Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

umesema vyema sana nakubaliana na wewe asilimia mia. Lakini nikusahihishe kidogo tu kuwa tanzania haina uwezo wa kuipiga malawi nina huakika na hilo.
Pili ikitokea vita nina tamani sana tanzania ishindwe (mimi ni mtanzania ninaipenda sana nchi yangu tanzania.). hii inchi ya mafisadi ikipigwa then naamini kabisa itakuwa nchi ya watanzania baada ya vita.

unakusudia mama, baba, dada, na wazee wauawe tu kwa vita ama unaamini mafisadi ndo watakao pigana!? Fikiri ndugu!!
 
Tatizo ni kuwa Wamalawi tangu uhuru wanajua kuwa ziwa lote ni lao, hata ramani zao zote zinaonyesha hivyo, pia utafiti hajauanzisha Joyce, tangu mtangulizi wake utafiti ulifanyika katika ziwa lote, wanachoshangaa kwa nini Watanzania wamesubiri wakati wa Joyce kudai ziwa, mbona hawakudai wakati Bingu anafanya utafiti
 
Mipaka ya nchi lazima ilindwe kwa gharama zote. Swala hili siyo la kisiasa ni la Taifa, hapa wa Tz wote viongozi na wananchi wote wake kwa waume tunatakiwa kuacha itikadi zetu za vyama na kuwa kitu kimoja.

Umoja wa namna hiyo unafaa kwenye nchi za madikteta. Rais aliingize taifa vitani kwa sababu ambayo ingeweza kuepukika na sote tushabikie kwa sababu ya kuonesha "umoja"? Kama Malawi wangekuwa na nia mbaya tusingeweza kujenga bandari Mbambabay wala kuwa na meli na boti na uvuvi wa maelfu ya Watanzania kwenye ziwa hilo. Kama Malawi wanaoamini kuwa ziwa lote ni lao hawajaamua wala kutishia kwenda vitani kwa sababu tunatumia maji ya ziwa "lao" iweje sisi leo recklessly tuzungumzia mambo ya vita kwa sababu tu wao wanafanya exploration? Hawajazuia meli zetu, hawajaanza kufukuza wavuvi wetu kutoka ziwani?
 
Mwanakijiji kumbe una chuki kwa Lowassa na unaonekana LIVE, mbona unamtaja sana yeye kuliko Sitta alietangulia kwa kauli dhaifu ya eti hatutishwi na malawi?

Sitta alizungumza kama kwa niaba ya JWTZ? Sitta ana madaraka gani katika mambo ya ulinzi na usalama ukimlinganisha na Lowassa?
 
Watu wengi wanadhani Diplomasia hufanikiwa bila Millitary Background.Diplomasia na hatua za kijeshi nyuma ya pazia ndiyo DIPLOMASIA yenyewe.Hili nililijadili sana kwenye thread iliyopita

sasa hivi hakuna sababu ya kuzungumzia mambo ya military background ya kina Lowassa. Mambo ya kuzungumzia tuna uwezo, vifaa na teknolojia kuweza kupigana na Malawi yanakuja vipi? Diplomasia ambayo mtu kawekewa silaha kichwani ni diplomasia gani? Hamuwezi kuwa na diplomasia kama wote mmelekezeana silaha. La kwanza ni kuweka silaha chini ili kuzungumza.

Wote tunajua Malawi ina jeshi na TZ inajeshi na tunajua kuwa majukumu ya majeshi haya ni kulinda mipaka. Haiitaji watu kuringishiana majeshi.
 
Nashauru Serikali kuruhusu safe passage ya walechoka na wanchari Toka (Tarime) wanaopigana turaise jeshi twende Malawi tukagine huko hii haitakuwa mara ya kwanza kufanya hivyo tawala zote zilizotangaliwa zilifanya hivyo, ila tutakachoteka ni halali yetu. Kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imejiondelea mizigo miwili kwa mara moja. Isitoshe most Malawian accept poofters, so we can bit them hand down
 
Mwanakijiji rafiki MWEMA<
Tutakubaliana kwamba diplomasia ya kutatua migogoro haimaanishi kuwa taifa au jamii haina nguvu za kijeshi za kupambana na mvamizi.Maana yangu ya diplomasia ni kule kutambua kwamba vita ni gharama kubwa kwa pande zote tena kwa miaka mingi kiasi kwamba Sun Tzu anatuarifu kwamba hakuna mshindi wa vita!
Hizi kauli za Waheshimiwa Sitta, Lowassa,na Membe ni kauli za kujaribu kufukia OMBWE la kiuongozi lililo wazi kwa yeyote kwa maneno yanayofanana na yale ya aliyekuwa Waziri wa Habari wa Kamandoo Saddam kuwa Jeshi lao lingewachinja Wamarekani wote waliojipeleka Baghdad!Kilichotokea ni historia .Tuwe makini na kauli hizi za kujitafutia jina kwamba eti Fulani anafanania fanania na Chief -in -Command Mtarajali!Diplomasia itumike, International Law itumike na baada ya hapo busara ISIYOKUWA YA WAHESHIMIWA Sitta,Membe,Lowassa na hata AMIRI JESHI MKUU WA SASA, itumike kabla ya option hatari isiyo ya ushindi ya VITA!
 
Mwana kijiji Nakuheshimu sana kwa makala zako.Lakini kwa hili nafikiri umeteleza tena sana.Si vyema kwa wakati huu kuonyesha kile unacho onyesha.Maana naona watu wengine wasio ishi katika maeneo husika baada ya kusoma comments zako wanasema bora tuwaachie wamalawi hilo ziwa.
Suala la mpaka wa TZ na Malawi ni la kihistoria na umewahi leta hata mtafaruku kwenye mabunge ya Uingereza kipindi cha ukoloni mkongwe.Serikali yetu pia imeanza mazungumzo kwa mda mrefu pia.Ukianzia kwa awamu ya kwanza ilishindikana baada ya kuona Mawali ina sera tofauti na Tanzania ambapo sera ya TZ ilikuwa ni kusaidia nchi za afrika kujitawala wakati malawi ilikuwa ni maswahiba wa makaburu.Hali hiyo kwa malawi imeendelea mpaka leo hii maana nchi nyingi za africa zinapinga vikwazo vyo ulaya na marekani kuhusu Sudani na nchi zingine lakini Joyce Banda anaunga mkono.Pia nchi za Africa zimeukataa ushoga lakini malawi imeukubali na sababu ni kutaka tu misaada.
Wakati wa awamu ya nne, kumekuwepo na mazungumzo ya nchi hizi mbili ambayo yanaongozwa na wataalam wa mambo haya kwa nchi zote mbili.Lakini cha ajabu ni kuwa pamoja na mazungumzo hayo kuendelea, wenzetu tayari wameingiza makampuni yao kwenye eneo linalogombaniwa pamija na kuambiwa wasitishe shughuli hiyo, sasa hapa ulitegemea amirijeshi wa Tanzania akampigie magoti Joyce ambembeleze?
Kuna jinsi tofauti za ustarabu wa watu inabidi ujue.Kwa mkuu wa nchi kama Rais, jinsi anavyo tembea, kuongea , kukaa ,facial expression, gestures na body language ni lazima iwe tofauti na mwananchi wa kawaida kama mimi na wewe.Hiyo ni elimu ya kidiplomasia ambayo viongozi wetu hupewa.Mfano Obama anavyo wapiga piga mgongoni viongozi wenzie wa nchi nyingine si kuwa anafanya kwa bahati mbaya, hilo ni jambo alilofundishwa na limepangwa kuwa hivyo.Yeye kama baba wa dunia, kama wamarekani wote wanavyo amini ni kama vile baba anampongeza au kumtuliza mtoto wake kwa kumpigapiga mgongoni.
