Wanaume kupika na kupakua ni ushamba jamani??

Sielewi ajabu iko wapi mwanaume kupika na kupakua chakula. Mwanaume anapooa anatafuta msaada juu ya mambo ambayo hana uwezo nao, tena anataka uhakika wa kuwpata msaada huo wakati wowote anapoutaka. Kama ni kupika, mwanaume anao uwezo wa kupika kwa ladha anayoitaka na pengine anaweza kupika kumzidi mwanamke.

Msaada anaoutaka kila mtu mzima anaujua. Hana ufariji ambao ni mwanamke tu aliyejaaliwa kuwa nao. Adam alipoumbwa ilionekana wazi atauhitaji na ndio maana Hawa ilibidi afanyike kuwapo. Ni ustaarabu wa binadamu unaomfanya aoe, vinginevyo angekuwa mbuzi asingeoa lakini faraja bado akaipata.
ana heri mkeo kakaangu ubarikiwe sana
 
Mchili bana!!
Sasa hapa mjini wewe unapasua kuni saa ngapi?, unakaa kwenye shimo mpaka nyoka aingie ndani?
nini kitakuwa substitute ya zile natural devision of labour ambazo kwa kijijini, zinakuja kutokana na mazingira?
kuna vitu vingine, we do for the family............not for gender.

that's why nilijiunga na hii forum!!i second this,FOR THE FAMILY!'embu' nilielekeze kilipo ki-batani cha senksi 'nikucharazie' mkubwa!!!
 
Jamani naomba tusipotoshe mila zetu za kiafrika,particularly Tanzania.Kila mtu amepewa majukumu yake ya msingi,mwanamme anakazi zake za msingi,mwanamke vilevile.Kupika chakula na kupakua ni jukumu la msingi la mwanamke.Huko kwetu bara hata pwani mwanamme amepewa jukumu la kwenda kuvua samaki(kutafuta kitoweo) na au kupeleka ng`ombe malishoni(kuchunga).Haipendezi kumpa jukumu hilo mwanamke;atanuka vumba/shombo nakadhalika.kazi ya jikoni inamfaa mamaa.Iwapo mmojawao anakuwa na matatizo kama vile kuumwa nk.hapana budi kusaidiana.vinginevyo itasadikika kuwa hilo dume limeshabugia LIMBWATA la sivyo tunaweza sema ni mrafi.Ni maoni tu....
 
Back
Top Bottom