Wanasayansi Wagundua Kondomu ya Majimaji Kwaajili ya Wanawake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
2833198.jpg

Monday, August 17, 2009 12:41 PM
Timu ya wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza kimiminika kitakachokuwa kikiwekwa kwenye uke wa mwanamke ili kuzuia ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. Wanasayansi katika chuo kikuu cha Utah nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza kimiminika kitakachokuwa kikitumika kama kondomu kwaajili ya kuzuia ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.

Kondomu hiyo ya kimiminika ina uwezo wa kunasa vijidudu vyote vyenye ukubwa kuanzia nanomita 50 na kuendelea. Hii inamaanisha kuwa mbali na kuzuia virusi vya ukimwi, pia zina uwezo wa kuzuia vijidudu vidogo sana vinavyosababisha ugonjwa wa papilloma.

Kondomu hiyo ya kimiminika kama mafuta jinsi inavyotumika ni hivi: mwanamke atachukua kimiminika hicho na kukiweka kwenye uke wake.

Kimiminika hicho kinapokutana na majimaji ya uke ambayo huwa na kiwango fulani cha tindikali, kimiminika hicho hubakia katika hali yake ya kawaida kama kimiminika lakini mbegu za kiume zinapoingia hubadilisha kiwango cha tindikali kilichokuwepo na kukifanya kimiminika hicho kibadilike umbile lake na kuwa kitu kigumu ambacho huzizunguka mbegu za kiume.

Baada ya tendo la kujamiiana kuisha na kiwango cha tindikali kwenye maji maji ya uke kurudia kwenye kiwango chake cha asili, mabaki ya kimiminika hicho hutoka.

Kwa mujibu wa wanasayansi hao, kimiminika hicho kitasaidia kuzuia mimba na magonjwa mengine ya kuambukiza ya zinaa.

"Tumetengeneza kondomu hizi za kimiminika ili kuwawezesha wanawake kujilinda na HIV bila kuwaomba wanaume zao wavae kondomu" alisema Patrick Kaiser, kiongozi wa timu ya wanasayansi iliyogundua kimiminika hicho.

"Kondomu ya kimiminika" bado ipo kwenye majaribio kwenye chuo kikuu hicho na itachukua miaka kama mitatu kabla ya kuanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu.

Wanasanyasi hao kwa sasa wanajaribu kuweka madawa ya kuzuia ukimwi kwenye kimiminika hicho ili kuongeza ufanisi wake.

Lengo la mradi wa kondomu hizo za kimiminika ni kuwawezesha wanawake katika nchi masikini za dunia ya tatu kuweza kupata kitu cha kujilinda na magonjwa ya zinaa kwa bei nafuu.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2833198&&Cat=2
 
Back
Top Bottom