Wanaume tunapopiga kura ya Macho; Universal Language...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,462
39,928
Wanaume tuna lugha moya tunayoelewana na kukubaliana mahali pote duniani. Lugha hii wanawake wanaweza kuihisi lakini ni ngumu sana kuilewa kwa wao pia wana lugha yao inayowaunganisha wanawake wote duniani. Kwa upande wetu wanaune lugha hii ina sehemu kubwa mbili;

1. Kukubaliana juu ya uzuri au mvuto wa mwanamke
Wanaume wanapokuwa pamoja haijalishi wapi na ni kina nani huweza kuangaliana na kukubaliana juu ya mvuto wa mwanamke fulani. Mwanamke anaweza kuwa anajipitia zake au yuko katika shughuli zake lakini wanaume wanapiga kura ya macho nakukubaliana kama huyo dada kweli anavutia. Maeneo makubwa kadhaa husababisha kura hii ya 'ndiyo' au 'hapana':

a. Umbo, Uzuri na Mavazi Vote (Figure, Beauty and Dress combo)
Hii ni kura ya juu kabisa ambayo mwanamme anaweza kuipiga kwa macho yake anapomuona mwanamke. Yaani, anakubaliana kabisa mwanamke huyo "katoka" kweli na anapendeza. Labda wanawake asilimia 20 tu wanaotembea mitaani hupata kura hii ya nadra. Mara nyingi hata hivyo kura hii hupigwa kwanza na mtu wako kabla hata hujatoka ndani. Mwanamme asiyepiga kura hii mara moja kwa mwenza wake kabla hawafungua mlango na kwenda nje hujiandalia matatizo; mwanammke usiposifiwa kuwa "umependeza" na mtu wako kabla hujatoka nje basi inabidi urudi kwenye kioo na kujiuliza na kama kweli jamaa labda alijisahau inapaswa umpe unyo.

Hata hivyo usijali sana maana kama kweli umependeza mwanamme wako atapata message tu za "pongezi" kutoka kwa wanaume wengine njiani ambao watakupigia kura bila hata ya ridhaa yake. Hapo ndipo unaweza kujikuta mkiwa njiani jamaa naye inabidi atoe kura yake kwa kukunong'oneza "umependeza hunny". Akikupata hivyo hadharani unatakiwa umrushie busu la ghafla - breaking news kiss!

b. Matiti and Cleavage Vote
Kura ya kawaida sana ambayo wanaume wanaipiga wakati mwingine bila kufikiria sana ni hii inayohusu seheu za kifua na wanawake wengine wanajua njia rahisi ya kumfanya mwanamme apige kura ya haraka ni mwongekano wa kifua. Hivyo, wanaume hupeana lugha ya 'seen that?' pale mwanamme anapopita huku kifua chake kikiwa aidha kimebarikiwa vyema au kimedokezwa kwa ubarikiio huo. Hili linahusiana na ukubwa au hata udogo wa kifua kwa wanaume haijalishi sana kwani inaweza kwenda kokote kutegemeana na mwonekano wa kifua hicho. Njia pekee ya kuhakikisha wanaume hawaangalii kifua chako ni kuvaa athletic bra!

c. Matiti and Bottom combo
Kura hii nayo ni ya kawaida sana kutolewa na wanaume hasa katika mazingira ya tafrija au hata mitaani. Wanaume wengi hupiga kura hii na kukubaliana kwa macho kuwa msichana au mdada fulani kwa kweli kapendeza au anavutia. Hata hivyo kwenye suala la "bottom" mtazamo wa wanaume umegawanyika kwa jamii zao za watu huku watu wenye asili ya Afrika wakiwa wanavutiwa sana na maumbo ya vitunguu vya mviringo au maboga huku wengine kati yao wakivutiwa na bottoms za vibuyu vya maji. Watu weupe hata hivyo wengi wao wanavutiwa na kiasi tu cha mwelekeo huo. Hivyo, utaona wanaume weusi pote duniani wanajua na wanakubaliana endapo anapita mtu ambaye kajaliwa hivyo na hupiga kura hiyo kwa macho yao. Nimewahi kuona wanaume karibu watano wasiojuana ndani ya hoteli walitupiana macho na kuambiana "yes ma'am" alipopita dada mmoja - na walikuwa ni Walatino, weusi na weupe lakini walikubaliana kwa tabasamu la kufurahisha.

Uzuri wa hili ni kuwa wanawake wanaojua kwua Mwenyezi Mungu kawajalia hili hawawezi kulificha kwa kweli na mara nyingi hasaa katika kipindi hiki cha majira ya joto huvaa nguo ambazo zinawahakikishia kuwa hawana "mshindani". Hili hata hivyo limesababisha baadhi ya wanaume kujikuta wanazabwa makofi hadharani hasa baada ya kushindwa kufuataili ila kanuni ya "one second look" tena kwa kufuatisha macho na siyo shingo. Wanaume wa aina hiyo hujikuta wanageuza (kukata shingo) shingo kabisa na kusahau wanaenda wapi na kujikuta aidha wanagongana na mtu au kugonga kitu na kusababisha kicheko.

d. Bottom na Miguu combination
Sasa japo wengi hubarikiwa hivyo vingi hapo juu ni wachache pia utawakuta wamebarikiwa bottom na miguu a.k.a "usafiri", 11, n.k Wale Kwa kweli bado utafiti wa kutosha haujafanyika wa kuweza kuelezea ni miguu ya aina gani hupendwa zaidi lakini wanaume karibu wote hukubaliana wanapoona miguu ya aina fulani. Wapo malacelebrity duniani ambao hujulikana zaidi kwa miguu yao na hawafichi kuionesha hadharani hivyo. Lakini huitaji kuwa celebrity kwa wanaume kukubali usafiri wako kwani wapo wanaume ambao wataipigia kura miguu yako wakati "wowote, saa yoyote, na mahali popote" itakapojionesha.

2. Lugha ya onyo la kutokusogelea au kuangalia kisicho chako

Tunayo pia lugha ya onyo kwa wanaume wengine wasiangalie mara mbili kwa wale tulionao . Ni lugha ya kumwambia mwanamme mwingine "unatafuta ugomvi". Hii ni lugha ya vita kakini mara nyingi katika mazingira ya kawaida tunakubaliana. Hii hutumika zaidi katika maeneo ya hadhara (public places) kana movie places, hotelini, sokoni ambapo wanaume wanaweza kujikuta wanatumia haki ya kuzaliwa ya kuoiga kura kwa macho. Wanawake mara nyingi wanakuwa wa mwisho kutambua kuwa wanaume wameshapeana maonyo na tahadhari pale ngumi na matusi yanapoanza.

Lugha hii ya onyo hutumiwa kama ishara ya mtu kuwa mwangalifu. Mara nyingi wanaume wenyewe huielewa bila kuambiwa hasa kama anajikuta anampigia kura ya macho mtu ambaye alidhania yuko peke yake na mara moja mwenye mali anajitokeza; wanaume wenyewe hukatisha upigaji kura huo kwa sababu wanajua siyo "heshima". Hata hivyo wapo wanaume "watukutu" ambao hawajali kama yule mtu mwingine yuko na mtu wake au la kwani watajaribu kumfanya mdada wa watu ajue kapigiwa kura. Nimewahi kuona mahali fulani (msiniulize ilikuwaje) ambapo jamaa alijikuta anampigia kura za kila namna dada wa watu aliyekuwa amekaa na jamaa yake hadi mdada wa watu akatabasamu huku uso kauficha kwa "menu".

Jamaa akatuma ombi kwa "macho" na binti wa watu - sijui kwanini- akalikubali kiaina na jamaa akajifanya anatoka kwenda msalana na dakika chache baadaye binti naye akaenda msalana. Walibadilishana namba za simu. Sijui kilichofuata. Jamaa mwenye mali hata hakustukia wala nini. Hili pia hutokea sana kwenye madisco na kumbi za starehe hasa kama mwanamme hapei attention kwa mwenza wake wakati mamia ya wanaume wamekaa na kupiga kura za aina mbalimbali.
 
Hiyo namba mbili nimeshaiona sana kwa hubby. Yaani akinipitia lets say kazini basi anawakata jicho wanaume wenzie lile la "msimzoee wife"

Wabaume tuna lugha moya tunayoelewana na kukubaliana mahali pote duniani. Lugha hii wanaweka wanaweza kuihisi lakini ni ngumu sana kuilewa kwa wao pia wana lugha yao inayowaunganisha wanawake wote duniani. Kwa upande wetu wanaune lugha hii ina sehemu kubwa mbili;

1. Kukubaliana juu ya uzuri au mvuto wa mwanamke
Wanaume wanapokuwa pamoja haijalishi wapi na ni kina nani huweza kuangaliana na kukubaliana juu ya mvuto wa mwanamke fulani. Mwanamke anaweza kuwa anajipitia zake au yuko katika shughuli zake lakini wanaume wanapiga kura ya macho nakukubaliana kama huyo dada kweli anavutia. Maeneo makubwa matatu husababisha kura hii ya 'ndiyo' au 'hapana':

2. Lugha ya onyo la kutokusogelea au kuangalia kisicho chako
Tunayo pia lugha ya onyo kwa wanaume wengine wasiangalie mara mbili kwa wale tulionao . Ni ligha ya kumwambia mwanamme mwingine "unatafuta ugomvi". Hii ni lugha ya vita kakini mara nyingi katika mazingira ya kawaida tunakubaliana. Hii hutumika zaidi katika maeneo ya hadhara (public places) kana movie places, hotelini, sokoni ambapo wanaume wanaweza kujikuta wanatumia haki ya kuzaliwa ya kuoiga kura kwa macho. Wanawake mara nyingi wanakuwa wa mwisho kutambua kuwa wanaume wameshapeana maonyo na tahadhari pale ngumi na matusi yanapoanza.
 
wanawake pia tuna lugha yetu ambayo wanaume hawaielewi kirahisi. tatizo letu sisi ni hadi ujenge trust kujua kama huyo unayemstua ana kifua ama vipi.huwa na-enjoy sana kuwa mahali na watu (wadada) ambao ukifanya signal moja tu wanaelewa and u keep smiling all the time. maybe wanaume hawapeani signal wakati tunawakodolea macho?:dance::grouphug:
 
Wanaume tuna lugha moya tunayoelewana na kukubaliana mahali pote duniani. Lugha hii wanawake wanaweza kuihisi lakini ni ngumu sana kuilewa kwa wao pia wana lugha yao inayowaunganisha wanawake wote duniani. Kwa upande wetu wanaune lugha hii ina sehemu kubwa mbili;

1. Kukubaliana juu ya uzuri au mvuto wa mwanamke

a. Umbo, Uzuri na Mavazi Vote (Figure, Beauty and Dress combo)
b. Matiti and Cleavage Vote
c. Matiti and Bottom combo
d. Bottom na Miguu combination

2. Lugha ya onyo la kutokusogelea au kuangalia kisicho chako


Kweli wanaume mna kazi... wanawake tuna mtihani.... Alafu mnashanga akina dada kujichubua, kutumia mchina ama kuvaa nguo nusu uchi....
 
Kweli wanaume mna kazi... wanawake tuna mtihani.... Alafu mnashanga akina dada kujichubua, kutumia mchina ama kuvaa nguo nusu uchi....


kwa kweli; nimewahi kuwa na mjadala na rafiki yangu mmoja wa karibu na tukawa na mjadala huu; alisema wanaume ndio wanasababisha haya yote kwa kina dada - mambo ya liposuction, kujichubua, kuongeza viwowo, boob jobs, n.k n.k Kwamba wanaume tunapiga mno kura kiasi kwamba kina dada wanafanya kazi ya ziada ili kuwepo angalau kwenye TOP TEN. Upande mwingine ni kuwa tusipopiga kura za namna hiyo dada zetu wangekuwaje sasa si wote wangekuwa wanafanana na kina siye na ingekuwa dhambi... I think.
 
Ndio maana vibinti vinapokuwa unakuta vinabadilisha hata nguo kumi kwa siku ili akipita awe among top 10. Yaani kuna raha yake pale unapohisi wanaume wamekukubali. Though it doesn't mean kuwa msichana kama huyo anawataka hao wanaume ila lazima kuna ka kujisikia vizuri kama wanaume wanageuka ukipita. Habari ndio hiyo.
 
Ndio maana vibinti vinapokuwa unakuta vinabadilisha hata nguo kumi kwa siku ili akipita awe among top 10. Yaani kuna raha yake pale unapohisi wanaume wamekukubali. Though it doesn't mean kuwa msichana kama huyo anawataka hao wanaume ila lazima kuna ka kujisikia vizuri kama wanaume wanageuka ukipitoa. Habari ndio hiyo.

Kuna madhara yoyote ya kisaikolojia endapo binti aliyejitahjdi kutoka anajikuta hapigiwi kura uwezekano wa kuwemo kwemye 25 bora haupo?
 
kwa kweli; nimewahi kuwa na mjadala na rafiki yangu mmoja wa karibu na tukawa na mjadala huu; alisema wanaume ndio wanasababisha haya yote kwa kina dada - mambo ya liposuction, kujichubua, kuongeza viwowo, boob jobs, n.k n.k Kwamba wanaume tunapiga mno kura kiasi kwamba kina dada wanafanya kazi ya ziada ili kuwepo angalau kwenye TOP TEN. Upande mwingine ni kuwa tusipopiga kura za namna hiyo dada zetu wangekuwaje sasa si wote wangekuwa wanafanana na kina siye na ingekuwa dhambi... I think.


Hio ni common knowledge.. cha ajabu ni pale wanaume wanapoponda mdada anae jaribu kufanya efforts ili walau avutie mbele ya macho ya watu, hio ndo hua siwaelewi kabisa...

Nashukuru for the insight....
 
Haya mambo ni ya kweli. Binafsin nachukia mambo mawili.

1. Dada aliyetoka na mtu wake kupoteza umakini (concentration) na kuishia kukodoa macho kwa wanaume wengine kana kwamba kafanya chaguo baya na hovyo kwa huyo aliye naye. Hii imenitokea mara nyingi na siipendi hii tabia.
2. Mwanamume kunifanya kana kwamba mimi ni toy na kutumia muda mwingi kumwangalia mwenzi wangu....Laiti wote tungeweza kutoa ujumbe usio na utata kwa kutumia hiyo namba 2. Inanikera sana kufanywa kama vile sipo (I don't exist) wakati nimetoka na mtu wangu ili tujirushe!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Haya mambo ni ya kweli. Binafsin nachukia mambo mawili.

1. Dada aliyetoka na mtu wake kupoteza umakini (concentration) na kuishia kukodoa macho kwa wanaume wengine kana kwamba kafanya chaguo baya na hovyo kwa huyo aliye naye. Hii imenitokea mara nyingi na siipendi hii tabia.
2. Mwanamume kunifanya kana kwamba mimi ni toy na kutumia muda mwingi kumwangalia mwenzi wangu....Laiti wote tungeweza kutoa ujumbe usio na utata kwa kutumia hiyo namba 2. Inanikera sana kufanywa kama vile sipo (I don't exist) wakati nimetoka na mtu wangu ili tujirushe!


...mstaafu umenikumbusha mbali sana.
Tabia hizo mbili hata mimi zilikuwa zinanikera sana.

Hata hivyo, inategemeana na Mwanamke uliyenaye. Kama yeye macho juu juu, wanaume wata respond.
Kama ni mtu wa kujistahi, nawe kukupa heshima yako...ni raha mustarehe.

Ama hili ni jambo kubwa la kuzingatia tangu wakati mpo kwenye uchumba.
Mwanamke mapepe hafai!
 
Hii ni kweli kwa kuwa siku hizi wanaume wamekuwa wanapenda vitu vinavyoonekana zaidi,na hayo ndo chanzo cha kuwepo biashara ya mwili coz baadhi ya wanaume hutamani na wanachotamani ni mwili wa mwanamke,matokeo yake akishakula na kushiba anakinai na hana shida tena coz amepata alichokuwa anataka,wanawake wasimjiamini na wanaotaka wataminiwe ndo wanakuwa kwenye tatizo hilo la kujichubua nk!
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom