Wanapotwanga kwa mbwembwe!

wanajaribu kutenegneza mazingira wasichoke pale ndio maana wanaimba na kujiburudisha pale wakati wa kutwanga maana sisi kijijini tunavuna mpunga kwa kwenda mbele enzi hizo kulikuwa machine za kusaga utata kwa hiyo ili mle ubwabwa lazima mpunga utwangwe ilikuwa burudani kinu kimzungukwa na masista kama watatu au wawili utafurahi mwenyewe
 
Kama ni nafaka kwenye kinu kikubwa basi huweka maji ili kukoboa na kuhakikisha nafaka inatoka vizuri.TAHADHARI..usizidishe maji maana nafaka badala ya kutoka unga, itatoka urojo na utapata hasara. .

Hii yawezekana ni mojawapo ya mijadala mikubwa sana kati ya watwangaji; wengine wanapenda kuweka maji mengi kwa sababu labda wanafikiria inaharakisha kukoboa lakini wanasema maji kidogo ndio mazuri kwa sababu kama uliyoitoa..
 
Lakini pia nimejiuliza kwanini wengi wanapenda kutwanga wawili wawili? Kwani kutwanga mtu mmoja pekee hakunogi au kutaondoa ladha yake. Manake ni kama punda hawawafanyi kazi mmoja mmoja hadi wawe wawili.
 
@ MMkjj post 62
Una uhakika hili ni jukwaa sahihi? anyway wahusika mtajua.
Unaposema watu wanaweka maji mengi wakitwanga, inategemea unachakatua nini.Kama ni mahindi ya makande au unakoboa kahawa basi maji mengi ni lazima maana baada ya hapo unahitaji kuanika yakauke. Kama unatwanga upate unga..kamwe hutaweka maji mengi.
 
Kama watwanga Kisamvu inakuwaje?
 
halaf mjini sku hizi kumeingia blender, hawataki tena kinu na mchi. dah! ama kweli tanzania tunahitaji katiba mpya.
 
Back
Top Bottom