Wanaume mshindweeee! Kila mtu anaumia, lol!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Kuna mdada, miezi mitatu iliyopita alimfumania mumewe na mwanamke ambaye ni rafiki yake ingawa sio kiviiiiiiiiiiile! Kama kawaida ya wadada akalia weeeeeeee mwishowe akaamua kumsamehe mpenzi wake baada ya jamaa kuahidi kutorudia tena na kwamba eti alikuwa ni shetani tu-aisee ktk hili tumshukuru Mungu wanawake kuwa viumbe wenye huruma, kwa kweli wangekuwa kama sisi midume, walahi dunia ingekuwa imekwisha. Basi maisha yakaendelea kwa furaha kana kwamba hakikutokea kitu.

Wiki iliyopita jamaa wakati anapata moja moto moja baridi maeneo ya Sinza Mori, akaona gari inapita mbele kwa siti ya abiria amekaa mkewe. Bila kujali dereva wa gari ana uhusiano gani na mkewe, jamaa akalifuatilia gari hadi liliposimama mbele ya nyumba ya wageni. Geti lilipofunguliwa gari ikaingia ndani ya geti. Wakati jamaa analifukuzia gari, watu wakashangaa nao wakaamua kufuatilia-unajua tena umbea wa mjini. Jamaa alipoingia ndani kupitia geti dogo, akamkuta mkewe kakaa makochini pale reception. Bila kuuliza mwanaume akaanza kumkaripia mkewe eti ni malaya na amekuwa akimsaliti tangu zamani ndiyo maana na yeye aliamua kutoka na mwanamke aliyemfumania mwanzoni. Iweje mke wa mtu aende guest na mwanaume mwingine kama sio umalaya ni nini? Kila mtu alibaki kumshangaa yule mwanaume, kwani si alimkuta reception amekaa iweje adai amemfumania na mwanaume?

Swali kwa wanaume? Hivi kwa nini huwa tunajihesabia haki sana ktk mapenzi kiasi cha kutembea na wanawake lukuki halafu tunageuka mbogo pindi wanawake wanapoamua kuiga yale tunayowatendea wao? Je hii ni matokeo ya mfumo dume au ndo kusema tu kwamba ni kujona kwamba sisi ni bora kuliko wengine ambao hatujali hisia zao na maumivu ya kusalitiwa?

Jamani wanaume, tujiulize na kujirekebisha, suala la mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu....... ni lazima likomeshwe.

Nawasilisha!
 
unajua mie nasema kuwa sie wenyewe wanaume tunajinyimia chance...tngekuwa hatuwaiti majina hawa wanawake oh wewe malaya or wewe kicheche naona tungekuwa tunafaidi sana kwani wanawake wangekuwa wanajiachia na kupata raha ya tunda bila kuwa na wasiwasi wakuwa judged na sie tusinge sumbuka sana katika kifukuza na kumpata demu.
 
mkuu ngoja nikalale maana hiyo lugha yako ya matamanio, hali ishanibadilika mie, mweeeeee! naenda kulala mimi
 
hujamalizia bana........... je ni kweli huyo mdada alikuwa katika michakato ya kuisaliti ndoa yake hapo guest au ilikuwa ni mambo ya kibiashara tu...........au ni hii miwani yangu, sijaelewa.
 
Haikujulikana mwenye mali si alikuja on time nadhani ndo akaharibu kwani jamaa hakuchelewa hata dk 3 kuwahi ndani. Ila kwa mazingira alowakutia ni wazi njemba ilikuwa inaenda kula mzigo sema tu mwenye mali aliwahi.
 
hii ndo raha ya jf, hata kama uko mgonjwa vp, utajitahidi utumie hata vidole vya miguu kufikisha ujumbe uupendao, hahahahahaaaaaaaaa! Mtambuzi natamani tu nikuvunje mbavu usiku huu. kucheka kwako ndiyo faraja ya mama ngina, si anajua ma care anayotoa kwa mgonjwa yana pay dividends!
 
Hiyo Story mbona hujamaliza!!

Tukumbuke Mkuki mtamu kwa nguruwe!!
 
ila unajua wanaume mnawafundisha wenyewe wanawake usugu, akishakufumania nae anaenda kujiachia kwa raha zake.
 
hujamalizia bana........... je ni kweli huyo mdada alikuwa katika michakato ya kuisaliti ndoa yake hapo guest au ilikuwa ni mambo ya kibiashara tu...........au ni hii miwani yangu, sijaelewa.

ashasema mambo ya umbea mitaani so usitegemee story kuwa na tamati ya kueleweka..
 
angetulia aone muvi nzima
mwanamke akishakufamania atakusaheme lkn lazima atalipiza
wachache sana labda kati ya 100 mmoja kwani akishapoteza imani kwako ndio kwishney lazima nae aonje dozi
aisee hakuna alie mkamilifu labda wazazi wetu
 
angetulia aone muvi nzima
mwanamke akishakufamania atakusaheme lkn lazima atalipiza
wachache sana labda kati ya 100 mmoja kwani akishapoteza imani kwako ndio kwishney lazima nae aonje dozi
aisee hakuna alie mkamilifu labda wazazi wetu[/QUOTE]

hapo kwenye red and bolded: mkuu watake radhi wazazi ako, yaani huna hata imani kamili kwao, mweeeee!
 
Kulaaaaaaaaaaaleki!

Leo ndo nimegundua kumbe ndyoko ni SHE!

Poor me!!
 
Kuna mdada, miezi mitatu iliyopita alimfumania mumewe na mwanamke ambaye ni rafiki yake ingawa sio kiviiiiiiiiiiile! Kama kawaida ya wadada akalia weeeeeeee mwishowe akaamua kumsamehe mpenzi wake baada ya jamaa kuahidi kutorudia tena na kwamba eti alikuwa ni shetani tu-aisee ktk hili tumshukuru Mungu wanawake kuwa viumbe wenye huruma, kwa kweli wangekuwa kama sisi midume, walahi dunia ingekuwa imekwisha. Basi maisha yakaendelea kwa furaha kana kwamba hakikutokea kitu.

Wiki iliyopita jamaa wakati anapata moja moto moja baridi maeneo ya Sinza Mori, akaona gari inapita mbele kwa siti ya abiria amekaa mkewe. Bila kujali dereva wa gari ana uhusiano gani na mkewe, jamaa akalifuatilia gari hadi liliposimama mbele ya nyumba ya wageni. Geti lilipofunguliwa gari ikaingia ndani ya geti. Wakati jamaa analifukuzia gari, watu wakashangaa nao wakaamua kufuatilia-unajua tena umbea wa mjini. Jamaa alipoingia ndani kupitia geti dogo, akamkuta mkewe kakaa makochini pale reception. Bila kuuliza mwanaume akaanza kumkaripia mkewe eti ni malaya na amekuwa akimsaliti tangu zamani ndiyo maana na yeye aliamua kutoka na mwanamke aliyemfumania mwanzoni. Iweje mke wa mtu aende guest na mwanaume mwingine kama sio umalaya ni nini? Kila mtu alibaki kumshangaa yule mwanaume, kwani si alimkuta reception amekaa iweje adai amemfumania na mwanaume?

Swali kwa wanaume? Hivi kwa nini huwa tunajihesabia haki sana ktk mapenzi kiasi cha kutembea na wanawake lukuki halafu tunageuka mbogo pindi wanawake wanapoamua kuiga yale tunayowatendea wao? Je hii ni matokeo ya mfumo dume au ndo kusema tu kwamba ni kujona kwamba sisi ni bora kuliko wengine ambao hatujali hisia zao na maumivu ya kusalitiwa?

Jamani wanaume, tujiulize na kujirekebisha, suala la mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu....... ni lazima likomeshwe.

Nawasilisha!
Mungu ametuonya tusi zini. Katika kutoka 20:14 imeandikwa, "usizini".
Kumwacha mke wako au mume wako na kuoa mtu mwingine yaweza kuwa halali kwetu lakini kwa Mungu ni dhambi. Luka 16:18 inasema "Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini."
Kutamani mtu asiye mume au mke wako nikuzini katika Mathayo 5:27 -28 "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake."
Yesu alimchukulia vipi mwanamke aliyeshikwa akizini? Yohana 8:10-11 Inasema, " Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? je! hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? akamwambia, hakuna Bwana. Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Endazako; wala usitende dhambi tena."
Nimapenzi ya Mungu tusizini. Imeandikwa katika Wathesalonike wa kwanza 4:3 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, muepukane na usherati."
 
Tokea enzi ya mitume na manabii: wanaume ruksa kutembea na wanawake lukuki. wapi umesikia mwanamke kaoa wanaume zaidi ya mmoja? Baba yangu alikuwa na wake watatu.
 
Haikujulikana mwenye mali si alikuja on time nadhani ndo akaharibu kwani jamaa hakuchelewa hata dk 3 kuwahi ndani. Ila kwa mazingira alowakutia ni wazi njemba ilikuwa inaenda kula mzigo sema tu mwenye mali aliwahi.

huyo jamaa sio mzoefu, utaendaje kwenye eneo la tukio ukiwa umeambatana na bomu, madhara yake ndio hayo............. mambo hayo yanataka uzoefu bana............... mnapanga miadi kisha mnakutana kwenye eneo la tukio kila mtu anakuja na njia yake na kurudi vivyo hivyo.. hakuna kuongozana kama mabata..............lol
 
Mungu ametuonya tusi zini. Katika kutoka 20:14 imeandikwa, "usizini".
Kumwacha mke wako au mume wako na kuoa mtu mwingine yaweza kuwa halali kwetu lakini kwa Mungu ni dhambi. Luka 16:18 inasema "Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini."
Kutamani mtu asiye mume au mke wako nikuzini katika Mathayo 5:27 -28 "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake."
Yesu alimchukulia vipi mwanamke aliyeshikwa akizini? Yohana 8:10-11 Inasema, " Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? je! hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? akamwambia, hakuna Bwana. Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Endazako; wala usitende dhambi tena."
Nimapenzi ya Mungu tusizini. Imeandikwa katika Wathesalonike wa kwanza 4:3 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, muepukane na usherati."

duh! wewe unafaa kuwa mhubiri aisee............ kipaji hicho mkuu
 
The tricky part of our lives is the fact that we so badly need each other. Mdau wa mambo ya mwanamke ni mwanaume na kinyume chake pia.
 
Back
Top Bottom