Wanasiasa,vyombo vya habari,watanzania ni 'mcharuko' wa wasiasa

Do santos

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
635
334
Angalia siasa za tanzania zinavyoendeshwa,angalia vyombo vya habari,angalia wanasiasa na wananchi,kwa mtu makini atashangaa nini muelekeo wao,nini madai yao,nini wanataka. Ni mcharuko kila mtu aseme,alalamike na media zitangaze na wananchi washabikie. Ni vurugu tu. Serikali imekubali katiba mpya,wananchi wanaelimishwa mambo ya katiba? Si wanasiasa,media wala wananchi,wamesahau au..? Maandamano! Maandamano! Sasa kimya au..? Sasa ni Loliondo kwa babu...! Media zote,wanasiasa,wananchi habari ni Loliondo..!Loliondo..! Uvccm..! Urais 2015..! Vipi kuhusu katiba mpya,maisha magumu,mafisadi,umeme nk..! Wanasiasa wetu ni 'mcharuko' au 'waupepo' au msimu...! Wananchi je ni 'mcharuko' au 'mkumbo'..? Media nazo ni 'mcharuko'..! au ushabiki..? Tuliyoyadai,kulalamikia tumeyapata kuendea mengine? Mwafalsafa mmoja anasema 'kitakapokuwa kingi kizazi cha zinaa ktk jamii fulani,basi itegemee jamii hiyo mmomonyoko wa maadili,kukosa adabu,madai ya hovyo,kutamani vurugu,mkubwa kutomhurumia mdogo na mdogo kumdharau mkubwa' Nawasilisha ni mtazamo tu kama ntakukwaza pole sana
 
Back
Top Bottom