Wanaume na wanawake wanapolalamika................ ....!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Ngoja niyadadavue malalamiko ya wanawake kwanza hapa chini:

1. Wanawake wanalalamika kwamba wanaume sio waelewa wazuri, yaani huwa wanatafsiri mambo tofauti na isivyo.

2. Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawajali hisia za wapenzi wao wala hawajali pia kuhusu mahitaji yao.

3. Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawajui kuonesha upendo , yaani hata wanapopenda inakuwa kama vile wanajisumbua tu, kiasi kwamba mwanamke anaweza kuhisi kwamba hapendwi.

4. Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawana muda wa kucheza na wapenzi wao kabla hawajafanya nao mapenzi yaani hawawaandai kabla ya tendo, wao huwarukia tu na kumaliza haja zao haraka na kugeuka ukutani kabla ya wao (wanawake) hawajaridhika.

5. Wanalalamika kwamba wanaume hawana mawasiliano, huwa hawajui kueleza hisia zao na mawazo yao, bali ni watu wa kunyamaza na kujifungia kwenye dunia yao wenyewe. Wanahisi kama kuelezea hisia zao na mawazo yao ni kuwa dhaifu.

6. Wanawake hulalamika kwamba, wanaume hawana muda wa kukaa nyumbani na familia zao, kwa sehemu kubwa ni watu wa nje tu.

7. Wanawake pia wanawalaumu wanaume kwamba, hawajali mustakabali wa usafi au kupendeza kwa nyumba.

8. Wanawake wanawalalamika kwamba, wanaume huwa wanafanya maamuzi yao bila kujali kuwa wanawake wapo na wanaweza kuwa na michango mizuri sana kwa hicho wanachotaka kukifanya. Huamua kama kwamba wanawake siyo sehemu ya familia.

9.
Wanalaumu kwamba, wanaume ndiyo wanaoanzisha au kuendekeza kutoka nje ya ndoa ukilinganisha na wao wanawake.

Malalamiko ya wanaume nayo nayadadavua kama ifuatavyo…..

1. Wanaume wanalalamika kwamba wanawake ni watu wa kulalamika, kukosoa na wenye vijineno vya hapa na pale visivyo na maana na vyenye kukera.

2. Wanaume wanalalamika kwamba wanawake wanajaribu sana kuwadhibiti na kuwakandamiza pale wanapoachiwa nafasi kidogo.

3. Wanaume wanadai kwamba wanawake huwa hawana furaha, mara nyingi wanaonekana kama vile wako kwenye simanzi fulani na wanapenda sana kununanuna hasa pale wanaume wanaposhindwa kuwatekelezea kile walichotaka hata kama hakina umuhimu kwa wakati ule.

4. Wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanawanyima unyumba kama adhabu ya kuwakomoa. Siyo kuwakomoa tu, bali huwa wanafanya hivyo kwa lengo la kuwashurutisha wakubaliane na utashi wao fulani.

5. Lalamiko lingine la wanaume kuhusu wanawake ni lile la kwamba, huwa hawafikirii kwa mantiki, bali mara nyingi kufikiri kwao huwa kunakumbwa na mhemko. Kwa hiyo, uamuzi wao mwingi hauangalii mantiki bali hujali zaidi hisia zao.

6. Wanawake wanalalamikiwa na wanaume kwamba, hali zao za kihisia huwa hazitabiriki. Yaani huwa zinabadilika kufuatana na mabadiliko ya miili yao ya kihomoni miilini mwao nyakati kama zile za siku zao(hedhi), nyakati za ujauzito na hata wanapokoma kuziona siku zao(menopause) .

7. Wanaume wanawalalamikia wanawake kwa tabia yao ya umbea, kwamba midomo yao huwasha sana hadi waseme kile walichokiona au kukisikia hata kama si lazima na pengine ni hatari.

8.
Wanawake wanalalamikiwa pia na wanaume kwamba, huwa wanatoka nje ya ndoa, hasa wanapohisi kukosewa upendo ndani, jambo ambalo haliwezi kuleta suluhu kwa tatizo hilo.

Kama wewe ni mwanaume na umegundua kwamba moja au baadhi ya malalamiko ya wanawake yanakugusa inabidi ubadilike na kufanya kinyume chake. Kama wewe ni mwanamke pia hali ni kama hiyo. Kama kweli una mdomo mwingi kwa mfano, ujue wanaume hawapendi tabia hiyo, hivyo huna budi kubadilika.
 
Naomba nikiri kwamba, kwenye malalamiko ya wanawake namba 5 na namba 8 zimenibamba..............
Duh, inabidi nibadilike kwa kweli................LOL
 
Umeonaee, Kasoro za wanaume 9 vs 8. Badilikeni!
Najua wanawake wengi mtasimamia hapo...............
Lakini na nyie wanawake malalamiko yetu kwenu, namba 3 na namba 4 zinawabamba sana.................LOL
 
Hiyo #4 mtoto akikosa lazima aadhibiwe...atajua vipi amekosa
Sasa ndio tunyimane UTUKUFU.....!
Kwani hakuna adhabu nyingine mpaka iwe hiyo?..............badilikeni bana..........!
 
wanawake
1 - wanalalamika kwa vile wanaume mara yigi wanakuwa a subira zaidi ila akina mama wanapenda uharaka kwa kulinganisha a kwa fulani.
4 - ni kweli tendo ndani ya ndoa limebaki kama mazoea tu kutokana na kuwa a mabadiliko mbali mbali wakati wa ndoa
5 - mawasiliano hukosekana kutokana na kujisikia / kudhalau / heshima
8 - kweli wakinamama wengi huamua kutokana na kuiga do maana wanaume wengi hujiamulia kulingana a waonavyo

wanaume
1 - kuwa a vijisababu hata visivyolazimu
3 & 4 - furaha inakosekana kwa vile matarajio yake hayakuwa
7 - kutoa mambo ya ndani hasa kama maelewano si mazuri
 
Naomba nikiri kwamba, kwenye malalamiko ya wanawake namba 5 na namba 8 zimenibamba..............
Duh, inabidi nibadilike kwa kweli................LOL

hiyo namba tano wewe? mie naona unatania maana unajua kudakua vikibodi hadi basi. inakuwaje huko hivyo na humu weye unaleta habri mbwembwe za kufurahisha roho?
 
hiyo namba tano wewe? mie naona unatania maana unajua kudakua vikibodi hadi basi. inakuwaje huko hivyo na humu weye unaleta habri mbwembwe za kufurahisha roho?

Unajua hata mimi nina maudhaifu yangu.......... lakini kwa kuwa nimeshayajua, imekuwa ni rahisi kuya-control na hata Mama Ngina anajua na hunikumbusha pale anapoona nimetoka nje ya mstari.....

Jamani mimi sio malaika nina kasoro pia...............LOL
 
Haya Mtambuzi nakuja nimesoma ....msg nimeelewa vizuri sana...hasa hiyo ya malalamiko ya wanaume kwa wanawake natafakari
 
Haya Mtambuzi nakuja nimesoma ....msg nimeelewa vizuri sana...hasa hiyo ya malalamiko ya wanaume kwa wanawake natafakari
Hebu ninong'oneze, ni namba ngapi imekubamba................?
Leo hapa nataka ukweli na uwazi.
 
4. Wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanawanyima unyumba kama adhabu ya kuwakomoa. Siyo kuwakomoa tu, bali huwa wanafanya hivyo kwa lengo la kuwashurutisha wakubaliane na utashi wao fulani.

hizi bakora sioni kama zitakoma..................ukichanganya na hii archaic feminist movement...................that is gripping Africa by storm.......................si unatujua watu weusi na kuiga hata yale ambayo hayafai kuigwa?
 
Haya Mtambuzi nakuja nimesoma ....msg nimeelewa vizuri sana...hasa hiyo ya malalamiko ya wanaume kwa wanawake natafakari

FirstLady1 .....unatafakari ili utunyooshee mambo au utushughulikie zaidi ya sasa?
 
Hiyo #4 mtoto akikosa lazima aadhibiwe...atajua vipi amekosa

Ningelishangaa kama Mademex asingekuja na hii khoja............................lol yaekea tuko kwenye kitanzi................lakini usichojua ni kuwa huo ndiyo mwanzo wa kushamiri nyumba ndogo.......khalafu lawama hamjilaumu......
 
4. Wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanawanyima unyumba kama adhabu ya kuwakomoa. Siyo kuwakomoa tu, bali huwa wanafanya hivyo kwa lengo la kuwashurutisha wakubaliane na utashi wao fulani.

Hiyo #4 mtoto akikosa lazima aadhibiwe...atajua vipi amekosa

Ningelishangaa kama Mademex asingekuja na hii khoja............................lol yaekea tuko kwenye kitanzi................lakini usichojua ni kuwa huo ndiyo mwanzo wa kushamiri nyumba ndogo.......khalafu lawama hamjilaumu......

hizi bakora sioni kama zitakoma..................ukichanganya na hii archaic feminist movement...................that is gripping Africa by storm.......................si unatujua watu weusi na kuiga hata yale ambayo hayafai kuigwa?

Kaka hiyo namba 4 ni kiboko ya mambo, wengi inatushikisha adabu...............
Ndio maana mie huwa nalia ili nipate kuonewa huruma....................................................LOL
 
Heshima yako baba,
Kwa upande wangu naona malalamiko ya wanawake kwenda kwa wanaume yote yana ukweli na yanastahili kwan ndio ukweli mtupu kwa wengi wenu,

Na malalamiko ya wanaume kwenda kwa wanawake kuna baadhi ni kutuonea tu km 5 na no 6,

Sio kweli kuwa hatuwezi kuwaza kwa mantiki wakati familia nyingi zenye maendeleo mama ndio anakua mshauri mkuu,na hata wanaume wengi wakioa ndio wanakua na maendeleo zaidi kuliko kabla,

Na hili no 6,wanaume wanajua kbs hali hiyo ni ya kimaumbile sio mapnz yetu kuwa ivo,iweje walalamikie hali hiyo badala ya kuielewa tu na kuikubali kwani ndio tumeumbwa ivo,

Ila hiyo No 4 kwa wanaume binafsi siwezi kuitumia kbs na km atakua anaisubiri hiyo ili atake advantage atachemsha,km ikitokea tukazinguana basi tunawekana chini namweleza langu la moyon tena mapema kabla ya mda wa kulala,nahahakikisha tumelimaliza na kurudia hali ya kawaida ili tukiingia kulala mambo yaende fresh!!
 
Naomba nikiri kwamba, kwenye malalamiko ya wanawake namba 5 na namba 8 zimenibamba..............
Duh, inabidi nibadilike kwa kweli................LOL

Hapo tu ndipo ninapokukubali, l mean kwa kukubali mapungufu yako; Salute!!!!!!!!!
ingawa sidhani kama unajuhudi za dhati za kubadilika LOL
 
Najua wanawake wengi mtasimamia hapo...............
Lakini na nyie wanawake malalamiko yetu kwenu, namba 3 na namba 4 zinawabamba sana.................LOL

Aisee mimi hapo hakuna hata moja linalonibana; labda kiduuuuuchu no 6; l mean kiduuuuchu!
 
hizi bakora sioni kama zitakoma..................ukichanganya na hii archaic feminist movement...................that is gripping Africa by storm.......................si unatujua watu weusi na kuiga hata yale ambayo hayafai kuigwa?

Hivi, if l may ask; umegombana/zozana/korofishana (whaterver) na mpenzio unategemea atakuwa na nge (hamu ya tendo la ndoa) na wewe? Au unataka afanye tu kwa kutimiza wajibu? Kama hiyo ndio mnaita kuadhibu nitakubali lakini l thought ile kitu inahitaji romantic atmosphere fulani hivi.
 
Back
Top Bottom