ya kupata elimu bali anaweza akawa ameambukizwa na virusi vya ukimwi kitu ambacho ni hatari zaidi.

Pia aliongeza kuwa watoto wa kike waliokatishwa masomo yao kwa kupata mimba wakiwa shuleni, wamekuwa wakipoteza muda wao kuwalea watoto huku wanaume waliohusika wakiendelea na masomo yao na baadaye kuoa wanawake wengine.

Kauli ya Waziri inatolewa wakati wanafunzi 1,026,806 walianza jana kufanya mtihani wao wa kumaliza elimu ya msingi ambapo wanatarajia kumaliza leo huku kukiwa na mapungufu ya asilimia 1.9 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kuhusu walimu wanaokimbia maeneo yao waliyopangiwa Mahiza amewaomba wawe wazalendo kwa kufanya kazi katika maeneo hayo kwani Tanzania ni ya kila mtu.

"Tanzania ni yetu sote, mazingira na jiografia ya nchi ndiyo urithi wetu hivyo nawaomba walimu msikimbie vituo vyenu vya kazi kwani watu tulio wengi hatujazaliwa mijini," alisema.
Hivi karibuni zimeripotiwa taarifa za walimu kukimbia maeneo waliyopangiwa hususan Shinyanga, Sindiga na Rukwa ambao zaidi ya 50 walitoroka.

Imetoka Mwananchi Gazeti
 
Wanaume wanaonyemelea wanafunzi wamchukiza WaziriNa Stella Mwaikusa

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza amesema anachukizwa na baadhi ya wanaume wanaowarubuni wanafunzi wa kike kufanya mapenzi na hatimaye kusababisha mimba na akasema kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Mahiza alisema wanaume wanaofanya vitendo hivyo wanakwamisha maendeleo ya mtoto wa kike.

“Hivi kweli wanaume watu wazima hawana namna nyingine ya kwenda kujikimu shida zao mpaka wakajikimu kwa wanafunzi?" aliuliza na kuongeza:

“Hivi hawa watoto wa kike wakiendelea kutoka kwa maelfu katika shule , tuna matarajio gani, tunataka kujenga Taifa gani na huu ni uonevu wa aina gani, naomba suala hili lisichukuliwe kimasihara,” alisisitiza.

Alisema kitendo cha watoto wa kike kupata mimba ni hatari kwao kwani hapo si kwamba atakuwa ameshindwa kufikia malengo yake ya kupata elimu bali anaweza akawa ameambukizwa na virusi vya ukimwi kitu ambacho ni hatari zaidi.

Pia aliongeza kuwa watoto wa kike waliokatishwa masomo yao kwa kupata mimba wakiwa shuleni, wamekuwa wakipoteza muda wao kuwalea watoto huku wanaume waliohusika wakiendelea na masomo yao na baadaye kuoa wanawake wengine.

Kauli ya Waziri inatolewa wakati wanafunzi 1,026,806 walianza jana kufanya mtihani wao wa kumaliza elimu ya msingi ambapo wanatarajia kumaliza leo huku kukiwa na mapungufu ya asilimia 1.9 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kuhusu walimu wanaokimbia maeneo yao waliyopangiwa Mahiza amewaomba wawe wazalendo kwa kufanya kazi katika maeneo hayo kwani Tanzania ni ya kila mtu.

“Tanzania ni yetu sote, mazingira na jiografia ya nchi ndiyo urithi wetu hivyo nawaomba walimu msikimbie vituo vyenu vya kazi kwani watu tulio wengi hatujazaliwa mijini,” alisema.
Hivi karibuni zimeripotiwa taarifa za walimu kukimbia maeneo waliyopangiwa hususan Shinyanga, Sindiga na Rukwa ambao zaidi ya 50 walitoroka.

Imetoka Mwananchi Gazeti

Hilo tatizo halikuanza leo na imani hata wakati wake akiwa mwanafunzi Bi Mwantumu Mahiza inawezekana amekumbana nayo au anawaelewa wanafunzi waliokumbana na hali hiyo, la muhimu hapa ni kuwaelimishwa hao wanafunzi njia za kujiepusha na hizo mimba aupia hao kina baba (babu )watumie mipira kama alivyowaeleza Aliye Kuwa Rais wa Tanzania Mzee Ali Hassan mwinyi ,jamii tayari imeshapotoka na sasa tunaelekea katika kuangamia na machafu siku hadi siku.
 
Kupunguza hili tatizo, wote wawili (anayegawa mimba na anayepokea mimba) wachukuliwe hatua zinazo lingana. Hii itasaidia wanafunzi kujilinda zaida. Sheria imwache tu pale ambapo itabainika kuwa hakukubaliana kufanya hicho kitendo bali alilazimishwa.
 
Back
Top Bottom