Pia viongozi hawa wakubwa wakikutana ni lazima watazamane usoni kwa msisitizo na macho makavu huku maki "shake mikono".Sasa hapo kama raisi wako akianza kuangalia chini au pembeni na anajiuma vidole ndo itaonekana watanzania wote mabwege maana kumbuka hapo anaiwakilisha nchi.
Pia jinsi ya kukaa wanapoongea pia ina mpangilio wake na mwisho ni kuwa hata kuingia kwenye mikutano, huwa kwa kwa maana ile ile wanajitahidi kuwa watu wa mwisho_Obama asingependa awe wa kwanza kuingia alafu Raisi toka malawi ndo awe wa mwisho, mara nyingi hapo kuna kuwa na busara kubwa za waandaaji wa mikutano hutumika.
Juzi juzi tu wamalawi walikuja juu baada ya kuona Raisi wao Joyce akimsalimia malkia Elizabeth kama vile anachuchumaa wakati wote ni Head of states.Si tu wamalawi walichukia bali watu wote duniani walishangaa na HII NDIO SABABU WAMALAWI WAKO AGGRESSIVE SASA HIVI MAANA WANADHANI KILA MTU SASA ANATAKA KUINYANYASA MALAWI KWA SABABU WANAONEKANA KUDHARAULIWA KWA SABABU YA HICHO KITUKO.
Kwa sababu hiyo hiyo , linapokuja swala la kuvamiwa mpakani, kiongozi wa nchi(au anayesema kwa niaba ya Raisi) hatakiwi awe na maneno ya kuremba ni kutoa maneno makavu na straight kama Membe,Sitta na Lowassa walivyo tamka.Hii haimaanishi wametangaza vita ila ni maneno ya kawaida kwenye position zao na siasa/diplomasia za kimataifa.Ndo maana hata Malawi hawajaomba msamaha ila wametumia lugha laini kuwa wataendelea na mazungumzo ila hawataacha utafiti maana ni eneo la kwao.Publicly wametunishiana misuri hivyo lakini nakuapia watakapo kaa kuongea, si kama ulivyo sikia waki tunishiana misuri.Hapo kila mtu alikuwa anaonyesha kuwa ni baba mlinzi imara kwa watoto wake hata kama kiukweli hana huo uwezo.
Ninacho furahi kwa viungozi wetu, wametumia maneno mazuri kama vile "Tutatumia kila linalowezekana kuhakikisha kuwa tunatatua matatizo haya kwa njia za mazungumzo (eg mazungumzo ya kiusuluhishi na mahakama) na kama itatulazimu basi jeshi letu limejipanga vizuri sana" Hii ni kauli ya kistaarabu mno lakini ya kiuongozi.Si ya kutangaza vita bali ya kutaadharisha upande wa pili kuwa suluhu ni muhimu sana kwa sababu bila hiyo suluhu kuna option nyingine itakayo tugharimu wote(sisi na malawi)
Kumbuka, kama wamalawi wataachwa waendelee na utafiti, halafu wakaanza kuchimba mafuta na gesi, basi itakuwa ni vigumu sana kuwatoa kwenye mpaka huo maana watakuwa tayari wamesha onja "Black gold (mafuta)"
Sasa huoni kwamba baada ya hizo kauli malawi wameanza kulegeza kamba na wamesha anza kutuliza raia wake kwa kuwaambia wewe watulivu maana serikali yao itafanya mazungumzo na serikali ya TZ?
Maana siku chache hapo nyuma tulipata shida sana kwa sisis tulio na access ya kufika malawi na kufanya nao mawasiliano ya mara kwa mara nao.Wengi wa Raia walikuwa wana tutukana sana na kueleza jinsi jeshi la malawi nililvyo imara na kwamba wako tayari kwa vita.Lakini baada ya kauli hii naona hao hao raia wame "panick"

Nawasilisha Hoja
 
MMM pamoja na maelezo yako fasaha,binafsi naona kama taifa tupo vitani tayari,tena vita kubwa na ghali kuliko vita ya kugombea mipaka ya ziwa moja tu. adui wetu mkuu kama taifa ni uongozi dhaifu na wa kifisadi wa taifa letu,uongozi unaoamini manunuzi ya magari ya kifahari kwenye barabara mbovu,uongozi unaoamini kwenye starehe kuliko afya na elimu.
Hii vita ni kubwa na ni ghali sana.
Watz tusitamani wa kuombea vita nyingine, tutumie nguvu zetu tulizonazo kwa mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake pale alipo hata ndani ya majeshi yetu ili tushinde hii vita tuliyonayo kwanza,hayo mambo ya mpaka na malawi yaweza subiri ikibidi hata miaka 100 ijayo hadi tumalize na tushinde hii vita inayotukabili kama taifa.
 
Kauli ya Sitta haikuwa kali na ya kuogofya, bali ilikuwa kauli ya -re-assure wananchi wa tanzania usalama wao, na iliongelewa mahali panapostahili, bungeni baada ya suala hili kuulizwa na zaidi akasema kauli rasmi ya serikali itatolewa na waziri wa mambo ya nje.
kauli zisizo faa zimetolewa na watu wawili walio fuatia, Koka la Mdimu na Kamati ya Ulinzi. Mdimu akiwa katika wizara tena inayo shughulikia diplomasia angekuwa mtu wa kwanza kuongelea hilo kuliko kuweka msisitizo wa vita, na mtu anaye kimbilia vita inaonyesha ni mtu dhaifu wa hoja au wa uhalisi wa jambo lenyewe, na si jambo jema kwa kiongozi wa namna hiyo kujaribu kudhalilisha nchi nyingine in public, mambo mengi yange fanyika behind the scene hii ndio inaitwa diplomasia. sasa tunavyo raise tension tunaonekana ni Taifa linalo penda kupigana pigana tu, na kauli ya kamati ya ulinzi na usalama nayo haikupaswa kutolewa,kwani hatujafikia huko? hatujasikia hata risasi moja toka upande wa pili kurushwa au raia au askari wetu kuuliwa au kunyanyaswa au hata vifaa vyetu kuharibiwa, na kama wanavyo sema watu walio karibu na mpakani kila mtu anaendelea na shughuli zake na uhusiano wetu bado upo mzuri kibiashara na kiujirani mwema. nafikiri Raisi anatakiwa kufanya reshufle ndogo huyu wa mambo ya nje ameisha jichafua na hili na kuichafua serikali yetu, na wa kamati ya ulinzi na usalama apewa naye kamati nyingine, na ni vizuri Raisi akatoa kauli iliyo nzuri kushusha hii tension tulio Raise bila sababu yoyote ili kuimarisha uhusiano wetu na watu wa Malawi.kwanza inakuwa ni sawa sawa na kugombania vifaranga ambavyo hata havijazaliwa -mafuta/gesi ya aslia?
 
Mkuu! Isije ikawa plan ya ccm ili kusiwepo uchaguzi 2015? kwa kisingizio cha hali ya hatari? manake lolote linawezekana kwa viongo wa aina ya hata nyasi mtakula?
 
Mwanakijiji nakuunga mkono, mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuunga mkono vita hii ya kipumbavu.Vita ta Kagera Iddi Amini nusra atusamabaratishe, Muulize Kamanda yeyote aliyepigana vile vita atakwambia kuwa Id Amini alikuwa strong, kosa kwamba alikosa nguvu ya wananchi Entebbe na Kampala na vikundi vya waasi wengi waliokuwepo enzi hizo kama Museveni,Obotte na wengineo.WANANCHI WASIWAPE KIBURI VIONGOZI DHAIFU UJINGA WA KUSHABIKIA VITA.
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji umenena vyema, ila kuongea amani si mara zote kuna lead results kuwa amani.Huwezi amini this time CCM wamepiga bao,ingawa sijui kama kweli walipanga hivyo au ni coincidence.

Hawa majirani zetu si wote wana akili timamu, kama wana timamu baso huwa wanazipeleka wanapojua.SI mara moja mipaka huwa majirani wanaingia na kufanya wapendalo na kuondoka, wamekuwa wakifanya jitihada nyingi sana hata kujaribu dilute watu wetu ili wajihalalishie mipango yao mirefu.

Hawa jamaa Lugha ya Vita imekuwepo malawi long time.Na hawa jamaa ndio walikuwa uchochoro wa makaburu kufuata wapigananaji waliokuwa wameweka kambi sehemu mbalimbali Tanzania, Zambia, na hata Mozambique.So nadhani hicho kibarua chao kimewaingia sana kiasi wanajiona kuwa Tanzania ya rais anayeonekana kuwa dhaifu na watu hawezi linda nchi .Pia wanadhani wametushika by surprise.

Nikirudi katika view zangu, Serikali sijui ni kwa woga au intentional wamepunguza tension at least by now.Na hao jamaa walio nyuma ya malawi pengine wamepiga mahesabu wakaona Bora waje Bonga kuchukua mikataba kuliko kuleta vita na wao wajiute pande zote mambo yanasimama au kupewa tabaka lingine.SI unajua tena Wakituboa wanajua china huwa hapati shida tubaka.Wakati waziri Membe akionyesha jumuia ya Kimataifa kuwa sisi bado tupo katika kusimamia Majadiliano.Ghafla akatokea Lowasa ambaye naye si wa serikali ila wanajua alichosema kama Mwenyekiti wa kamati Muhimu na mtarajiwa katika kugombea kupitia CCM.Yaani haina tofauti ya kumpa mtoto kauli ya kumfurahisha mbele ya wageni na kwa ujanja ukampa sura ya mauaji.Then ukamwambia twende nyumbani.

Wamalawi wanapenda vita, wamalawi wanawa judge watanzania kwa kuangalia elimu na maendeleo ya watu walipakana nao wanaona kuwa pengine nchi mzima imechoka hivyo, nchi nzima ina watu wasiokuwa na elimu na pengine wajinga.Hawa vibaraka wa makaburu na wasaliti wa Africa si watu w akuamini sana,pamoja na umasikini wao.Sasa nadhnai ndio kipindi cha Tz kuweka wapelelezi wa kudumu huko na ikibidi tuanze pandikiza viongozi wetu, ili tuje wasignisha mikataba kirahisi na wasije ingia tena kwetu.

MCHEZO HAPA UMEKUWA STICK AND CARROT.Ila Malawi na watanzania wameona stick, wangine wameona carrot.So magamba wameshaonyesha kufanikiwa zuia vita kabla ingawa sijui kama kweli waliplann hivyo, au katika kigugumizi kama cha EPA ,Mh EL akapiga hizo za nishikeni nisimvunje.Jamaa wakapata ujumbe kuwa wakajipange upya au waachane na hiyo habari.SOmetimes kuzuia vita ni kuingia full mkoko, adui mwenyewe akajiulize, au hata kichapo ch amwanzo kimfanye akajiulize kama kuna uwezekano wa kuchinda kwa chochote.
 
sasa hivi hakuna sababu ya kuzungumzia mambo ya military background ya kina Lowassa. Mambo ya kuzungumzia tuna uwezo, vifaa na teknolojia kuweza kupigana na Malawi yanakuja vipi? Diplomasia ambayo mtu kawekewa silaha kichwani ni diplomasia gani? Hamuwezi kuwa na diplomasia kama wote mmelekezeana silaha. La kwanza ni kuweka silaha chini ili kuzungumza.

Wote tunajua Malawi ina jeshi na TZ inajeshi na tunajua kuwa majukumu ya majeshi haya ni kulinda mipaka. Haiitaji watu kuringishiana majeshi.

Kinachofanyika ni kitu cha kawaida kabisa kwenye medani za siasa za kimataifa.Kauli kama hizi zina detterence effect.
Pia hii ni siasa ya kimataifa na tunakosea sana pale tunapoamini kwamba diplomasia inaweza kufanikiwa bila shinikizo.Suala la kuweka majeshi chini au kutoongelea millitary strength pia tutakosea na watu hawaelewi kwamba hata wakati wa vita Diplomasia bado inafanyika
Kutatua migogoro kwa njia ya kidiplomasia kuna:
-Kushawishi kabla ya kufikia hatua ya kutishana
-Kukirimu/kuhonga kwa ushawishi wa raslimali au mamlaka
-Lobbying ya kutafuta sapoti kwa jumuiya ya kimataifa
-Shinikizo la kijeshi au shinikizo la vikwazo vya kiuchumi(coercion)
-Ama vyote kwa pamoja

Pia kinachofanyika ni kuondoa sasa hofu wananchi na kuongeza ari ya jeshi na kama nilivyosema kuleta detterence effect kwa nchi hasimu.Hii ni propaganda ya kidiplomasia na haiepukiki
 
tatizo ni haya matamko ya kulinda mipaka kuwa inajirudia rudia, alicho tamkaa Sitta bungeni ilikuwa inatosha, waziri wa mambo ya nje yeye alipopata nafasi ya kutoa official statement ya serikali alitakiwa kukazia hiyo diplomasia ya kutatua kwa mazungumzo,na kuwepo kwa exit strategy , mfano tukienda mahakama ya kimataifa tukashindwa na wewe ulisema utatumia jeshi itakuaje? pia kumbuka tunazungumzia siku hizi economic diplomacy,sas mtu mnaye pigana nae mtaongea naye nini mambo hayo, tusichukulie Malawi tunaishi nayo sikumoja bali maisha yetu yote. Mbona wao waliweza kumzuia Raisi wao kutoa hotuba na waziri wa mambo ya nje akatoa kauli ya ki-diplomasia, kwamba mazungumzo yanaendelea, hayo ya tarehe 27/07/12 na ujumbe wao wa bunge umekuja. Sasa ni vizuri Raisi wetu akafanya ziara Malawi au akatoa neno kupunguza mumkari huu.
 
Sharti mojawapo ni lazima hawa watatu watoe watoto wao wa kiume kuwa mstari wa mbele ktk vikosi ikiwa tutaingia vitani. Vita si mchezo!
 
Back
Top Bottom