Wanasheria na Ufisadi na Mikataba mibovu, je bado tunawahitaji?

gollocko

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
2,945
2,275
Leo katika gazeti la majira imeripotiwa kuwa serikali iliingia mkataba na kampuni ya utafutaji gesi ya Pan African Energy Tanzania Limited ili kutafuta gesi hapa nchini na katika mkataba huo CAG (Mkaguzi mkuu wa serikali) amegundua kuna kiasi kimeongezwa kimakosa kinachofikia dola za kimarekani mil.28.

Huu ni mwendelezo wa mikataba mibovu ambayo hulalamikiwa kila kukicha hapa Tanzania na karibu kila wizara au idara za serikali kuna utitiri wa mikataba mibovu. Cha kushangaza tuna utitiri wa wanasheria na mikataba yote hii wanasheria huusika kwa asilimia kubwa!

Sasa najiuliza baada ya ufisadi wote huu kwenye mikataba tunayoingia kila kukicha hapa nchini bado tunahitaji wanasheria kweli?
 
tunawahitaji sana,

kinachotokea wanashauri vizuri lkn mikataba inaenda kuchakachuliwa mbele ya safari

ww jiulize nani anashuhudia mikataba hiyo, je ni yule aliyeshauri au mwingine
 
Back
Top Bottom