Wanaume wa sasa hawana tofauti na Wanawake

Ndokeji

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
698
475
Siku moja nikiwa na safiri kuelekea Dar esalam kutoka mbeya nikiwa kwenye kituo cha mabasi, kulikuwa na wazee wawili, walikuwa na maada ambayo walinifanya niwadadisi kwa undani zaidi ,wakidai kuwa vijana wa kiume wasasa hawana tofauti na mwanamke isipokuwa maumbile tu ndiyo yanawatenganisha mengine yote nisawa ,walitaja sababu 1. Vijana hawana ujasili. Wanaogopa kumukabili mwanamke 2. Kwenye ndoa mwanamke amekuwa na amri sawa na mwanaume 3. Waoga hata kumtokea mwanamke 4.wakikutanisha macho na mwanamke huwa wakwanza kuinamishwa kichwa chini 5. Akimtongoza mwanamke yeye ndiye wakuuma uma nyasi na kushika ukuta 6. Walio kwenye ndoa humpikia mwanamke wakidai haki sawa 7.huosha vyombo 8.mwendo wamelegea legea kama wanawake 9. Huongea kwa kurembua rembua 10.HAWANA NGUVU kila siku kwa waganga kutafuta nguvu za kiume 11.wanakubali kuhongwa wakiita zali la metali
 
1. 'Wamukabili' mwanamke kwani mwanamke ni adui yao?
2. Kua na maelewano/majadiliano ndani ya nyumba kuna ubaya gani? Maana kinachowauma ni wazo la mwanamke kuweza kushauri/sisitiza kitu ambacho hata mwanaume anaona ndicho sahihi na sio zaidi ya hapo.
3. Wanafikia vipi kuoa? Na aliyekwambia kumtokea mwanamke ni ujasiri nani? Ujasiri onyesha kwenye kupambana na simba sio kutongoza.
4. Kumkodolea mtu macho kunamhakikishia vipi mtu uanaume wake umekamilika?
5. Hao unaowaongelea ni wavulana au tuseme watoto wa kiume na sio wanaume ndio wanaotongoza uchochoroni kwenye majani na kuta.
6.Kumpikia mke sio haki sawa, ni mapenzi na maelewano.
7. Wakati wanapokua single na wanaosha vyombo/au wale wanaofanya kazi mahotelini uanaume wao hua unachukuliwa na sabuni ehhh?
8. Unataka watembee kama wanajeshi wako jeshini?
9. Mtu anaongeaje kwa kurembua? Sauti nayo hua inarembua?
10. Wanawake nao wakipewa nguvu za kiume watakua wanaume? Wanaopata hayo matatizo kutokana na magonjwa kuumwa kwao nako ni kwasababu sio wanaume ehhh?
11. Hamna aliyezaliwa anacho. . . kika mtu anapewa kuendana na anachotoa.
 
jino kwa jino
 
Ndokeji,kindly refer uzi wa The Boss,tofauti kati ya 'wavulana' na 'wanaume'
Ukimaliza hapo rejea uzi wa Aspirin 'sisi wanaume bana'!
 
12 hata mavazi wanavaa kama wanawake, suruali nyekundu, za pink, za blue, blouses zenye darts, sarawili chupa/tite
 
wazee wakiona yote hayo na wakifanya comparison na enzi zao wanaget confused
 
Siku moja nikiwa na safiri kuelekea Dar esalam kutoka mbeya nikiwa kwenye kituo cha mabasi, kulikuwa na wazee wawili, walikuwa na maada ambayo walinifanya niwadadisi kwa undani zaidi ,wakidai kuwa vijana wa kiume wasasa hawana tofauti na mwanamke isipokuwa maumbile tu ndiyo yanawatenganisha mengine yote nisawa ,walitaja sababu 1. Vijana hawana ujasili. Wanaogopa kumukabili mwanamke 2. Kwenye ndoa mwanamke amekuwa na amri sawa na mwanaume 3. Waoga hata kumtokea mwanamke 4.wakikutanisha macho na mwanamke huwa wakwanza kuinamishwa kichwa chini 5. Akimtongoza mwanamke yeye ndiye wakuuma uma nyasi na kushika ukuta 6. Walio kwenye ndoa humpikia mwanamke wakidai haki sawa 7.huosha vyombo 8.mwendo wamelegea legea kama wanawake 9. Huongea kwa kurembua rembua 10.HAWANA NGUVU kila siku kwa waganga kutafuta nguvu za kiume 11.wanakubali kuhongwa wakiita zali la metali
mkuu na kushika ukuta zimo? bora nilivyokuwa sio kijana wa kisasa
 
12 hata mavazi wanavaa kama wanawake, suruali nyekundu, za pink, za blue, blouses zenye darts, sarawili chupa/tite

Ni kweli vijana wengi wa sasa wameharibika sana,vitendo vya kupaka poda,lipshine,kuvaa hereni,kuweka nywele dawa,kupaka mkorogo, kuvaa majeans ya kike na vitopu,kuongea kwa mapozi kwa kubana pua kuliko wasichana,kutembea kwa mikogo kuliko wakinadada.
Kusuka nywele..ni baadhi ya vitu vinavyoonyesha kupotoka kwa wavulana wengi wa kizazi hiki!
Mungu awanusuru!
 
Heeheeeheeee! Ni vizuri kuwa walikuwa wanawaongelea wavulana... siyo wanaume!!! Na hao wazee kuna kitu walisahau sijui ni kwa sababu ya uzee?! Wavulana wanapenda sana kuacha wazi na kuyaonyesha makalio yao pamoja na kuwa hayana mvuto wowote...!!! Pyutuuuuu.
 
umenena vyema dada!

1. 'Wamukabili' mwanamke kwani mwanamke ni adui yao?
2. Kua na maelewano/majadiliano ndani ya nyumba kuna ubaya gani? Maana kinachowauma ni wazo la mwanamke kuweza kushauri/sisitiza kitu ambacho hata mwanaume anaona ndicho sahihi na sio zaidi ya hapo.
3. Wanafikia vipi kuoa? Na aliyekwambia kumtokea mwanamke ni ujasiri nani? Ujasiri onyesha kwenye kupambana na simba sio kutongoza.
4. Kumkodolea mtu macho kunamhakikishia vipi mtu uanaume wake umekamilika?
5. Hao unaowaongelea ni wavulana au tuseme watoto wa kiume na sio wanaume ndio wanaotongoza uchochoroni kwenye majani na kuta.
6.Kumpikia mke sio haki sawa, ni mapenzi na maelewano.
7. Wakati wanapokua single na wanaosha vyombo/au wale wanaofanya kazi mahotelini uanaume wao hua unachukuliwa na sabuni ehhh?
8. Unataka watembee kama wanajeshi wako jeshini?
9. Mtu anaongeaje kwa kurembua? Sauti nayo hua inarembua?
10. Wanawake nao wakipewa nguvu za kiume watakua wanaume? Wanaopata hayo matatizo kutokana na magonjwa kuumwa kwao nako ni kwasababu sio wanaume ehhh?
11. Hamna aliyezaliwa anacho. . . kika mtu anapewa kuendana na anachotoa.
 
Ulimwengu wa wazee wetu na wa sasa ni tofauti hiyo ndiyo inawafanya waone wanaume wa sasahivi wapo tofauti. UKANDAMIZAJI NA KUMFANYA MWANAMKE SI BINADAMU HIYO ILIKUWA MAIN IDEOLOGY YA WAZEE WETU HAIFAI. WATUACHE TUANDIKE CHAPTER YETU YA KWAO IMEPITA
 
Back
Top Bottom