Sasa labda mnisaidie na hili: Mimi kuna shost wangu ameishi na mwanaume miaka zaidi ya kumi sasa na huyo bwana alipata bahati ya kwenda kusoma UK alipomaliza shule akaamua na kuchukua uraia wa UK kabisa. Walizaa mtoto mmoja ambapo huyo bwana alipopata uraia akamchukua mwanae kwenda kuishi naye huko ila huyu shost akamwacha huku. Kila kukicha ni promises za kumwoa na kumhamishia UK lakini cha kushangaza miaka inazidi kuyoyoma dada wa watu yuko bado hapa bila bila. Sasa mdada amepata mtu mwingine hapa bongo na anataka kumwoa kikwelikweli. Huyu mdada anataka kukubali ndoa na huyu jamaa baada ya kuona miyeyusho ya huyo mchumba wa UK imezidi. Sasa anajiuliza je kwa miaka yote waliyokaa na huyo bwana na wana nyumba na magari walipata wakiwa pamoja kwa huo muda vitagawanyika vipi na je katika kugawana mali atajua huyo mtu huko UK ana utajiri kiasi gani ili kama ni pasu kwa pasu wagawane?? Nimeiweka hapa ili kama kuna mtu mwenye kujua zaidi amshauri huyu mdada maana ni rafiki yangu na sitaki adhulumiwe. thanks