It is so sad that we are left with holes and people suffered from these skin diseases while the company is enjoying supernormal profit. This is the time we should say no to these exploitation and damages to human, animals and environment.
We should keep into accountability those who has involved in these scandals until the last minute
Inatia hasira sana jinsi watu wanavyonyanyasika katika nchi yao kwa sababu ya watu wachache wasiyo na Utu, wanaojari
kushibisha matumbo yao bila kufikiria cheo ni dhamana na duniani wote tunapita. Hakika rushwa ni Ugonjwa mbaya sana katika jamii.
Hivi kumbe jamaa wanamuhonga mpaka rais, shame on you JK, ndio maana wanaua hata hawachukuliwi hatua yoyote na wanazidi kulindwa. Its so sad. Naamini Mungu atatoa hukumu ya haki kwa wote walioshiriki kwa namna yoyote kutesa raia hawa wasio na hatia.
duh!
hii inatisha, hivi wanaharakati wetu wako wapi? wapi Deus Kibamba,wapi mama Ananilea Nkya,wapi Francis Kiwanga and Co?
inaumiza sana, uchunguzi wa wabunge uchwara wa Magamba hautatusaidia kitu, kama wanaparurana kwa posho ya 70K TZS je marushwa manene ya BARICK wanayaruka kweli? inahitaji ujasiri wa Kiungu kupambana na uharamia huu....
Kuna watu wengine wanasema eti hatuwezi kuwafanya kitu kwa kuwa tulisign mkataba, sidhani mkataba ulijumuisha ukatili huu??!
Kama nikiwa Rais nitakuwa dictator for at least 3 yrs kuwashughulikia wenye nia ovu dhidi ya raia wangu...ntafunga watu wote wanaonyamazia hali hii, hakuna cha mahakama wa nini...kama kuna watumishi wa issues za mazingira wanashinda kwenye viyoyozi halafu mie niwaache kisa utawala wa sheria!..nyambaf.
watumishi wa mazingira wote wapo Dar na bado viwanda vinatiririsha majitaka kwenye makazi ya watu i.e. TBL,KTM n.k kwa nini?? kwa nini??
agriiiiiiiiiiiiiiiiiii!ahuuuuuuuuuuuuuu! napata hasira.
Mbona vyombo vya habari nchini havituoneshi haya? Je, hawana uzalendo pia kama CCm na serikali yake?
Pili, kama muamar ghadafi ameonekana mbele ya jumuiya ya kimataifa hana sifa tena ya kutawala nchi yake kwa kuwa amegeuka muwaji wa raia anaowaongoza; imekuwaje serikali ya CCM haifananishwi na ghadafi? UNAFIKI WA WAMAREKANI NA WAZUNGU WA ULAYA WOOTE!!!!!
Global Apartheid...That's all what I can say regarding this video and what's happening in North Mara. Apartheid manipulating itself in different forms across different geographical places.
Kuna Makubwa zaidi ya hayo migodini, huko North Mara kunawakati alikuwepo GM kutoka Australia akiitwa Bill Macnevin, niliwahi msikia akisema "Rais Wenu hawezi kufanya Kitu, itakuwa Mbunge, Wabunge, Wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa wote waomba lift kwenye Ndege yetu".
Migodini kunazaidi ya Watanzania Wajuavyo ni SA mpya.
SISI WATANZANIA TUNA HURUMA SANA HURUMA YETU IMETUPONZA MPAKA TUNAFANYIWA HIVI NA TUNANYAMAZA KIMYA, TUNAPORWA RASIMALI ZETU NA KUNYANYASWALAKINI TUPO KIMYA, WAHENGA WANASEMA KIMYA KINGI KINA MSHINDO. LAKINI IS TOO LATE
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.