Wanaume wa Tanzania na romance

Ashangedere

Senior Member
Aug 9, 2010
119
31
asalaam aleykum wanajamvi, kuna jambo huwa linanitatiza saaana kuhusu ndoa nyingi (si zote) za kitanzania.
Hivi kuenda na mke wako kwenye sherehe na kukaa nae ni kinyume cha maadili yetu???
Kumshika mke wako mkono mbele ya watu hata kama watoto wapo ni kinyume cha maadili yetu??? au ni kuwafundisha watoto wawapende na kuwathamini wenzi wao pindi wa kiwa wakubwa???
Kumuweka mke wako mbele kuliko marafiki na ndugu mfano: Rafiki anakuambia muende somewhere kuhave fun ukimwambia uko busy na wife ni kinyume na maadili?? kuna jambo lingine linanishangaza saaaaana, siku ya harusi tunashikana mikono kanisani, tunakula keki moja tena twalishana na mdomo, tunadance ziro distance mbele ya umati lakini baada ya hapo yote yanakuwa KINYUME NA MAADILI, hapo kanisani kila mtu anakaa upande wake, kushikana mikono kushney,kwenye sherehe kama hamjuani no kudence no romance, no what, naombeni wanaume hapa jamvini mniambie why this is happening.... Je mnajua howmuch your wives wanapenda romance??? I can assure you women love romance more than anything else, we love displaying affection kwenye public japo kwa mipaka. Plz wanaume naombeni views zenu on this.
 
mie sisubirigi afanye, nikijickia kufanya nafanya vyovyote vile ninavyojickia bila kuvunja sheria, c wangu bwana bac nipo nae free na anatakiwa nae ajibu mapigo kama hataki kec....na kweli kwenye wedding mabusu kibao ngoja leo mpo kwenye cjui party ya ofc, yupo busy na colleagues, hapo hapo na mie ndio nabana.
 
tatizo wanaume wa kitanzania eti ukiwa bize na wife washkaji wanakwambia mwanamke anakuendesha,anyway mi kama nataka unibebe unikumbatie unikiss anywhere u must do,thats the meaning of love,love has no limitation ch muhimu ni kuangalia tu mpo katika situation gani
 
mie sisubirigi afanye,
Safi kumbe wewe sio tegemezi
nikijickia kufanya nafanya vyovyote vile ninavyojickia bila kuvunja sheria
Nataka nijue vyovyote vile ndio inakuwaje nataka nione mfano halisi
,
c wangu bwana bac nipo nae free na anatakiwa nae ajibu mapigo kama hataki kec
Nafikiri huyo mwenza kwenye chama yupo ngoja nifuatilie kadi yake ni namba ngapi
...
.na kweli kwenye wedding mabusu kibao ngoja leo mpo kwenye cjui party ya ofc
Hizi shughuli ni zuri sana uwe una mruhusu mara kwa mara kwenda kwenye hizi hafla
,
yupo busy na colleagues, hapo hapo na mie ndio nabana.
Nafikiri ninavyofikiria hapa sijakosea
 
Jamani,
wanawake wananiboa,
wanataka kila kitu aanze mwanaume kufanya.
Utafikiri wao ni vipofu, viziwi, viwete, na wana ulemavu wa namna zote

sema baadhi...wengine tukijickia/ hamu ya kufanya hiki au kile, tunafanya!
 
Jamani,
wanawake wananiboa,
wanataka kila kitu aanze mwanaume kufanya.
Utafikiri wao ni vipofu, viziwi, viwete, na wana ulemavu wa namna zote

baadhi ya wanawake wanaogopa kushushuliwa kwani unakuta walishajaribu sikumoja wakashushuliwa so wanakuwa wanyonge japo wanapenda na wanaogopa kuanzisha
 
tatizo wanaume wa kitanzania eti ukiwa bize na wife washkaji wanakwambia mwanamke anakuendesha,anyway mi kama nataka unibebe unikumbatie unikiss anywhere u must do,thats the meaning of love,love has no limitation ch muhimu ni kuangalia tu mpo katika situation gani

tatizo mnapenda sana show game, wakati sisi tupo very realistic kwa mambo mengi tu!
 
baadhi ya wanawake wanaogopa kushushuliwa kwani unakuta walishajaribu sikumoja wakashushuliwa so wanakuwa wanyonge japo wanapenda na wanaogopa kuanzisha

Ukiona hivyo ujue hakupendi ulilazimisha kuolewa. Wanawake wengi wa tz wanatabia ya kulazimisha ndoa na mtu anaweza hata kubeba mimba ili mradi aolewe so kwa kufanya hivyo unakuwa umelazimisha ndoa na ndio maana mambo kama hayo yanatokea. Kama mtu alikuoa akiwa amedhamiria na sio kulazimishwa hawezi kukushushua matokeo yake atafurahia. Na sio hilo tu hata infidelity haiishi kwa sababu ya mambo kama hayo ya kulazimisha ndoa.
 
hivi vitu ni tamaduni tu unajua tofauti yetu na wazungu ni kwamba wazungu wanaonyesha mapenzi kwa vitendo kabisa kama mtu kafurahi anaonyesha kwa vitendo ila sisi waafrika tuko tofauti kutokana na tamaduni zetu utakuta mtu anampenda sana mwenzi wake lakini kuonyesha wazi anaogopa kutokana na tamaduni zetu hata kwenye harusi utakuta MC ndio anawaongoza au padre na sheikh kuwa unaweza kufunua shela na kumbusu au mchum mchum mwaaa baada ya hapo inachobaki ni wivu tu na kuulizana mbona umechelewa ulipitia wapi au mbona nimekutumia msg hujajibu yaani mapenzi yetu yanaonekana kwa wivu wivu tu na si kwa vitendo

na siku ukijifanya kubusu busu kwenye sherehe za kikazi au harusi (zakualikwa) mkitoka hapo kama sio gazeti la udaku kuwatoa front page basi ujue ndio itakuwa discussion kwa waalikwa wote

mapenzi ya kiafrika na kibongo yana miundo mbinu yake tofauti na sinema na movie za Marichuy, tunayaweza wenyewe
 
vunja ukimya ....

siku ukijiskia unataka maua ......mpigie simu umwambie leo usirudi home mpaka uje na maua! yanini kujikera kwa kutaka mwanamme afahamu ile inaitwa 'ilmu lghayb' (elimu iliyojificha) ya kusoma mawazo yako?
 
Hii sredi nimeipenda, mi siku moja nimeenda kwenye arusi nakutana na mshkaji yuko na waif wake hadi arusi inaisha hawajaongea, kama vile haitoshi ilipofika muda wa msosi waifu akazuga kwenda msalani, aliporudi akaunga foleni nyuma ya hubby wake kama mtu wa tatu, sikuipenda kabisa ile. Kama vipi si wangeacha kuja tu. Ila jamaa alikuwa anautafuta ukaribubila mafanikio.
 
ukiona hivyo ujue hiyo ndoa ni kongwe ina miaka zaidi ya mitano, ndoa kongwe zina visa sasa si bora hao walikaa pamoja kuna nyingine unasikia mtambulishaji anasema baba mdogo na mkewe popote mlipo tunaomba msimame unakuta baba mdogo anasimama mbele ya ukumbi na mkewe anasimama upande wa pili kabisa
 
haki ya nani Funzadume wewe hamnazo, nimecheka sana, ndoa zina mambo jamani, sasa walilazimishwa kwenda huko, ingekuwa mi ni bora nisiende kabisa.
 
asalaam aleykum wanajamvi, kuna jambo huwa linanitatiza saaana kuhusu ndoa nyingi (si zote) za kitanzania.
Hivi kuenda na mke wako kwenye sherehe na kukaa nae ni kinyume cha maadili yetu???
Baadhi ya wanawake na wanaume wengine wagumu kama mihogo
Kumshika mke wako mkono mbele ya watu hata kama watoto wapo ni kinyume cha maadili yetu??? au ni kuwafundisha watoto wawapende na kuwathamini wenzi wao pindi wa kiwa wakubwa???
Wengine wamerithi kuna rafiki yangu aliniambia tokea amewafahamu wazazi wake hajawahi kuona hata siku moja wameshikana mikono kila mtu kivyake
Kumuweka mke wako mbele kuliko marafiki na ndugu mfano: Rafiki anakuambia muende somewhere kuhave fun ukimwambia uko busy na wife ni kinyume na maadili??
Wengi ukifanya hivyo utaambiwa umelogwa au umetupiwa kitu na mwanamke
kuna jambo lingine linanishangaza saaaaana, siku ya harusi tunashikana mikono kanisani, tunakula keki moja tena twalishana na mdomo, tunadance ziro distance mbele ya umati lakini baada ya hapo yote yanakuwa KINYUME NA MAADILI, hapo kanisani kila mtu anakaa upande wake, kushikana mikono kushney,kwenye sherehe kama hamjuani no kudence no romance, no what, naombeni wanaume hapa jamvini mniambie why this is happening....
Ukiona hivyo ujue mapenzi au ndoa tayari imeishachakachuliwa na small house inafanya kazi kwa niaba yako
Je mnajua howmuch your wives wanapenda romance???
Tunajua lakini it BEGINS WITH YOU vile vile
I can assure you women love romance more than anything else, we love displaying affection kwenye public japo kwa mipaka. Plz wanaume naombeni views zenu on this
.
Let it be that way and it shouldn't change
 
Ila kiukweli jamani kushikana mikono kwenye harusi au mkusanyiko wa watu ni ujasiri, unless ni katika vipindi vya kutegana (initial stages za uhusiano). Nazionaga sana chuoni kwa wenzangu wa UDSM wanakumbuka njia flani ya Yombo kuelekea Hall 4 na Hall 3 ndio mambo hayo kwa sana. Malizeni chuo afu mkutane kwenye harusi au matukio mengine na wahusika, kwa bahati wawe walioana, unakuta kimyakimya kama sio wao. Izi mambo ni noma.
 
Halafu sijui kwanini mwingine ukimshika mkono anasema anaona aibu anakwambia sipendi tushikane mikono mbele za watu, halafu baadae huyo huyo anaanza kusema ohooo sijui u dont show me love and affectionate
 
Ukiona hivyo ujue hakupendi ulilazimisha kuolewa. Wanawake wengi wa tz wanatabia ya kulazimisha ndoa na mtu anaweza hata kubeba mimba ili mradi aolewe so kwa kufanya hivyo unakuwa umelazimisha ndoa na ndio maana mambo kama hayo yanatokea. Kama mtu alikuoa akiwa amedhamiria na sio kulazimishwa hawezi kukushushua matokeo yake atafurahia. Na sio hilo tu hata infidelity haiishi kwa sababu ya mambo kama hayo ya kulazimisha ndoa.

Usiseme hivyo kuna wanaume wanasema ukimtaka mwanamke unamfanyia chochote lakini ukishamuweka ndani ndio baasi. hapo utakuta mama ulibembelezwa ile mbaya kuolewa uliobwa na kufanyiwa yoote, lakini sasa ukimwambia nataka uwe romantic anakuambia kwani wewe si wangu tu kwani lazima nikufanyie hivi na vile?? kwanza tumeshaoana kwani unataka nini tena?? wala sio kwamba mtu alilazimisha ndoa, lakini hata hiyo mnayosema ya kulazimisha ndoa mi hainiingii akilini mwanamke hawezi kukurupuka na kukulazimisha lazima muwe na mahusiano na mahusiano mwisho wake ni ndoa sijui kama kuna mwanamke alilazimisha kuolewa na mwanaume asie na uhusiano nae!! aonjae asali sharti achonge mzinga!!!
 
haki ya nani Funzadume wewe hamnazo, nimecheka sana, ndoa zina mambo jamani, sasa walilazimishwa kwenda huko, ingekuwa mi ni bora nisiende kabisa.
Utakuta ndoa ni ya mtu wa karibu na mnatakiwa wote muwepo. Nyumba hizi zinaficha mengi sana kuna jamaa niliwahi kuwaona wametoana out wenyewe pale Girrafe Hotel sijui walikuja kusuluisha ugomvi basi walikaa pale hawakuongea mwanzo mwisho na baada ya m/mke kumaliza chakula akamwambia jamaa maliza haraka tuondoke jamaa akamwambia usini-force kula haraka kilichofuata yule dada akabeba funguo za gari akanyanyuka akamwambia utanikuta kwenye gari. Yule m/ume alikasirika halafu watu kibao waliona ile movie ilivyoenda baadae akaagiza mzinga wa konyagi kubwa akaunywa kama juice ulivyoisha akatoka kumfuata mwenza wake kwenye gari
 
Back
Top Bottom