Wanasheria wa serikali: Ni hujuma au hamjui kazi yenu??

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Napata shida shida sana kuelewa kwamba inakuwaje serikali inapoteza kesi nyingi sana ambazo inafungua na kusimamiwa na wanasheria wake? Achilia mbali hizi za kifisadi angalia kesi za akina Zombe, Mungai na sasa Mwakalebela!

Sisemi kwamba nataka hawa jamaa wafungwe, la hasha! issue ni kwamba kesi hizi (mfano ya Mungai na Mwakalebela) eti zimefutwa kwa sababu kuna vipengele vya sheria havikufuatwa wakati wa kufungua kesi..

Haiingii akilini, ni vipengele gani ambavyo wanasheria binafsi wanavijua lakini nyinyi wa serikali hamvijui?? Hii ni aibu kubwa kwenye tasnia nzima ya sheria!

Sijui wadau wengine mnalionaje hili...Mi nahisi ni hujuma inaofanywa na hawa watu!
Naomba kuwasilisha.
 
Last edited by a moderator:
Kuna tatizo Tanzania katika suala zima la Sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) NO 9 ya mwaka 1985 marekebisho ya mwaka 2002.

Inaruhusu Jamhuri kutoa shtaka mahakani kama haina nia ya kuendelea na shtaka hilo au inaruhusu hakimu kufuta shtaka hilo kwa kifungu cha 225(5) kama siku 60 zimepita na upelelezi haujakamilika.

Sasa haingii akilini mtu anapekekwa mahakamani wkt upelelezi haujakamilika inaashiria nini?

Kimsingi polisi wanatakiwa kukamilisha upelelezi ndio wamfikishe mtu mahakani kama nchi za wenzetu,Tanzania bado tunatumia mfumo wa kizamani ukituhumiwa tu unapelekwa mahakani upelelezi utakamilika huko huko ndio maana kesi nyingi wanashindwa.

La pili kwa wakili wa serikali anapaswa kujua namna ya kuandaa hati ya mashtaka,Kwa ishu ya Mwakalebela hati ya mashtaka ilikuwa batili kuchanganya sheria mbili kwenye hati moja ya mashtaka kwa hapo lazima kesi hiyo ifutwe.

PIa wanakurupuka kufungua kesi bila kuwa na ushahidi wa kutosha nk nk kwa hivo tuna kasi kubwa mbele yetu.
 
Last edited by a moderator:
Mode nimetafuta Kule kwenye Kona ya Sheria lakini sijapaona: Naomba niweke hoja yangu hapa!
Napata shida shida sana kuelewa kwamba inakuwaje serikali inapoteza kesi nyingi sana ambazo inafungua na kusimamiwa na wanasheria wake? Achilia mbali hizi za kifisadi angalia kesi za akina Zombe, Mungai na sasa Mwakalebela!
Sisemi kwamba nataka hawa jamaa wafungwe, la hasha! issue ni kwamba kesi hizi (mfano ya Mungai na Mwakalebela) eti zimefutwa kwa sababu kuna vipengele vya sheria havikufuatwa wakati wa kufungua kesi..Haiingii akilini, ni vipengele gani ambavyo wanasheria binafsi wanavijua lakini nyinyi wa serikali hamvijui?? Hii ni aibu kubwa kwenye tasnia nzima ya sheria!
Sijui wadau wengine mnalionaje hili...Mi nahisi ni hujuma inaofanywa na hawa watu!
Naomba kuwasilisha...

Kuna kitu kinaitwa "Due Process" (An established course for judicial proceedings or other governmental activities designed to safeguard the legal rights of the individual), Jaribu kusomasoma kwenye mtandao kuhusu hii kitu. Breach of Due process ni moja ya sababu kubwa ya kupiga chini mashitaka.
For entertainment and learning purposes, tafuta series inaitwa "The Practice" hasa season 4, 5, 6 and 7. Utaona kesi ambazo zinaonekana ziko wazi lakini zinapigwa chini kwa ajili ya "due process" na mambo mengine ya kisheria.
 
Hakuna motisha, bora liende, mishahara kiduchu, wana njaa hao usipime tofauti na mawakili binafsi ambao kwao million moja sio shida.
 
Ni ujinga na visa vya serikali ya CCM hususani kinapowadia kipindi cha uchaguzi! Walishawahi kumfunga Ismail A. Rage ili ampishe Prof. Kapuya alipoonekana ni threat kwake hali kadhalika kwa Mwakalebela kwa mama Monica Mbega lakini yeye hakufungwa bali kesi yaken imetupiliwa mbali!
 
issue ya msingi ni hii, je, ni kweli wanafanya kwa bahati mbaya kwasababu hawajui sheria, au wanajua sheria lakini wanafanya makusudi kwa kumfeva accused, kumpa mianya ya kushinda kesi hata kama atapelekwa mahakamani kwasababu labda wamepewa kitu kidogo? kwa uelewa wangu ni kwamba,ni mawakili wa serikali wachache sana waliofanya kazi walau miaka 5, ambao wanaweza kushindwa kufanya vizuri mahakamani. ukiona amefanya hivyo ujue kafanya makusudi kwa maslahi yake. hii pia wanaifanya mahakimu sana, anachukua rushwa halafu anamfunga mshitakiwa, lakini katika mwenendo anajua ameenda kinyume sehemu fulani hivyo mchitakiwa hata kaifungwa hata mwaka unaweza usiishe atakata rufaa na mahakama ya juu itamtoa. ni hakimu huyo wa chini alitengenenza mazingira ya mchitakiwa anayefungwa akatokee juu, na anakuwa amechukua rushwa.

wengi huwa wanasema ati, mtu kama unapenda rushwa hata upewe mshahara gani na marupurupu gani huwezi kuacha. ukweli ni kwamba, ni watu wachache sana wataendelea kula rushwa kama mazingira ya kazi yameboreshwa na ni supportive. WAKILI WA SERIKALI ambaye mshahara wake mdogo, hana hela, unampa kuendesha kesi ya mtu mwenye hela, ni wachache sana wanaweza kuacha hiyo rushwa kwasababu kwanza wanajua hata wasipochukua hawafaidiki chochote na serikali. cha msingi serikali iwaongenzee maslahi, iwajali na kuwalinda ili waione hiyo kazi ni mahali pa kutafuta maisha na si pa mateso tu. kwasasahivi, mawakili wengi wa serikali wapo pale kutafuta madili tu na dili hata kama la rushwa likitokea haachi kwasababu wana ukata sana. hiyo ofisi ni chungu mno, nilishafanya kazi huko, ni chungu mno. ukiwa na roho ndogo unaacha kazi mwaka mmoja tu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom