Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Mshiiri

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
2,012
507
Ni muda mrefu nimekuwa nafanya utafiti katika hii kanda ya mapenzi na kugundua kuwa wanaume wengi hufa kabla ya wake zao hata kama wamezaliwa mwaka mmoja na kubaini kuwa tabia za wake zao huwafadhaisha na kuwafanya waishi maisha magumu sana na kupata yale maradhi ya kufisha kama HYPERTENSION, SAIKOSISI, STROKE N.K

Madhanio wakati wa utafiti ni kuwa je wanaume wasio katika ndoa je wanashambuliwa sana na magonjwa haya ya kufisha kama cohort wao walio katika ndoa? Hatimaye ikabainika kuwa wasio katika ndoa ni wachache sana karibu na hamna ila walio kwenye ndoa ni wote, kama sio aina moja ni nyingine. Hitimisho likawa wanawake huchangia vifo vya mapema vya wanaume katika ndoa.

Je, ni kwanini? Hii ni sehemu nyingine wazi ya utafiti.

Je. kuna aliyefanya utafiti binafsi kuhusu hili na nini hatima yake?

Nawasilisha!

=========
Chris Mauki anasemaje?
(Kwanini wajane ni wengi kuliko wagane??)

Mtalaamu saikolojia na mahusiano Dk. Chris Mauki anatoa sababu zifuatazo:

1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha ' life expectancy':
Kama unafahamu hili jambo linaloitwa 'life expectancy'; utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao.


2. Ugumu katika kufunguka:
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza. Na kwa mtaji huu watakufa sana tu

3. Ugumu katika kusamehe:
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote. Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sna kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

4. Tabia hatarishi:
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

5. Ugumu katika kujali afya:
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo. Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

6. Msongo wa mawazo:
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo 'stress' ingawa kwa nje wanajitahisi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.


Maisha sio mabaya kiasi hicho, maisha ni mazuri. Chagua kuishi

Chriss Mauki


Pamoja na kwamba wanawake ndiyo wamekuwa wakielemewa na majukumu mengi na mazito kimaisha, lakini ni hao hao ambao wamethibitika kuishi kwa muda mrefu kuliko wanaume.

Kulingana na jarida la Human Nature la huko nchini Marekani ni kwamba tofauti hiyo ya umri wa kuishi kati ya wanaume na wanawake haikuanza jana wala juzi bali ni ya siku nyingi sawa sawa na historia ya binadamu mwenyewe.

Kwa hiyo ni suala la maumbile. Katika utafiti uliowahi kufanywa ulibaini kwamba tabia iliyopindukia mipaka ya kujihatarisha na kukandamiza mihemko ya kihisia kwa upande wa vijana wa kiume, inahusiana moja kwa moja na vifo vya mapema vya wanaume vijana na hata kupunguza umri wao wa kuishi ukilinganisha na wanawake.

Tabia nyingine ambazo pia zinawaweka wanaume kwenye hatari ya kufa mapema ni pamoja na uvutaji sugu wa sigara, ulevi, uendeshaji mbaya wa magari na vurugu nyingine.

Wanaume wengi wana maradhi ya kihisia kuliko wanawake, pamoja na kwamba inaonekana wanawake hukabiliwa sana na sononi za kimaisha.

Hebu chunguzeni kisha mniambie, ni akina nani wenye Kisukari, shinikizo la juu la damu, matatizo ya moyo, matatizo ya kiakili na mengine yanayofanana na hayo, kati ya wanaume na wanawake?

Kama mkifanya utafiti wenu kwa makini mtabaini kwamba ni wanaume.

Hebu niwaulize, hivi ni akina nani wanaokufa kwa kutafuta fedha au umaarufu kati ya wanaume na wanwake?

Jibu liko wazi. Ukisikia mwanamke ni jambazi utashngaa, ukisikia mwanamke ni tapeli, lazima utashangaa, ukisikia mwanamke mdhulumu mirathi, pia utashangaa. Kitakahokushangaza ni ugeni wa wanawake kwenye aina hiyo ya maisha.

Wanaume wengi wanaingia kwenye shughuli au tabia hizo hufanya hivyo kwa sababu wanataka kuthibitisha kwamba, wanaweza, wamefanikiwa na kuonesha tofauti yao na wanawake ambao hawajaweza. Wanataka kuwaonesha wanawake kwamba wamemudu.

Mwanaume huwa na umri mfupi kuliko mwanamke kwa sababu anataka kuwa mkuu, anataka kushinda na anataka kuonesha jamii kwamba, anastahili kuliko wengine.

Anaposhindwa kuonesha ndipo pale anapoingia kwenye tabia mbaya zaidi kama ulevi wa pombe, uvutaji bangi,utumiaji dawa za kulevya, na kupata sononeko na kusongeka kiakili. Yote haya yana madhara makubwa kwa afya na usalama wake. Yote haya yanamfupishia maisha yake. Anakuwa amechagua kuishi kwa muda mfupi kwa hiyari yake.
 
Sina uhakika kama hii ina ukweli.

Mawazo yangu ni kuwa, zamani labda hata sasa hivi wanaume ndio walikuwa wanafanya kazi na wamama wanakaa ndani tu.

Sasa unajua tena mitulinga ya kazini inavyodhoofisha miili ..na hii inajionyesha sana wakati wa uzeeni..na yawezakana ikachangia wanaume kuzeeka na kufariki mapema kuliko wanawake
 
...hayo ni maajabu ya nature,....kwani hayaishii kwa binaadamu peke yake. Chunguza hata mifugo na wanyama wa majumbani....

Paka/mbwa/ng'ombe/mbuzi/jogoo dume wataishi muda mrefu lakini jike ndilo litalo survive longest.

Kwenye maisha ya ndoa vile vile, mara nyingi wanaume ndio hufariki kwanza, labda kwa kuwa wanaume wengi huoa wanawake walio na umri mdogo kwao. Vile vile ikumbukwe miili ya kina mama ina ziada ya hormones kukabiliana na misukosuko ya ubebaji mimba hivyo kuwafanya wawe na bonus ya umri zaidi tofauti na 'wasaga lami'.

Maoni yangu tu...
 
Umesema walio ktk ndoa ni wachache. Je life span yao ikoje kwa kuwa hawana watu wa kuwapa pressure? Ama utafiti wako umeishia kwa waliooa tu. Tujuze kama nikutoa talaka tutoe ili tuweze kuishi siku zinazostahili.
 
Nina mashaka na utafiti wako, katika utafiti wangu wa kupitia makala mbalimbali ukweli ni kwamba wanaume tulio wengi tunajiusisha na maisha hatarishi kama kunya pombe kupindukia, uvutaji wa sigara, kula chakula kingi kuliko mahitaji halisi ya mwili na majukumu mengi ya ziada zikiwemo nyumba ndogo ambazo zinatupa misongo(stress) mingi katika maisha.

Lakini pia wanaume wengi hasa wa kiafrika tunapenda kujiona tuko ngangari matatizo madogomadogo ya mwili tunavumilia, lakini wanaweka wengi wanakimbilia hospitali kujua tatizo ni nini sababu hawavumilii matatizo ambayo yanaonekana ni madogo hivyo wanajikinga na magonjwa mengi.

Matokeo yake wanawake wanaishi miaka mitano na zaidi kuliko wanaume.
 
ni kweli kabisa , wanawake ukaa mda mrefu sabau wanajali san afya zao ila sisi madume twajifanya tumeumbwa kwa mateso , na ujuwaji mwingi sana kwenye maisha , kama vile kutowashirikisha wake zetu kutokana na matatizo yetu tunayoyapata either kazini or mtaani ndio maana tunakuwa na majukumu yanayoshinda uwezo wetu wa kufikili.
 
Sina uhakika na utafiti wako ila ninachoweza kuchangia ni kuwa waname wengi hufa haraka zaidi iwapo wake zao ndio watakao anza kufariki kuliko wanawake wanaofiwa na waume zao. Ni kwanini? sijui labda tuwaachie wataalam wa sosholojia watusaidie kutafuta uhalisia wa haya mambo.
 
Utafiti wako unafanana na ukweli kabisa.

Hali hiyo ipo kila mahala!

Hata mimi naamini kwamba presha za mwanaume za kuendesha maisha ya familia zinamcost calories nyingi sana kiasi ana`wear-out` haraka sana, hatimaye anajisababishia sumu mwilini na kuwahi kunako haki!.
 
