Wanaume na manguo ya ndani

Suzie

JF-Expert Member
May 7, 2010
1,259
409
Jamani kaka na vijanaume vyetu mbona mnazidi kuvaa hizo kata K mpaka mnatia kichefuchefu, nimeangalia sijui tamasha la fiesta huyo anaitwa Ney yaani yeye ni boxer kabisa na wala sio bukta, Linex lakwake chafuu alafu kalianika, Jo Makini mtu mzima na yeye anavalia suruali chini ya makalio upuuzi mtupu. Nyie wakaka wa JF kabla hamjaanza kutusema mavazi wanawake embu wafundisheni wadogo zenu ndo tutawaheshimu au na nyie mmedondoshea mnatafuta soko dizaini Arabuni
 
FUATA MAMBO YAKO HAPO UTAKUFA NA PRESHA TU.....KAMA YESU MWENYEWE ALISHINDWA KUMFANYA KILA MTU AFUATE ANACHOKIPENDA SEMBUSE WEWE...Kama we hupendi ni bora ukakaa kimya kuliko kujipa pressure zisizo za maana... Ukizaa mfundishe tu mtoto wako asiwe hivyo...

HATA KWA WANAWAKE KELELE ZINAPIGWA NYINGI TU..... Lakini ndo yanaongezeka kuwa majinga ya mavazi
 
Kiusanii inakubalika,, ila hilo la hizo nguo zenyewe kuwa chafu ndilo la kujadili..
 
Hii ni kwa binadam yeyote kuwa personality yake ndiyo inaonesha nini anacho mwake kichwani nani aweza akawa.Iwe ulimbukeni au hata ushamba but it is too much....!Ya wezekana kwa kutokuwa na upeo finyu or even exposure kwenye swala zima la yeye nani awe ndio inafikia unakuta wanaigana na kuja na bad interpretation kwamba msaani lazima avae kata K ili nguo ya ndani ionekane.binafsi nawazarau sana.
 
Jamani kaka na vijanaume vyetu mbona mnazidi kuvaa hizo kata K mpaka mnatia kichefuchefu, nimeangalia sijui tamasha la fiesta huyo anaitwa Ney yaani yeye ni boxer kabisa na wala sio bukta, Linex lakwake chafuu alafu kalianika, Jo Makini mtu mzima na yeye anavalia suruali chini ya makalio upuuzi mtupu. Nyie wakaka wa JF kabla hamjaanza kutusema mavazi wanawake embu wafundisheni wadogo zenu ndo tutawaheshimu au na nyie mmedondoshea mnatafuta soko dizaini Arabuni

hupaswi kutuhukumu wanaume wote kwa kosa la jamii flani!hata hivyo wasanii wetu wengi hawajui mpngilio mzuri wa mavazi wawapo ktk kazi yao{show}...nijukumu letu wote kama jamii iliyostarabika pamoja na waandishi wa habari kuwaelimisha na kuwakosoa!
 
Back
Top Bottom