Wanaume kuwaficha wake zao juu ya akaunti zao. Why??

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Baadhi ya wanaume wamekuwa na akaunti ambazo hazijulikani na wake zao (Yaani hazijulikani kuwa zipo, sio zina sh ngapi..).

Mfano mzuri ni stori ya leo kwenye magazeti kuwa baada ya hali ya milipuko ya G,mboto, kuwa mbaya mwanamke mmoja anaeleza kuwa mume wake 'aliungama' kwake mambo kadhaa, ikiwemo kumpa taarifa juu ya akaunti ambazo huyo mke alikuwa hazijui...

Swali; Ni sababu zipi zinaweza kumfanya mwanaume awe na akaunti ambayo mke wake haifahamu?
 
ntarudi baadae ila ni kweli wanaume wengi huficha baadhi ya Account zao tena hasa wa Kichagga, kuna jamaa aliwahi niambia wahindi wanaweka wazi mambo yao ya kifedha kwa wake zao including turnout na mzunguko wa biashara ndio maana wanafanikiwa.
 
Jiulize kwa nini Bank wanapokupa ATM kadi wanakuambia ile namba ya siri usimpe yeyote na uliharibu lile karatasi linalokuwa na ATM card password. Hapo ndo utajua jibu unaloliuliza hapa. Pia sidhani kama account number inafichwa maana imeandikwa kwenye ATM card hivyo mkeo anaweza kuisoma na kuandika pembeni kwa matumizi yake kama anahitaji
 
Mimi naamini kua kumweleza mke au kutomweleza kunachangiwa na mambo mengi, kwanza usiri ndani ya familia- mke awezakua kila anapozungumza na shoga,ndugu au rafiku aweza kueleza tunahela nyingi,au mme wangu tajiri kuliko wako nk.
pili nidhamu ya matumizi, mke aweza kuhitaji kwa matumizi yasiyo ya lazima alimradi tu zipo na anafahamu zipo. na tatu ni uaminifu, anaweza kuchukua kiasi kidogo kidogo au hata kikubwa bila taarifa ya mumewe na siku zikihitajika anasema nilitumia kwa matumizi ambayo mumewe hayafahamu.

Msishangae saana yapo hayo.
 
ntarudi baadae ila ni kweli wanaume wengi huficha baadhi ya Account zao tena hasa wa Kichagga, kuna jamaa aliwahi niambia wahindi wanaweka wazi mambo yao ya kifedha kwa wake zao including turnout na mzunguko wa biashara ndio maana wanafanikiwa.

Hapa umegusa patamu, maana iliwahi kuelezewa sana tabia za wanawake wa kichagga hapa... Kuwa kama umemuoa, helayako yake,na yake yake... Kuwa atafanya kila linalowezekana kuendeleza kwao kabla hata ya mambo ya muhimu ya familia yenu... Kuwa anaweza kuwa na akaunti yake yenye hata mil 10, lakini akiona laki yako anaitaka... n.k

Inawezekana hii ndiyo inaweza kuwa imewafanya wanaume wa huko, walau wawe na ka-akiba ambako wifi hakafahamu?
 
Baadhi ya wanaume wamekuwa na akaunti ambazo hazijulikani na wake zao (Yaani hazijulikani kuwa zipo, sio zina sh ngapi..).

Mfano mzuri ni stori ya leo kwenye magazeti kuwa baada ya hali ya milipuko ya G,mboto, kuwa mbaya mwanamke mmoja anaeleza kuwa mume wake 'aliungama' kwake mambo kadhaa, ikiwemo kumpa taarifa juu ya akaunti ambazo huyo mke alikuwa hazijui...

Swali; Ni sababu zipi zinaweza kumfanya mwanaume awe na akaunti ambayo mke wake haifahamu?

Sababu mojawapo, huyo mwanaume ana nyumba ndogo ambayo anaidumia kupitia account hiyo; pili huyo mwanaume hamwamini mkewe, na ana mpango wa kumwacha huko mbeleni!
 
Jiulize kwa nini Bank wanapokupa ATM kadi wanakuambia ile namba ya siri usimpe yeyote na uliharibu lile karatasi linalokuwa na ATM card password. Hapo ndo utajua jibu unaloliuliza hapa. Pia sidhani kama account number inafichwa maana imeandikwa kwenye ATM card hivyo mkeo anaweza kuisoma na kuandika pembeni kwa matumizi yake kama anahitaji

hapo nakubaliana nawe mkuu.umeongea kama wazee kumi.
 
Wanawake wengi sio wasiri ndio maana hawaambiwi siri kama hizo!!!Wanapenda kujitapa kwa wenzao na utegemee lundo la matumizi kama akaunti ina hela!!!Eva alidanganywa kirahisi na nyoka na maswala ya hela yanagusa uhai na ustawi wa maisha.
 
Ninakubaliana nanyi, mwanamke akishajua kuna pesa , yeye ndo wakwanza kuanza kupanga matumizi. hata kama pesa hiyo umeiweka kwa ajili ya shughuli fulani. atafanya kila njia aweze kuzitumia. atakopa litu anakwambia anadaiwa hiki au kile ili mradi tu anajua pesa ipo. mengine unaweza ukaona ni sababu za msingi- for good. lakini ndo malengo yanapotezewa hapo.
 
Wanawake wengi wana matumizi mabaya hasa wakijua ana mwanaume anamtegemea kama mumewe au mpenzi wake. Hivyo ni jambo la kawaida kabisa mwanamke kutumia hadi senti ya mwisho kwa mambo yasiyo ya lazima kama urembo nk, akijua kuwa mumewe kesho atampa zingine
 
Wanawake wengi sio wasiri ndio maana hawaambiwi siri kama hizo!!!Wanapenda kujitapa kwa wenzao na utegemee lundo la matumizi kama akaunti ina hela!!!Eva alidanganywa kirahisi na nyoka na maswala ya hela yanagusa uhai na ustawi wa maisha.
BOLD: kunaaaaa....ka ukweli flani hapa
 
ntarudi baadae ila ni kweli wanaume wengi huficha baadhi ya Account zao tena hasa wa Kichagga, kuna jamaa aliwahi niambia wahindi wanaweka wazi mambo yao ya kifedha kwa wake zao including turnout na mzunguko wa biashara ndio maana wanafanikiwa.

Mbona kuna contradictions?
Wachagga na Wahindi wote husemekana kuwa wanafanya biashara na kufanikiwa .Mchagga anaficha accounts zake, mhindi anaweka wazi...hapo pananichanganya kikubwa. Kufanikiwa inatokana na kuweka wazi accounts?.......
 
Mh mimi sina cha kuficha, kila kitu peupeeee! Hata ATM card tunabadilishana
 
kuna akaunti za pamoja na hii ya kwangu iendelee kuwa ya kwangu......kwani akaunti ni namba au pesa?...okey kama ni namba achukue hii hapa 01j1024235683

''the man is nothing but the secrecy and self reliance''
 
Jiulize kwa nini Bank wanapokupa ATM kadi wanakuambia ile namba ya siri usimpe yeyote na uliharibu lile karatasi linalokuwa na ATM card password. Hapo ndo utajua jibu unaloliuliza hapa. Pia sidhani kama account number inafichwa maana imeandikwa kwenye ATM card hivyo mkeo anaweza kuisoma na kuandika pembeni kwa matumizi yake kama anahitaji

jibu hili limetulia.....ni hekima ya sulemani
 
Back
Top Bottom