Wanasiasa na upendeleo ktk huduma za jamii

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,169
Tuna matatizo makubwa ktk Elimu na huduma za afya.

Ktk ubora wa matokeo ya mitihani ya shule za sekondari, Top ten ni shule za binafsi. Huko ndo wanakosoma watoto wa wanasiasa wetu. Wanaitwa ktk fundraising na wataoa pesa za serikali kusaidia shule za binafsi wakati za serikali zikiyumba kwa ukosefu wa pesa.

Wataalaamu wa tiba ni wachache kiasi cha kutia aibu. Lakini wanasiasa wetu wanakwenda kutibiwa nje.

Ziangalie hospitali za serikali. Kuna fani hatuna kabisa wataalamu au ktk hospitali kubwa kama Muhimbili, Bugando &KCMC yupo mmoja au wawili au hakuna kabisa. Kwa wale wachache waliopo hawapatikani. Kila wakati utaambiwa yuko ktk kazi zingine za serikali.
Mara nyingi wako ktk dispensaries au hospitali binafsi. Hili ni tatizo ambalo sitalizungumzia naamini linatokana na uzembe wa maamuzi ya Serikali.

Kwa kutaka upendeleo wanasisa wetu wanawatumia madaktari hawa kama madaktari binafsi wa familia zao. Madaktari hawa husafiri na mawaziri na hata wabunge. Kwa kuwa hulipwa posho, kwao hilo ni ‘dili’ kwa lugha ya sasa na Dk hujisikia vizuri, lakini kwa Dk bingwa anapoondoka na kuacha hospitali nzima haina mwingine wa kuwahudumia wananchi, ni uzembe wa kupindukia.

Tuna ulegevu ktk kuamua ni ipi nguvu ya Serikali na ni ipi ya ki-siasa. Sasa hivi hata Mbunge (muwakilishi wa wananchi) husafiri na muajiliwa kama huyu. Dk huacha wagonjwa na kwenda nyumbani kwa Mbunge kutoa tiba kwa mtoto au house girl wakati wa saa za kazi.

Mtindo huu ndo unawafanya wanasiasa hawa kutoona umuhimu wa kuboresha huduma za jamii, mbali na ofisi zao kutoa nafasi ya kutibiwa nje ya nchi. Hint niliyoipata ni kwamba ofisi ya spika ina fungu kubwa sana kwa ajili ya huduma kama hizi kwa wabunge.

Elimu sasa hivi iko ktk madaraja. Sekondari za kata siyo za wanasiasa. Taarifa za ndani ya Wizara ya Elimu na .... zinaonyesha tangu Rais, mawaziri, wabunge na wakurugenzi. Hakuna anayesomesha mtoto wake ktk shule ya kata. Lakini hawa wanaopongeza uanzishwaji wake.

Inanipa uthibitisho kwamba 'wataalamu' hupanga mipango ambayo hata wao hawana imani nayo na bado tunaamini wanatupangia mipango ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom