Wanapotwanga kwa mbwembwe!

nafikiri ni kazi ngumu .. so kuletwa mbwebwe ni kuirahisisha kidogo na kujaribu kuondoa ile notion ya kufanya kazi ngumu na kuenjoy.. nimeshawahi kuona watu wakitwanga mpaka wanabadilishana mitwangio .. na wanafanya kwa ustadi mkubwa sana ... its interesting to the eye .. wanaimba .. ila ni ways za mababu zetu maana hata kulima .. like community work .. nyimbo hutawala just to eeeez the work
 
Hivi kwanini kina dada wengine wakati wanatwanga, wanatwanga kwa mbwembwe na kupiga makofi kabisa? WEngine wanaimba na nyimbo na miguno juu; haiwezekani kutwanga tu vikaisha? Nazungumzia kutwanga nafaka ambazo zinahitaji wakati mwingine unyunyizie maji ili zitwangike vizuri.

Nimeyaona haya kijijini. Wanaofahamu huu ufundi wa kutwanga.

fumbo mfumbie mjinga................. mwerevu......................................
 
Kwa kweli ni hoja nzito sana; maana nadhani kuna utaalamu fulani unahusika. Watwangaji wanaojifunza utaona wanavyong'ang'ania mtwangio utadhani utawakimbia; lakini wataalam wanaweza hata kupiga soga huku wanatwanga....
Wanajipa rythm ya kazi. Kutwanga sio rahisi, ili kupunguza uzito wa kazi, makofi yale yanawapa ka muziki fulani na hivyo kuwapa stamina ya kuendelea na kazi. Ni kama kuimba ukikimbia mchakamchaka.
 
Sijui wengine mnazungumzia vitu gani lakini miye nazungumzia kutwanga kutwanga naona wengine mmenda mbali kweli! .. hii fasihi

Sasa utatwangaje kimya MMM kama umelazimisha chakula chako unaandaa kwa ajili yako mwenyewe shurti ufurahie mavuno
 
Maji yanayoongezwa baada ya kutwanga ni kazi gani?[/FONT]
Sio maji yanaongezwa, bali ni vitone vya maji huyuyiziwa wakati wa process ya kutwanga toka stage ya kukoboa hadi kutwanga unga ili vumbi la unga lisipeperuke, hayo matone ya maji ni kuongeza kuhesiwe na kupunguza vumbi, hata kule kusaga mashineni, maji huongezwa kidogo.

Ila pia kuna utaalamu wa kushika mchi, ili kuuzua usiteleze, watangwaji hutemea mate kigogo na kufikicha mikono ili kuzuia friction kati ya mchi na mkono.

Nimeamini kweli, Mzee Mwanakijiji, ni mwanafasihi, sio tuu anazama ngenye ngeli, mashairi, nahau na tamathali za semi, bali pia azama kwenye kuzungumza kwa dhana!. Jamaa ni fanani!.
 
mm nafikiri wanaonyesha ufundi wao, maana kijijini mara nyingi mziki ni nadra, so
they intertain themselves, ila kuna ambao hata wanakata kata kiuno nakwambia, basi tu
nawaombea furaha

But also to fill in men psychological love vacuum!
 
...wengine hutwanga wakisikilizia, ...wengine hutwanga kwa vishindo!
 
Mwanakijiji, we mambo ya vijijini wayaleta hapa Mjini??, huko huko na mitwango yako!!!!, sisi huku twasaga!!!!
 
Nilikuwa nautafuta wimbo huu kwa siku nyingi sana. Kumbe Mshikaji Tizedboy kashauweka kwenye youtube. Nashukuru sana ingawa umechanganya topic.

Nilikuwa siku zote nikisikia wimbo wa Koffi Olomide, basi unanikumbusha huu wa kiu ya jibu.

Kuna sehemy zinafanana sana sana utafikiri mmoja kaiga mwingine. Ila Sikinde walianza kuimba.

Last edited by a moderator:
Sijui wengine mnazungumzia vitu gani lakini miye nazungumzia kutwanga kutwanga naona wengine mmenda mbali kweli! .. hii fasihi

Mwenzetu Mmkjj kwani wewe unazungunzia kutwanga kupi maana kutwanga ni kutwanga tu. Pamoja na kwamba siku hizi mashine za kusaga zimetapakaa nchi nzima thanks to IGA ( Income Generating Activities) project au miradi ya kupunguza umaskini, bado kuna raha ya kula chakula cha nafaka za kutwanga mwenyewe hasa kama unataka kutwanga kiasi kidogo tu. Kwa wale wadada au wamama au hata wakaka/wababa wanaotwanga wanatumia ufundi kuhakikisha.kinachotwangwa hakirukiruki. Mfano kama unatwanga vitunguu swaumu kwenye kinu kidogo shurti utie chumvi kidogo. Kama ni nafaka kwenye kinu kikubwa basi huweka maji ili kukoboa na kuhakikisha nafaka inatoka vizuri.TAHADHARI..usizidishe maji maana nafaka badala ya kutoka unga, itatoka urojo na utapata hasara.

KAZI yeyote ile shurti uitafutia namna ya kuifurahia. Hata maofisini mtu huweka mziki umsindikize ili kupunguza shurba. Kadhalika wakina dada wanapotwanga huweza kuimba na kupokezna kwa kurusha na kudaka mitwangio yao kama namna ya kuifurahia kazi.Ndio utamaduni ulivyo.Waaafrika kazi huendana na nyimbo au ngoma.
 
...ha ha ha WoS!,
mbona umeadimika hivyo?!...
Kwa kuongezea,
Mortar_and_Pestel.summ.jpg
Kila kinu na mtwangio wake.
 
Mzee wa kijiji, kwa kweli hata mimi nimeshtushwa na uwepo wako mahali hapa! Ni kama kumuona mwalimu mkuu darasani ile vap! afu mlikuwa mnapiga kelele.
Anywei,
KWa kweli kutwanga kwahitaji utaalamu na mbinu za kujikip busy. Nakumbuka nikienda kulima, tunalima huku ukiimba, tunalima kila mtu na mstari wake, tunalima weee kila mtu na jembe lake..kamwe hambadilishani! walitumia vyema jembe lako, waongeza utundu hapa na pale, wasimama, wainama, walima kiupande upande, tena wasimama tena..wasonga..kuna wakati wajisikia kuchoka basi washusha jembe (au sijui lashuka lenyewe)..wapumzika. Kuna wakati wahisi kama mikono imekauka, basi watilia mikono mate na kazi yaendelea.
Kila mtu kwa jembe lake..
wakati fulani mtaitana, "Aisee nanii" waendeleaje huko kwako..wengine wako mstari wa tano wengine wa pili na siye wakukua hata wa kwanza na tumechoka vilivyo...jembe limeanguka! limekataa kuinuka hata kwa kulishika na kulazimisha kulima..lol!
Mwanakijiji, nadhani hivyo ndo huwa kwa kutwanga...
ni jambo zuri ukilima na kamziki cha taratibu kutoka kwenye karedio kako ka mkulima..ila ndo ivo kwa wa huko kwenu kijijini labda ata kamukulima akuna...so inabidi mtunge rhythm zenu. Labda we waimba mwenzio yuaweka beat..all in ni ili kazi iende, inoge na msichoke haraka.
Na huko ndo kulima kwetu!!!
 
Nilikuwa nautafuta wimbo huu kwa siku nyingi sana. Kumbe Mshikaji Tizedboy kashauweka kwenye youtube. Nashukuru sana ingawa umechanganya topic.

Nilikuwa siku zote nikisikia wimbo wa Koffi Olomide, basi unanikumbusha huu wa kiu ya jibu.

Kuna sehemy zinafanana sana sana utafikiri mmoja kaiga mwingine. Ila Sikinde walianza kuimba.

Nimichanganya wapi na wewe, ujui kuwa mwjj anakiu ya jibu, kuhusiana na wanaotwanga kwa mbwembwe!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom