Wanaume Kupeleka Watoto Kliniki

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Kuna Mjadala huu wa wanaume kusaidia akina mama kuwapeleka watoto wao kiliniki!
Mtazamo mmoja unaona hili kama ni kubeba kila kitu cha wazungu na kwamba huu ni mtazamo ulipigwa tope la kikoloni. Kwamba haiwezekani, utakwendaje kliniki dume zima -- kwanza utajuaje kipimo cha maziwa. Kwamba haifai kabisa
Lakini wapo wanaoona kuwa kuna haja ya wanaume kuwasaidia wake zao -- hata kama inawezekana zamu za kuosha masufuria -- hapa ni vema tukapata uzoefu wa waliooa ama kuolewa na wazungu.
Pia jamii yetu inalaani sana hili, tena kwa jamii ya wagoyangi hili haliwezekani abadani, lazima watasema kala limbwata, lukomolo ama shuntama.
 
Huwa nampeleka mwanangu Klinik tangu amezaliwa. na majuzi mama yake alimpeleka wakamuuliza vipi baba anaumwa???

Mie sidhani kama ni vibaya kumpeleka mtoto klinic maana nadhani nikimpeleka nakuwa mwangalifu na mdadisi zaidi kujua maendeleo yake na pia nakuwa mmbeya kumweleza mtabibu kila kitu kuhusu mtoto ili nijue kama yupo sahihi au la. Pia naamini katoto kanaenjoy sana kubebwa na baba yake (hata akiwa ni mlezi). I am proudly kumsaidia wife wangu kumpeleka mtoto klinic na hii si limbwata kwani akinijia prety nitamsalimu kuanzia chini kwenda juu.
 
mie sioni tabu, na wala sio geni kwangu, baba yangu alikuwa akinipeleka klinic na hospitali, baba yangu huyo wala hakuwahi kuishi na wazungu wala uzunguni ni m-local kupindukia, kwahiyo kwangu mimi hili naona si kuiga uzungu, ni jambo la kawaida labda nitashangaa kuona mwanamme anaona aibu kumplekea mwanae klinik, nashukuru pia sijapata mwanamme mwenye asili ya huko kwenu au mwenye desturi hii ya kutokubeba au kupeleka mtoto hospital mbona ningeachwa mie!
 
angalieni siku zinakuja, yule aliye mkubwa na atakuwa kama mdogo

kusaidiana ni jambo jema sana kuliko, ....
 
Back
Top Bottom