Wanasayansi Waja na Mpya - Nyama Zatengenezwa Maabara

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080


3667058.jpg

Nyama za maabara ziko njiani Thursday, December 03, 2009 1:30 AM
Kwa mara ya kwanza wanasayansi wamefanikiwa kutengeneza nyama katika maabara na wanatarajia baada ya miaka mitano ijayo watu wataacha kuchinja ng'ombe na wanyama wengine na kuanza kula nyama zitakazotengenezwa kwenye maabara. Wanasayansi wa nchini Uholanzi wanatarajia baada ya miaka michache ijayo watu wataacha kuwachinja wanyama kwaajili ya nyama zao na wataanza kula nyama zitakazotengenezwa kwenye maabara.

Wanasayansi hao wamefanikiwa kutengeneza nyama ya nguruwe kwa kutumia seli za nyama ya nguruwe.

Kwa hatua waliyofikia sasa, nyama ya nguruwe iliyotengenezwa maabara iko katika hali ya utepe tepe lakini wanasayansi wanatarajia ndani ya miaka mitano ijayo wataweza kutengeneza steki ya nyama ya nguruwe na nyama za wanyama wengine kwenye maabara.

Hakuna mtu aliyeionja nyama hiyo iliyotengenezwa maabara lakini inatarajiwa kuwa miaka michache ijayo nyama za maabara zitakuwa katika ubora wa hali ya juu kiasi cha kwamba watu wataacha kuwachinja ng'ombe na wanyama wengine kwaajili ya nyama zao.

Makundi ya watetezi wa wanyama wameifurahia habari hii na wamesema kuwa hawatakuwa na mzozo tena iwapo wanyama hawatauliwa kwaajili ya nyama zao.

"Nyama hizi zitaokoa uchafuzi wa mazingira na kama zitakuwa na ladha kama nyama halisi watu watakuwa wakizinunua", alisema Profesa Mark Post, wa chuo kikuu cha Eindhoven University ambako utafiti wa nyama za maabara unaendelea.

Nyama za maabara zitawaokoa mamilioni ya wanyama kuchinjwa kwani seli kutokana na nyama za mnyama mmoja zitatumika kwenye maabara kutengeneza kiasi kikubwa cha nyama ambacho kingepatikana iwapo mamilioni ya wanyama wangechinjwa.

Mradi wa nyama za maabara unafadhiliwa na serikali ya Uholanzi na umepata nguvu zaidi baada ya wanasayansi hao kufanikiwa kutengeneza nyama za samaki kwenye maabara.
 
Back
Top Bottom