Wanaowania Ubunge EAC toka CCM hawa hapa...

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Vijana CCM wachangamkia Ubunge EAC

Leon Bahati | 22 March 2012 | Mwananchi

WANACHAMA 32 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejitokeza kuwania nafasi nane za Ubunge wa Afrika Mashariki kupitia chama hicho tawala, wengi wao wakiwa ni vijana.

Kwa kawaida kila nchi mwanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), hutoa wabunge tisa kwenye bunge hilo maalumu kwa ajili ya kujadili masuala nyeti.

Hapa nchini mchakato wa kuwapata wabunge umeanza na Ofisa Uchaguzi wa CCM, Rojas Romuli alithibitisha kuwa tayari wanachama 32 wameshachukua fomu kuwania nafasi za kuteuliwa na chama kwenye nafasi hizo.

Ingawa Romuli alikataa kuitaja orodha kamili ya waliochukua fomu hizo jana, habari za uhakika zilithibitisha majina ya watu kadhaa ambao walichukua fomu hizo.

Miongoni mwao ni pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, James Ole Milya na Dk Zainab Ghama ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kibaha Mjini.

Wengine wanaodaiwa kuchangamkia fomu hizo ni Dk Richard Kasunda, Janet Milya, Baraka Kange, John Ng'ongolo na Balozi Christopher Liundi.

Kwenye orodha hiyo pia wapo wabunge wawili wa Afika Mashariki waliojitokeza kutetea nafasi zao ambao ni Dk Aman Kabourou na Janet Mmary.

Romuli alikiri majina hayo kuwamo kwenye orodha hiyo , lakini akasisitiza kuwa chama kinawataka wanachama wengi zaidi kuendelea kujitokeza ili kuongeza ushindani.

Alisema kwenye orodha hiyo ya watu 32, wanaume ni 26, wanawake sita na robo tatu ya waliochukua fomu hizo ni vijana.Alisema mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni kesho jioni na mchakato wa kuanza kufanya mchujo "unatarajia kufanyika mapema iwezekanavyo."

Kulingana na bunge lililopita, Romuli alisema, CCM ilitoa wabunge wanane, watano wakitokea Tanzania Bara na watatu visiwani huku miongoni mwao wanawake wakiwa watatu.

Kwenye bunge hilo, vyama vya upinzani vilikuwa na mbunge mmoja na kwamba mpangilio huo unatarajiwa pia kujirudia tena.

MY OPINION!
Dr Kaborou hana tija, ni bora apumzike ama apumzishwe!
 
Duh!!!! wapi BENO? huyu akiachwa na hapa naona safari yake ya kisiasa ndio imeishia hapa!!!!
 
Wapi wa Zanzibar? kumbuka Bilal alikuwa Mmoja wa hao Wabunge; na pia yupo Mtoto Mwingene wa Mwinyi ambaye ni Mbunge wa East Africa.
 
Duh!!!! wapi BENO? huyu akiachwa na hapa naona safari yake ya kisiasa ndio imeishia hapa!!!!

atagombea uenyekiti UVCCM safari hii zamu ya wabara atapata ingaw aitabidi akampigie magoti Prince RIZ1
 
Yule mtoto wa malecela ameishia wapi tena?! Nakumbuka alisha tangaza nia. Au bado yuko Newyork city?
.

Watu walimsimanga sana humu ndani huyu bwana baada ya kuonesha nia ya kuthubutu.Sasa isijekuwa akawa kavunjika moyo ingawa kwenye siasa zetu za dunia ya tatu ukiwa na moyo wa nyama hutakuja ziweza. Inakupasa uwe na moyo wa chuma na kifua kipana maana majungu,fitina,visa,mizengwe,unafiki n.k vinachukua sehemu kubwa ya siasa zetu.
 
Duh, nimestuka nilipoliona jina la baraka Kange. ni kifisadi papa hicho. Jamaa nimesoma nae India, ametapeli wengi kwa kweli. Hasahasa (freshers) wanafunzi wageni waliokuwa wanakuja kuanza masomo. Na kama mabinti alikuwa anawataka kimapenzi sana. Ili awape msaada, wanapokuwa shida au hawajui information flan.

Hivi CCM huwa wana records za mtu, au huwa wanaokota tu mtu yoyote. Jamaa akipita nitakidharua hiko chama.

Afu nakumbuka jamaa hata degree hakumaliza. Na wala alikuwa haileweki anasoma chuo gani na anaingia darasani saa ngapi. Tulisikia tu amerudi bongo. Jamaa mishemishe na deals nyingi sana.
 
Huo ni ufala mambo ya India na hilo yanahusiana nini!? Watu wengine bana! Ama ulitaka watu wajue ulisoma India!? ACHA HIZO JITOKEZE WEWE BASI TUONE HATA KAMA UTAJADILIWA sanasana utakuwa mmoja wa wale watakaokatwa kabla ya kufika kwenye vikao husika.
 
hahaha, pole Baraka kange, ila mimi nimeongea ukweli. kama ni uongo jitetee mkubwa.
kiukweli watu kama nyie wezi na matapeli mkifugwa na kuletewa mzaha, mtazidi kuangamiza hili taifa letu. ni sawa na hawa kina ADAM MALIMA..... inawezekana wana historia kama yako.

mimi si muumini wa siasa, wala sihitaji kugombania uongozi wowote wa kisiasa....ila kaka CCM wakikuchagua, nitakidharau sana hiko chama... watajihidhirishia kuwa hamna watu wenye nidhamu humo ndani ya chama chenu. mpaka nyie matapeli mnapata nafasi ya kuwawakilisha jamii...duh
 
Duh, nimestuka nilipoliona jina la baraka Kange. ni kifisadi papa hicho. Jamaa nimesoma nae India, ametapeli wengi kwa kweli. Hasahasa (freshers) wanafunzi wageni waliokuwa wanakuja kuanza masomo. Na kama mabinti alikuwa anawataka kimapenzi sana. Ili awape msaada, wanapokuwa shida au hawajui information flan.

Hivi CCM huwa wana records za mtu, au huwa wanaokota tu mtu yoyote. Jamaa akipita nitakidharua hiko chama.

Afu nakumbuka jamaa hata degree hakumaliza. Na wala alikuwa haileweki anasoma chuo gani na anaingia darasani saa ngapi. Tulisikia tu amerudi bongo. Jamaa mishemishe na deals nyingi sana.

Mkuu,

Kuna hii tabia ya baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vikuu ughaibuni kuwapiga majungu wenzao,huu unafiki tu.Pengine mtu anafanya hivyo kwa kuwa yupo nyuma ya KEYBOARD na hawezi kuongea haya wakiwa face to face.Vijana acheni unafiki,tusijenge taifa la hovyo.Kama kuna tofauti ambayo ni personal kati yako na yeye ni better uzimalize nje ya jukwaa hili.Hata hivyo niwatendee haki ya kuwapa benefit of doubt anyways

Tujenge tabia ya kuja na uthibitisho unapotoa tuhuma dhidi ya mtu. Vipi mkuu,unaiheshimu CCM hadi sasa kwa lipi? na ni kwa nini kama huyo jamaa akipitishwa unaona kama vile itakuwa kigezo mojawapo cha wewe kukidharau hicho chama?
 
Back
Top Bottom