One important reason is the big delay “and advantage” women have over men in terms of cardiovascular disease, like heart attack and stroke. Women develop these problems usually in their 70s and 80s, about 10 years later than men, who develop them in their 50s and 60s. For a long time, doctors thought the difference was due to estrogen. But studies have shown that this may not be the case, and now we know that giving estrogen to women post-menopause can actually be bad for them.

One reason for that delay in onset of cardiovascular disease could be that women are relatively iron-deficient compared to men “especially younger women, those in their late teens and early 20s” because of menstruation. Iron plays a very important part in the reactions in our cells that produce damaging free radicals, which glom onto cell membranes and DNA, and may translate into aging the cell. In fact, in our diets, red meat is the main source of iron, and lack of iron is probably one major reason that being vegetarian is healthy for you. There was a very good study looking at the intake of red meat and heart disease in Leiden in the Netherlands: in regions where people didn't eat red meat, those populations had half the rate of heart attack and stroke compared to the populations that did eat red meat.

Another more complicated possibility [for women's longevity] is that women have two X chromosomes, while men have one. (Men have an X and a Y.) When cells go through aging and damage, they have a choice in terms of genes “either on one X chromosome or the other. Consider it this way: you have a population of cells, all aging together. In some cells, the genes on one X chromosome are active; in other cells, by chance, the same set of genes, with different variations, are active on the other X chromosome. Don't forget, we all have the same genes” the reason we differ is because we express different variations of those genes, like different colors of a car. Now, if one set of variations provides a survival advantage for the cells versus another, then the cells with the advantage will persist while the other ones will die off, leaving behind more cells with the genes on the more advantageous X chromosome. So, in women, cells can perhaps be protected by a slightly better variation of a gene on the second X chromosome. Men don't have this luxury and don't get this choice.

It's very unclear [how big an effect that could have]. I've seen men who have done horrendous damage to themselves over time with smoking and drinking and who still get to 100 and older though that's very, very rare. They might have the right combination of some really special genetic variations that we call "longevity enabling genes” which we're on the mad hunt for. Meanwhile other individuals may do everything right and only make it into their 80s. That may be because they have what we call "disease genes," some genetic variations that are relatively bad for them. Now some of these [disease genes] may be on the X chromosome, [meaning that women who have the second X chromosome with which to compensate, would have an advantage]. But it's really still a very complicated puzzle to tease out.

[There are a few other reasons that men die earlier in life more often than women.] Men in their late teens and 20s go through something called "testosterone storm." The levels of the hormone can be quite high and changeable, and that can induce some pretty dangerous behavior among young men. They don't wear their seatbelts; they drink too much alcohol; they can be aggressive with weapons and so on and so forth. These behaviors lead to a higher death rate.

Another area where we see higher death rates among men is among the depressed “especially older men. If they attempt suicide, they are more likely to succeed than women.

Overall, about 70% of the variation around average life expectancy [just over 80 for women and just over 75 for men in the U.S.] is probably attributable to environmental factors your behaviors and your exposures. Probably only 30% is due to genetics. And that's very, very good news. There's so much we can do. Most of us should be able to get into our late 80s. What's more, to get to older ages, like the centenarians, you are necessarily compressing the time you're sick to the end of your life. It's not a case where the older you get, the sicker you get. It's very much the case that the older you get, the healthier you've been.

But, in general, there are maybe three things men do worse than women. They smoke a lot more. (That gender gap is fortunately shrinking, since men are smoking less and less.) They eat more food that leads to high cholesterol. And, perhaps related to that, men tend not to deal with their stress as well as women. They may be more prone to internalizing that stress rather than letting go though that's a fairly controversial point. Nonetheless, stress plays a very important role in cardiovascular disease.

Source: Breaking News, Analysis, Politics, Blogs, News Photos, Video, Tech Reviews - TIME.com
 
Sina uhakika kama hii ina ukweli.

Mawazo yangu ni kuwa, zamani labda hata sasa hivi wanaume ndio walikuwa wanafanya kazi na wamama wanakaa ndani tu. Sasa unajua tena mitulinga ya kazini inavyodhoofisha miili ..na hii inajionyesha sana wakati wa uzeeni..na yawezakana ikachangia wanaume kuzeeka na kufariki mapema kuliko wanawake


Hizi ni baadhi ya sababu ndugu.....

...hayo ni maajabu ya nature,....kwani hayaishii kwa binaadamu peke yake. Chunguza hata mifugo na wanyama wa majumbani....

Paka/mbwa/ng'ombe/mbuzi/jogoo dume wataishi muda mrefu lakini jike ndilo litalo survive longest.

Kwenye maisha ya ndoa vile vile, mara nyingi wanaume ndio hufariki kwanza, labda kwa kuwa wanaume wengi huoa wanawake walio na umri mdogo kwao. Vile vile ikumbukwe miili ya kina mama ina ziada ya hormones kukabiliana na misukosuko ya ubebaji mimba hivyo kuwafanya wawe na bonus ya umri zaidi tofauti na 'wasaga lami'.

Maoni yangu tu...

another possible cause

Nina mashaka na utafiti wako, katika utafiti wangu wa kupitia makala mbalimbali ukweli ni kwamba wanaume tulio wengi tunajiusisha na maisha hatarishi kama kunya pombe kupindukia, uvutaji wa sigara, kula chakula kingi kuliko mahitaji halisi ya mwili na majukumu mengi ya ziada zikiwemo nyumba ndogo ambazo zinatupa misongo(stress) mingi katika maisha. Lakini pia wanaume wengi hasa wa kiafrika tunapenda kujiona tuko ngangari matatizo madogomadogo ya mwili tunavumilia, lakini wanaweka wengi wanakimbilia hospitali kujua tatizo ni nini sababu hawavumilii matatizo ambayo yanaonekana ni madogo hivyo wanajikinga na magonjwa mengi. Matokeo yake
kweli kabisa.... wanaume wanachukua risks zaidi na kuhatarisha maisha... tabia nyingine kama hizo ulizotaja pamoja na misukumo kutoka jamii kama vile kutokutakana kuonekana mayai - hawatafuti tiba kwa magonjwa..vyote hivi kuchangia kufupisha maisha..


ni kweli kabisa , wanawake ukaa mda mrefu sabau wanajali san afya zao ila sisi madume twajifanya tumeumbwa kwa mateso , na ujuwaji mwingi sana kwenye maisha , kama vile kutowashirikisha wake zetu kutokana na matatizo yetu tunayoyapata either kazini or mtaani ndio maana tunakuwa na majukumu yanayoshinda uwezo wetu wa kufikili.

Kabisa.... wanaume hujiua polepole kwa kutokupenda kuomba msaada hata wa mawazo


hii kali.... unanikumbusha nyuki..dume inabidi life baada ya kutoa na ndivyo walivyoumbwa,,,, sijui kama kuna option ya kukataa!?


Ila tutake tusitake...wanaume mmeumbwa katika hali ya kutoishi miaka mingi kama wanawake pamoja na kuwa wanawake wanapitia magumu na pia huvumilia mengi ikiwa ni pamoja na manyanyaso ya wanaume.Ingekuwa kufa kwa manyanyaso kama mtoa mada anavyotaka kudai... basi wanawake na hasa wa vijijini wangeisha!
 
Zaidi ni pale unaposikia kuwa mkeo anamegwa na rafiki yako au jamaa flani!
Ndo pale wengi wanakufa na maumivu yao.
 
sijafanya utafiti wowote siriaz..lakini najaribu kuangalia mazingira nitokayo pale kijijini..idadi ya wajane wanaotuzunguka akiwemo mama yangu mzazi..inatisha!!wamebaki kina mama/bibi peke yao kule nyumbani........tumaini lao lipo kwa watoto wao na kama mungu amewajaalia vijukuu mapema basi ikiwapendeza wamuache pale nyumbani akae na bibi/mama...

hivi wenzangu huko mtokako mmeshaliona hilo?...wanaume wamekuwa wakiripotiwa either kufa mapema zaidi au kufa mapema tu kwa sababu kadha wa kadha..........wanaume mnalizungumziaje hili suala...tumejiandaaje..au tunajiwekea mazingira gani ya kupunguza idadi ya wajane n ayatima hasa ukizingatia wanaume ndio vichwa vya familia...................eeh Mungu tunusuru!!

ebu tujaribu kuliangali ahili.............
 
Back
Top Bottom