Wanasiasa – hivi ‘ndugu’ lilikuwa na mapungufu gani?

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Huko nyuma wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere watu wote tuliitana ‘ndugu’; raisi aliitwa ndugu raisi, Spika – ndugu spika, mbunge – ndugu mbunge, waziri – ndugu waziri na watu wasiokuwa na cheo chochote cha kisiasa pia waliitwa ndugu – ndugu fulani.
Wabunge wetu kwa kutumia kodi zetu wakajadili mswaada bungeni na kupitisha (sijui kwa faida ya nani na kwa tija ipi?) kuwa wao (wabunge, Spika, mawaziri n.k) waitwe ‘waheshimiwa’ na raisi aitwe’ ‘mtukufu’!!! eti Mheshimiwa mbunge fulani, mtukufu raisi!!

Ikiwa hizo title za mheshimiwa na mtukufu ni za hao wanasiasa je wale wasio katika makundi hayo ya kisiasa walipewa title gani? Kama hao waliotajwa ndiyo waheshimiwa na watukufu basi wasiokuwepo katika makundi hayo ya kisiasa hawaheshimiwi na wala siyo watukufu!
Pamoja na title kubwa kubwa walizo jipa wameendelea kufanya madudu katika uongozi wa nchi yetuHali hii imeleta matabaka makubwa kati ya waheshimiwa na wasioheshimiwa na kuwafanya watu watafute kuitwa waheshimiwa kwa gharama yoyote.
Hivi Title ya ‘ndugu’ kwa wanasiasa ilikuwa na mapungufu gani?
 
Back
Top Bottom