Wanaume tukumbushane tulipobalehe

Mi nlikuwa nkimuona msichana nnaemfil tu mapigo ya moyo huzd spid km mtu aliekimbia masafa marefu na ilhali nimesimama!
 
Hii ni barua yangu ya kwanza kabisa ya kutongoza.

61969_442761964109_696474109_4986692_7706433_n.jpg

EMT duuh we mkali,
hapa ulikuwa na umri gani hivi
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Moja ilitokea Hm na mtoto wa mama mdogo wa kike. Aliletwa kwa ajili ya kukaa na mtoto wa sista. Si unakumbuka kufuli zilianza kuvaliwa ukubwani. Basi nilitia bonge la kaptula la kaki, halafu kumbe kati ina tobo. Mtoto kaja ndo nae keshabalehi. Mimi nimekaa zakari ziko nje. akaanza kunitani (umeficha mayai kwenye kaptula) huku anasogelea ashike. Nilimulabua kibao, kilio chake kilikuwa balaa. tulikuwa wenyewe, nikaanza kubembeleza. weee uchezo wa baba na mama usifanyike.
 
Heheheheh. . .
Mi mvulana alikua akiniambia "mambo?" namjibu "chupi ya mgambo". . ."ni vipi??" = "vipisi" anageuza zake.

hahahaha lizzy jamani u gonna scare the birds away bora kama ulishaacha hayo majibu!
 
kuna dada nilivutiwa naye nikiwa la tatu.. Alikuwa dawati la mbele yetu. Nikamwambia rafiki yangu wa dawati moja,yeye alikuwa akijifanya ni mjuzi wa mambo mengi. Akaniambia usipate shida,mwandikie barua.
Nikaogopa suala la barua,akasema angeandika yeye,na kuandika jina langu. Nikamwambia dili ikibaunsi tukifika kwa mwalimu mi na wewe urafiki wetu utaisha,we nipe mistari,niandike mwenyewe. Akaanza,mpendwa ......... Naomba kile kitu kilicho chini ya kitovu chako... Nikamuuliza mbona kama matusi? Ataelewa au ataona nimemtukana.. Akasema hiyo ndiyo njia ya kikubwa ya kufanikisha,na hakuna mwanamke yeyote anayekataa njia hiyo.

Akazidi kuniambia hata watu wazima,au walimu wa kike,yaani wanawake wote ni rahisi,na kuwa wanawake wanampenda mwanaume anayewatongoza. Mi kwa shingo upande nikanyosha nikampa na kumwambia akasomee nyumbani. Naye alikuwa mbishi,akasema atasoma palepale,bahati mbaya akamwonyesha na jirani yake. Ilikuwa ni aibu,kwani niliomba anirudishie barua yangu akakataa..mwenzake akampump,eti apeleke kwa mwalimu wa darasa,ambaye binti yule alikuwa ni bibi yake...

Nikamwomba radhi sana,ila hakuwa amechukia,ila alionyesha kutotegemea jambo lile kutoka kwangu.. Akaamua kwenda kwa mwalimu wa darasa ambaye alikuwepo mbele anaandika na kusahihisha daftari. Nilitamani ardhi ipasuke nidumbukie ndani. Nikaomba bora nichapwe yaishe,kuliko niiambiwe nije na mzazi wangu. Alienda dada yule na kukaa kama dakika tano,kisha akarudi akiwa ameninuna na amejaa hasira. Nikasubiria kuitwa,sikuitwa hata siku moja. Nadhani alinisamehe hivyo hakupeleka barua ile. Nilimlaumu aliyenipa mistari ya barua,naye akasisitiza,mwanamke kuichukia barua ile lazima atakuwa mshamba..Nilimshangaa sana. Uhusiano hata wa salamu ulikufa kati yangu na dada yule..

Cha ajabu tulipokuwa la saba nilirudia tena mchezo wa barua na dada yule. Nikamwambia akasomee nyumbani akasema hataki kusubiri,ila alijawa furaha sana. Siku hiyohiyo tulikutana mstarini saa nane. Akaniambia angenijibu kesho yake. Sasa ikawa akiniona ananipenda ikaishia hapo.Kampani tu ya kawaida. Hata hivyo mi ilinitosha sana. Kwa sasa ameolewa ana watoto wawili,na ni air hostess wa shirika fulani la ndege..
 
hahahaha lizzy jamani u gonna scare the birds away bora kama ulishaacha hayo majibu!

Amy ndege wakiwa wawili watatu wanapendezesha kufurahisha masikio, wakizidi wanakua wasumbufu, kelele kila upande.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom